Tulipo toka!!!!!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,577
8,596
Nakumbuka niliwahi kuazima suruali ya jirani yangu dingriz nikamwambia naenda town siku tuliyo ahidiana sikutokea nikiwa bado naosha na raba za bora nimezipaka chaki zimekuwa nyeupeeee nashati la nylon nimepitisha kamba!!jamaa akashindwa kuningoja akanifata town nakusema mbona haujaja mimi kesho naenda kanisani ilinibidi nikatize ziala nirudi homd nimpe jeans lake!!!!mzisha ya wakati wanyerere!!Jewe we unakumbuka nini wakati wa ngazi 4???ua chacha?au mwishonii wakati wa cordry??
 
wakati huo mtu akivaa VIP, anawaringishia watu, balaa ni pale inapokata uzi wa kati...anastuka iko makwapani kama sidiria.
gari la ugawaji likipita kariakoo mtu analikimbiza mpaka vingunguti ili apate robo kilo ya sukari na kikombe cha bati akh! tumetoka mbali:smile-big:
Na hapo mtu akiwasema vibaya VIONGOZI anasemwa "HUYU NI KIBARAKA sio MWENZETU" maweeeee
 
Duka la kijiji mkoa mzima disgn ilikuwa moja!Duka la RTC!Viberti vinatoka china vya box ya mbao wachina walianza long kutuchakachua!!
 
Enzi hizo tulikuwa tuna ambiwa Dunia nzima hali ni hiyo hiyo, huku wakisema 'Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM, tunaitikia ZIDUMUUU! Baadaye hawakutwambia zisidumu-wakachakachua kimtindo sijui siku hizi dira (Vision) ya Taifa nini?
 
Wakati huo stepller ilikua ikikaa mezni kwa mwalimu mkuu tu na haikua ajabu mwanafunzi kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana kwa kukutwa na kalamu nyekundu..nakumbuka ata nyimbo walizokua wanatufundisha.."chama cha mapiduzi Tanzania...eeeh..chama cha mapinduzi Tanzania eeeh..Nyerere kasema Tuunganishe chama..tuunganishe chama Tanzaniaaa...tumetoka mbali"
 
Nakumbuka redio zile za mkulima (za mbao) tulikuwa tunakwenda kusikiliza kwa balozi wa mtaa. Sukari ikija kwenye duka la kijiji mnapanga foleni mpaka unachoka unaweka jiwe kwanza na pia unalazimishwa kununua na bidhaa nyingine ambazo zilikuwa hazinunuliwi. Nakumbuka pia mashati ya Juliana (yenye picha ya mwewe) ukiwa nalo wewe ni mtu kijijini kwenu. Suala kupaka chaki kwenye raba nimefanya sana. Lol! Kweli tumetoka mbali.
 
Perfume ya YOLANDA na YUU... Siku ya Disko basi tunaazimana bweni zima toka kwa mchizi mmoja mtoto wa mwenyekiti wa CCM wa wilaya. wakati huo nguo ya ndani ni VIP, kasheshe ikikatika katikati basi unacheza Disko unastukia ipo kifuani inazidi kupanda juu.
 
Enzi zile za gramaphone. Unazijaza upepo (no umeme, no batteries) na zilikuwa zinakula vijisindano vidogo vidogo ile mbaya. Sauti ni moja tu - maximum!
 
Enzi za radio zilizokuwa zinaendeshwa na betri kuubwa external, ukiwa dhaifu huibebi hiyo betri.
 
Kuna ndugu yangu(naomba anisamehe atakaposoma ni kukumbushana tu )alikosa sherehe ya kumaliza mafuzo ya mgambo,baada ya babu yetu kuvaa kaptura yake ,ambayo ndio pekee iliyokuwa inavalika kwenye sherehe na kanisani ,ililazimika kushinda ndani siku hiyo !mpaka leo hatujui dhamira ya babu ilikuwa nini,MUNGU AMREHEMU!
 
kuna Thread Nzuri sana ya haya mambo ya kukumbushana ilianzishwa na FMES, hipo humu nadhani "inaitwa tujikumbushe historia ya nchi yetu-picha"
nadhani ina mambo mengi mno ndani na ni real flash back, jaribuni kuicheki mtaenjoy sana
 
Mi nakumbuka gari la kugawa mikate, lilikuwa likipita mitaani na kusambaza mikate ya siha. Pia nakumbuka viatu flani vya plastiki, vilikuwa vikiitwa chachacha na suruali za mchelemchele.
 
Kitu ambacho sitokuja kukisahau maishani mwangu ni babu yangu jinsi alivyokuwa na uzalendo na nchi hii.
Kipindi cha vita ya Kagera alijitokeza akitaka awe miongoni mwa askari watakao shiriki vita.
akapimwa akaonekana afya yake hairuhusu hivyo arudi tu nyumbani.
Babu yangu alilia sana, alikosa amani mpaka vita inaisha na aliilaumu sana serikali kwa kumbania nafasi adimu ya kulitetea Taifa lake.
 
Back
Top Bottom