Tulipandisha mwenge wa Uhuru mlima Kilimanjaro mwaka 1961 kama ishara ya kupiga uonevu

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Tulipopata Uhuru Taifa letu lilipandisha mwenge wa Uhuru juu ya mlima Kilimanjaro na tukaweka maazimio ambayo ndio dira yetu.

Moja kati ya maazimio ni kupinga uonevu popote pale ulipo,na dhidi ya mtu yeyote yule

Tuliupandisha mwenge ulete tumaini,upendo mahali penye chuki na heshima palipojaa dharau

Sasa hakuna upendo tena,watu wanawekwa ndani hata nje ya utaratibu,kuna chuki kubwa kwa wale ambao hawana muono mmoja na wao,dharau zimejaa,wanasiasa wanadharau watu na wao kujifananisha na mungu.

Ni mwendo wa kuwawinda tu wale usiokubaliana nao na kuwaweka ndani.

Ule mwenge wa Uhuru ni kiashiria cha uhuru wetu wa kikatiba na ulipandishwa mlima Kilimanjaro kila mtu auone mwanga wake.

Uhuru wetu ni haki yetu
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,730
2,000
Katika historia ya nchi hii, hajapata kutokea kiongozi anayeendekeza visasi vya kisiasa kama HUYU.....jamaa kajawa kajawa na chuki, wivu, husuda, unafiki, uzandiki, ukatili, majungu, fitina, uroho, uzabinabina, ukorofi, uchawi, umajimbo, ukabila, udikteta na kila dalili ya sifa mbaya. Ningekuwa mwanasheria, hivi sasa angekuwa yuko kizimba kimoja na yule Dominick wa LRA kule the Hague.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom