Tulipofikia kwa miaka 19 bila Mwalimu Nyerere, Taifa halina dira ya kueleweka na siasa zetu zinaacha njia yake

Thadei Ole Mushi

Verified Member
Oct 13, 2018
27
100
Na Thadei Ole Mushi

Kwa waliozaliwa wakati Baba Wa Taifa anafariki mwaka huu watakuwa wamefikisha umri wa miaka 19. Ni umri ambao kisheria unamtambua mtanzania kama mtu mzima na mwenye maamuzi yake binafsi.

Tafsiri yake ni kwamba toka Mwl Nyerere amefariki hadi leo tumeshatimiza Umri wa kutafakari na kuamua wenyewe kama nchi. Kwa sasa tunapaswa kupevuka kisiasa na kuangalia ni kwa Namna gani tunaweza kujikwamua.

KIUCHUMI.

Toka mwalimu Nyerere atutoke bado kama taifa hatujapata Dira kamili ya kutuongoza tunataka kwenda wapi. Kila awamu inakuja na kauli mbiu yake na wakishaondoka tunaachana nayo tunaanza kauli mbiu nyingine na tunasahau kabisa alichoasisi aliyetangulia.

Mkapa alikuja na sera ya Uwazi na Ukweli japokuwa leo sioni sera hii ikifutwa sana. Kumekuwa na Sintofahamu kwenye vyombo vyetu vya habari aidha kwa kukosa weledi wanashindwa kukidhi matakwa ya kiuandishi na wanashindwa kuisaidia Serikali katika kufikia malengo yao ya kuhabarisha wananchi bila woga. Sera hii tumeifanyia matamga mwaka jaba pale ambapo nchi ilipoamua kujitoa kwenye umoja wa nchinzinazoheshimu uwazi (transparent) katika uendeshaji wa maswala yao.

Kipindi cha Kikwete tulikuja na sera ya Kilimo kwanza. Leo hii kilimo kwanza kipo wapi? Wakulima wengi wa Tanzania ambao ni karibu Robo tatu ya watanzania wote wanalima kilimo cha kujikimu. Yaani unachokilima hata hakikutoshi kwa matumizi ya nyumbani. Je tuna mipango gani na kilimo chetu kwa sasa hivi?

Niliwahi kusema siku moja kuwa nchi zinazotuzunguka kwetu ni fursa tosha kama tutaamua kufanya kilimo chenye tija. Tunaona wenzetu wanavyohangaika kutafuta mahindi tu hapa kwetu..... serikali itengeneze sera itakayowasadia wakulima kulima zao hilo ili tupate cha kutosha na cha kufanyia biashara.

Kwangu kitendo cha kufunga mipaka ili mahindi yasitoke siliungi mkono sana badala yake kwa kuwa fursa hiyo imejitokeza basi Serikali ilazimishe kila mtu kulima kwa nguvu kazi yao ni kuwawekea wakulima mazingira mazuri tu ya kuwapatia pembejeo ili tuchukue hizi fedha za wenzetu chapchap. Kitendo cha kufunga mipaka ni kuzuia akili isifikirie zaidi nini tunachoweza kufanya.

Mh Magufuli kaja na Sera ya viwanda sintoshangaa baada ya yeye kutoka madarakani atakayekuja kuanza jambo lingine.

Taifa linakuwa kila Siku linaandaa sera na kuzifungia kwenye makabati. Lazma sasa tukubali kutumia mipango ambayo tumeshaiandaa na kuifikisha mwisho. Kama ni viwanda basi tuhakikishe dira hii inafika mwisho nk. Si kila mtawala anaingia na sera yake ya Maendeleo.

KISIASA

Kisiasa jambo kubwa tunalohitaji kulifanyia kazi kwa sasa ni kuimarisha Demokrasia yetu. Kama Taifa lazma tukubali kuwa siasa zetu tunataka kuziendeshaje... je ni kwa mfumo wa Kidemokrasi au ni kwa mfumo wa Kifashist.

Kuna dalili ya Siasa zetu kupevuka na kuvuka mipaka ya Kidemokrasia na kuingia kwenye siasa za kimapinduzi. Dalili hizo zipo wazi sana kwa sasa na kama nchi tunapaswa kutupia jicho eneo hili.

DALILI

Crane Brinton katika nadharia yake ya mapinduzi aliyoiandika kwenye kitabu chake cha " Anatomy of revolution" anafananisha mapinduzi na homa. Katika mazingira hayo Brinton anasema homa si jambo la kufurahia na linapaswa kuepukika au kutibiwa kwa mapema pindi dalili za homa hiyo zinapojitokeza.

Kwenye nadharia hiyo Brinton kutokana na uzoefu alioupata kwenye American revolution, France Revolution na British revolution alihitimisha nadharia hii kwa kusema kuwa kuna hatua kuu tatu za taifa kupitia hatimaye mapinduzi kutokea iwe katika mazingira yoyote yale.

Mapinduzi siku zote huanza kwa matatizo ndani ya jamii kujitokeza hatua hii ni ya awali kabisa "pre-Revolutionary"

Tatizo kuu hapa huwa ni Serikali kukosa fedha za kuwahudumia wananchi wake na njia pekee ya kukimbia tatizo hilo ni kuongeze na kuibua kodi mbali mbali kwa wananchi (over taxation).

Hatua ya pili ni criticism hapa ni kundi la wasomi kujitokeza kwa wingi kukosoa mfumo wa utawala uliopo. Katika revolutions zote duniani zilizowahi kutokea katika kipindi ambacho serikali huonekana udhaifu wake ni wakati huu ambao kundi la wasomi wataanza kuwakosoa watawala.

Ukosoaji huu ukizidi serikali hutumia nguvu ya Dola kudhibiti wakosoaji hao kwa kuwakamata na kuwafunga au kuwaweka kizuizini.

Baadaye Polisi na Jeshi hukataa kutumika kutetea maslahi ya watawala na kuungana na wananchi. Iliwahi kutokea kwenye mapinduzi ya Misri na mapinduzi ya Rusia. Kule ufaransa utawala vyombo vya Dola vilishindwa kuwadhibiti waandamanaji. Kule Ivory Cost Ghabo alikatwa makofi mbele ya mke wake na waliokuwa wakimkinda.... mara nyingi taifa likifikia hatua hii huwezi kuyazuia tena mapinduzi hayo.

Katika hali ya kawaida kwa sasa ni kama yanaanza kujitokeza hapa kwetu. Tumeanza kuinyemelea hatua ya pili kwa sasa ni Lazma tukubalibkubadilika kabla ya hatua ya tatu haijajitokeza.

Mapinduzi ni "hope" (Matumaini) watu wakianza kujenga Imani kuwa wanaweza wanaweza kweli. La msingi ni kutafuta njia ya kuwafanya wasianze kujenga hiyo Imani.

Mfalme wa Ufaransa alikuwa akiwashangaa wananchi wake wanakosaje mkate wakati yeye anakula Keki....

Tumesikia Katibu mkuu was CCM akidai kuwa wananchi hawataki tena kupiga kura kwa kuwa uchaguzi kwao ni kama kituko. CCM aliyoiacha mwalimu Nyerere si hii inayoendeshwa na kina Polepole. CCM ya Nyerere iliheshimu katiba yake. Kwa sasa hapa kwetu mtu anajiuzulu toka Chadema akihamia CCM anapewa tena jukumu la kugombea. Niliwahi kusema kama CCM Ikiamua Leo uchaguzi wa marudio uwe mwisho inawezekana. Hakuna mbunge ambaye yupo tayari kujiuzulu kuhamia chama kingine kama hajui kuwa huko anakokwenda anaenda kupewa tena nafasi, CCM ndio inayochochea hii hama hama.

KIJAMII

Kijamii hapa nitaongelea mambo mawili tu nalo ni umoja wa kitaifa. Vyama na makabila yetu yanataka kututoa kwenye mstari. Kwa siku za karibuni watu wanajitambulisha kwa makabila yao.

Vyama vyetu vinajigawa kikanda, minongono inazidi kuwa kuna upendeleo jambo ambalo siliamini sana.

Kwa mara ya Kwanza baraza la mawaziri linatoka ikalazimu watu kutoa ramani ya Tanzania inayoonyesha mikoa na mgawanyo wa mawaziri. Hii ni ladha mpya inayoanza kuingia kwenye siasa zetu.

Wengine wananongona kuna wanaopendelewa wenye kosa linalofanana mmoja anaadhibiwa mwingine anaachwa. Tunamuenzi kwa Namna gani mwalimu Nyerere? Katika kumbukizi hii ya Mwalimu Nyerere hebu tuwalete watanzania pamoja. Sisi sote ni Ndugu kama ni Kucheka tucheke wote na kama ni Kulia tulie wote haki huliinua Taifa.

Jambo la pili tuangalie sheria zetu zinawasaidaje wananchi kufurahia nchi yao. Ni kweli kuwa Bomoa Bomoa inafuata Sheria ila si vibaya tuakachanganya sheria hiyo na busara. Angalieni familia zinazotoa machozi watu wamekopa na kuwekeza katika ujenzi leo hii wanapondeka moyo mno. Wakati wakijenga Serikali ilikuwepo na kuna watu walikuwa wakilipwa kwa ajili ya kuwashauri hawa watu waliokuwa wanajenga.

Kwa kuwa mm ni Mgeni kwenye ukurasa huu kwa Leo acha niishie hapa...

Ole Mushi
0712702602
FB_IMG_1539497853491.jpeg
 
Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
1,993
2,000
Nyerere alifariki 1999
Huduma mbovu za Afya,Elimu,maji,,umasikini,katiba isemayo Diwani na mbunge anapingika mahakamani ISIPOKUWA RAISI . Vyote hivi havikuanza kuwepo kuanzia 2000.
 
ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,459
2,000
Tunako elekea nchi yetu Tanzania ni neema tu kwa wale wanao itakia mapenzi mema, play your part brother!
Na kwa wale wanao itakia mabaya nchi yetu watakufa wote pamoja na kizazi chao walahi
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,497
2,000
Tunako elekea nchi yetu Tanzania ni neema tu kwa wale wanao itakia mapenzi mema, play your part brother!
Na kwa wale wanao itakia mabaya nchi yetu watakufa wote pamoja na kizazi chao walahi
Hizi ajali zinaua watu wa maana wanabaki mazwazwa.
 
Sungusela

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
682
500
Na Thadei Ole Mushi

Kwa waliozaliwa wakati Baba Wa Taifa anafariki mwaka huu watakuwa wamefikisha umri wa miaka 19. Ni umri ambao kisheria unamtambua mtanzania kama mtu mzima na mwenye maamuzi yake binafsi.

Tafsiri yake ni kwamba toka Mwl Nyerere amefariki hadi leo tumeshatimiza Umri wa kutafakari na kuamua wenyewe kama nchi. Kwa sasa tunapaswa kupevuka kisiasa na kuangalia ni kwa Namna gani tunaweza kujikwamua.

KIUCHUMI.

Toka mwalimu Nyerere atutoke bado kama taifa hatujapata Dira kamili ya kutuongoza tunataka kwenda wapi. Kila awamu inakuja na kauli mbiu yake na wakishaondoka tunaachana nayo tunaanza kauli mbiu nyingine na tunasahau kabisa alichoasisi aliyetangulia.

Mkapa alikuja na sera ya Uwazi na Ukweli japokuwa leo sioni sera hii ikifutwa sana. Kumekuwa na Sintofahamu kwenye vyombo vyetu vya habari aidha kwa kukosa weledi wanashindwa kukidhi matakwa ya kiuandishi na wanashindwa kuisaidia Serikali katika kufikia malengo yao ya kuhabarisha wananchi bila woga. Sera hii tumeifanyia matamga mwaka jaba pale ambapo nchi ilipoamua kujitoa kwenye umoja wa nchinzinazoheshimu uwazi (transparent) katika uendeshaji wa maswala yao.

Kipindi cha Kikwete tulikuja na sera ya Kilimo kwanza. Leo hii kilimo kwanza kipo wapi? Wakulima wengi wa Tanzania ambao ni karibu Robo tatu ya watanzania wote wanalima kilimo cha kujikimu. Yaani unachokilima hata hakikutoshi kwa matumizi ya nyumbani. Je tuna mipango gani na kilimo chetu kwa sasa hivi?

Niliwahi kusema siku moja kuwa nchi zinazotuzunguka kwetu ni fursa tosha kama tutaamua kufanya kilimo chenye tija. Tunaona wenzetu wanavyohangaika kutafuta mahindi tu hapa kwetu..... serikali itengeneze sera itakayowasadia wakulima kulima zao hilo ili tupate cha kutosha na cha kufanyia biashara.

Kwangu kitendo cha kufunga mipaka ili mahindi yasitoke siliungi mkono sana badala yake kwa kuwa fursa hiyo imejitokeza basi Serikali ilazimishe kila mtu kulima kwa nguvu kazi yao ni kuwawekea wakulima mazingira mazuri tu ya kuwapatia pembejeo ili tuchukue hizi fedha za wenzetu chapchap. Kitendo cha kufunga mipaka ni kuzuia akili isifikirie zaidi nini tunachoweza kufanya.

Mh Magufuli kaja na Sera ya viwanda sintoshangaa baada ya yeye kutoka madarakani atakayekuja kuanza jambo lingine.

Taifa linakuwa kila Siku linaandaa sera na kuzifungia kwenye makabati. Lazma sasa tukubali kutumia mipango ambayo tumeshaiandaa na kuifikisha mwisho. Kama ni viwanda basi tuhakikishe dira hii inafika mwisho nk. Si kila mtawala anaingia na sera yake ya Maendeleo.

KISIASA

Kisiasa jambo kubwa tunalohitaji kulifanyia kazi kwa sasa ni kuimarisha Demokrasia yetu. Kama Taifa lazma tukubali kuwa siasa zetu tunataka kuziendeshaje... je ni kwa mfumo wa Kidemokrasi au ni kwa mfumo wa Kifashist.

Kuna dalili ya Siasa zetu kupevuka na kuvuka mipaka ya Kidemokrasia na kuingia kwenye siasa za kimapinduzi. Dalili hizo zipo wazi sana kwa sasa na kama nchi tunapaswa kutupia jicho eneo hili.

DALILI

Crane Brinton katika nadharia yake ya mapinduzi aliyoiandika kwenye kitabu chake cha " Anatomy of revolution" anafananisha mapinduzi na homa. Katika mazingira hayo Brinton anasema homa si jambo la kufurahia na linapaswa kuepukika au kutibiwa kwa mapema pindi dalili za homa hiyo zinapojitokeza.

Kwenye nadharia hiyo Brinton kutokana na uzoefu alioupata kwenye American revolution, France Revolution na British revolution alihitimisha nadharia hii kwa kusema kuwa kuna hatua kuu tatu za taifa kupitia hatimaye mapinduzi kutokea iwe katika mazingira yoyote yale.

Mapinduzi siku zote huanza kwa matatizo ndani ya jamii kujitokeza hatua hii ni ya awali kabisa "pre-Revolutionary"

Tatizo kuu hapa huwa ni Serikali kukosa fedha za kuwahudumia wananchi wake na njia pekee ya kukimbia tatizo hilo ni kuongeze na kuibua kodi mbali mbali kwa wananchi (over taxation).

Hatua ya pili ni criticism hapa ni kundi la wasomi kujitokeza kwa wingi kukosoa mfumo wa utawala uliopo. Katika revolutions zote duniani zilizowahi kutokea katika kipindi ambacho serikali huonekana udhaifu wake ni wakati huu ambao kundi la wasomi wataanza kuwakosoa watawala.

Ukosoaji huu ukizidi serikali hutumia nguvu ya Dola kudhibiti wakosoaji hao kwa kuwakamata na kuwafunga au kuwaweka kizuizini.

Baadaye Polisi na Jeshi hukataa kutumika kutetea maslahi ya watawala na kuungana na wananchi. Iliwahi kutokea kwenye mapinduzi ya Misri na mapinduzi ya Rusia. Kule ufaransa utawala vyombo vya Dola vilishindwa kuwadhibiti waandamanaji. Kule Ivory Cost Ghabo alikatwa makofi mbele ya mke wake na waliokuwa wakimkinda.... mara nyingi taifa likifikia hatua hii huwezi kuyazuia tena mapinduzi hayo.

Katika hali ya kawaida kwa sasa ni kama yanaanza kujitokeza hapa kwetu. Tumeanza kuinyemelea hatua ya pili kwa sasa ni Lazma tukubalibkubadilika kabla ya hatua ya tatu haijajitokeza.

Mapinduzi ni "hope" (Matumaini) watu wakianza kujenga Imani kuwa wanaweza wanaweza kweli. La msingi ni kutafuta njia ya kuwafanya wasianze kujenga hiyo Imani.

Mfalme wa Ufaransa alikuwa akiwashangaa wananchi wake wanakosaje mkate wakati yeye anakula Keki....

Tumesikia Katibu mkuu was CCM akidai kuwa wananchi hawataki tena kupiga kura kwa kuwa uchaguzi kwao ni kama kituko. CCM aliyoiacha mwalimu Nyerere si hii inayoendeshwa na kina Polepole. CCM ya Nyerere iliheshimu katiba yake. Kwa sasa hapa kwetu mtu anajiuzulu toka Chadema akihamia CCM anapewa tena jukumu la kugombea. Niliwahi kusema kama CCM Ikiamua Leo uchaguzi wa marudio uwe mwisho inawezekana. Hakuna mbunge ambaye yupo tayari kujiuzulu kuhamia chama kingine kama hajui kuwa huko anakokwenda anaenda kupewa tena nafasi, CCM ndio inayochochea hii hama hama.

KIJAMII

Kijamii hapa nitaongelea mambo mawili tu nalo ni umoja wa kitaifa. Vyama na makabila yetu yanataka kututoa kwenye mstari. Kwa siku za karibuni watu wanajitambulisha kwa makabila yao.

Vyama vyetu vinajigawa kikanda, minongono inazidi kuwa kuna upendeleo jambo ambalo siliamini sana.

Kwa mara ya Kwanza baraza la mawaziri linatoka ikalazimu watu kutoa ramani ya Tanzania inayoonyesha mikoa na mgawanyo wa mawaziri. Hii ni ladha mpya inayoanza kuingia kwenye siasa zetu.

Wengine wananongona kuna wanaopendelewa wenye kosa linalofanana mmoja anaadhibiwa mwingine anaachwa. Tunamuenzi kwa Namna gani mwalimu Nyerere? Katika kumbukizi hii ya Mwalimu Nyerere hebu tuwalete watanzania pamoja. Sisi sote ni Ndugu kama ni Kucheka tucheke wote na kama ni Kulia tulie wote haki huliinua Taifa.

Jambo la pili tuangalie sheria zetu zinawasaidaje wananchi kufurahia nchi yao. Ni kweli kuwa Bomoa Bomoa inafuata Sheria ila si vibaya tuakachanganya sheria hiyo na busara. Angalieni familia zinazotoa machozi watu wamekopa na kuwekeza katika ujenzi leo hii wanapondeka moyo mno. Wakati wakijenga Serikali ilikuwepo na kuna watu walikuwa wakilipwa kwa ajili ya kuwashauri hawa watu waliokuwa wanajenga.

Kwa kuwa mm ni Mgeni kwenye ukurasa huu kwa Leo acha niishie hapa...

Ole Mushi
0712702602 View attachment 897612
Karibu sana jamvini !
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom