Tulipofika tunahitaji uongozi safi ili tuishinde vita dhidi ya Corona

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
WHO, Kama shirika lenye dhamana ya afya duniani imetambua Corona ni janga la kimataifa. Ikiwa ina maana dunia haitokua salama hadi adui huyu maradhi amethibitiwa duniani kote. Na kwa msingi huo kila nchi lazima ipambane kuchangia dunia kuendelea kuwa mahala salama pa kuishi.

Kimsingi unapotaka kupambana na changamoto iwayo yote inahitaji , maarifa sahii, taarifa sahii, nyenzo sahii (resources) na uongozi safi.

Nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zina mchango mdogo Sana wa kuzalisha maarifa sahii yaliyozalishwa na tafiti, na hivyo kwa sehemu kubwa utegemea mataifa yaliyoendelea, na kupitia shirika la Afya duniani kuzalisha maarifa sahii juu ya Magonjwa mbalimbali. Mara nyingi taarifa hizo zikipokelewa huwa zinakua customized kulingana na context yetu. Kwa njia hii tumefanikiwa kukabiliana na changamoto nyingi za kiafya zilizowahi itikisa dunia Kama Polio, Surua, Ukimwi, Malaria, n.k

Katika vita ya Corona tunamshukuru Mungu kwa jitihada za wanasayansi Kwa kuzalisha taarifa nyingi sahii, ingawa mengi bado hayafahamiki. Katika mazingira kama haya ni mafanikio makubwa Sana na jambo la kheri kufanikisha upatikanaji wa chanjo ndani ya kipindi kifupi Cha mwaka mmoja toka mlipuko wa ugonjwa wa Corona utangazwe.

Ndani ya mwanga huu wa maarifa na taarifa na nyenzo (resources) Kama chanjo bado Kama Taifa tumeshindwa kutoa uongozi wa kipi hasa kifanyike.

Nasema hivyo kwani wote tunashuhudia utofauti na mtanziko wa njia gani tuifuate tunapokabiriana na changamoto hii ya ugonjwa wa Corona.

Wakati dunia kwa sehemu kubwa ikiwa ina amini nguvu na nafasi ya sayansi, jamii nyingine zenyewe nimechukua mlengo tofauti.

Mathalani Taifa letu ni miongoni mwa jamii za kimataifa ambazo sayansi haizingatiwi na badala yake tiba asili na imani kwa Mungu imepewa mwangwi wa kimamlaka. Hata hivyo, Kwa bahati mbaya pamoja na kuchukua mwelekeo huo bado hakuna miongozo iliyo bayana ya namna ya kutekeleza mwelekeo huo.

Tunaposema piga nyungu, je nini hasa maana ya nyungu? nini kitumike as contents? Kwa kiasi gani? Katika stage ipi ya ugonjwa? Kwa njia gani? Marangapi kwa siku ? Kwa muda gani ? nini matokeo yake ya muda mfupi na muda mrefu ?

Tunaposema tumwamini Mungu, je tunamwamini Mungu yupi ? Wa kiprostant au Allah? au mungu wa jadi? Tuna mwamini tukiwa tunafanya nini? Kwa njia gani , mpaka lini? na je Mungu ameweka mashart gani ili ajibu maombi? Je tuko ladhi kama taifa kufuata mashart yake ili ajibu kwa wakati ? na kuhani yupi anatuongoza ?

Ukiona confusion hii utafahamu tunashindwa kuwa na mkakati unaoeleweka wa pamoja katika vita hii na haina shaka ndo maana tunakinzana na kutofautiana.

Inabidi tuelewe nchi hii imejengwa katika misingi ya kikatiba , na katiba imeweka utaratibu wa namna taifa tunapaswa kuishi na kuendeshwa.

Katiba yetu inatambua serikali haina dini ila watu wake wana dini. Na Kuna mgawanyo mzuri kabisaa nini serikalini ifanye na taasisi zingine zikiwemo za dini zifanye ,ila kwa pamoja tutalenga ku-push agenda ya maendeleo ya Mama Tanzania.

Kwa msingi huu Serikali lazima itoe muongozo wa kiuongozi ni njia ipi ifanyike kwa namna ipi na kwa resources zipi. Kupitia wizara ya afya Serikali itoe uongozi kwa kutekeleza na kutiza wajibu kwa mjibu wa sheria, taratibu na miongozo.

Asasi za kiraia zitoe mchango wake wa kiuongozi kati sphere of their operations, na zifanye kwa kufuata guidance za mamlaka kuu ambayo ni serikali.

Taasisi za dini pia zituongoze katika wigo waliopewa wa kikuhani kwa kuzingatia sheria na utaratibu ili kuweza kupambana na adui corona anayetishia utulivu na ustawi wa jamii yetu.

Wananchi pia tuache tofauti za kiitikadi na milengo ya kisiasa. Tushikamane na tutimize wajibu wetu kwa kufuata miongozo na taratibu za kijamii.

Vita hii tunao uwezo wa kuishinda tukiwa na uongozi safi na mshikamano wa pamoja.

Waione viongozi katika nyanja zote

Ni sauti ya mtu aliaye nyikani

2021@production
 
Back
Top Bottom