Tuliozusha, kufurahia, kushadadia na hadi kutaka kuchukua kazi ya ‘Israeli' tusaidiane kujibu haya maswali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,418
108,517
1. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) ni wazima?

2. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) tungetokewa na hiyo hali tungejisikiaje?

3. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) tuna uhakika wa 100% na Afya zetu?

4. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) huyo fulani angetokewa na mabaya hali yetu ya Kimaisha ingebadilika?

5. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) tumeshaingia mkataba na Mungu kuwa hatutokufa na tutaishi Milele?

6. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) tuna Hofu ya Mungu kweli?

7. Je, Sisi ( Mimi na Wewe ) tumeshajiandaa kwa Adhabu Kali ya Mungu inayotungojea Mbinguni ?

Bado ( Mimi na Wewe ) hatujachelewa kutubu na kubadilika.

Asubuhi njema nyote na Mwenyezi Mungu atusamehe sote.
 
GENTAMYCINE,

Naomba nijibu swali namba 4. Jibu ni ndiyo hata kama siyo leo, but nina imani maisha yangebadilika, kutoka hapa yalivyo sasa hivi kwenda kwenye ahueni, na la muhimu sana kuliko yote tungerudishiwa Uhuru wetu wa kutoa maoni yetu yasiyomfurahisha yeye bila kutishiwa kuuwawa.

Kumbuka siyo mimi tu, bali asilimia kubwa sana ya wananchi sasa hawawezi kununua kilo moja ya nyama, wala kilo moja sukari, ambayo utakumbuka mwaka 2014 ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 1400.

Kiwanda cha Sukari cha Kagera baada ya kugundua uwezo wa watu kununua (purchasing power) umeshuka, wameanzisha package ya chini ya 1/4 kilo inayouzwa shs 700, (umaskini).
 
Salaam rafiki,

Binadamu yeyote anayefurahia kifo cha mwenzake bila kujali ni Nani huyo ni mtu wa shetani na nafasi yake anaijua ni kwenye lile ziwa liwakalo siku zote.

Uatamaduni mpya umezuka awamu hii ambapo Watanzania wanafurahia maradhi, maumivu au vifo vya wenzao. Kwa bahati mbaya hata baadhi ya viongozi wa juu wa Serikali wamejitokeza hadharani kuunga mkono ujinga huu.

Hivyo, hata wao wanapopata majanga inakuwa kama sherehe kwa walioumizwa na kejeli zao awali. Nakumbuka vizuri maneno ya kejeli ya Mwigulu Nchemba alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, siku alipopata ajali ya kugonga punda baada ya kutumbuliwa, watu walimpa pole punda badala ya binadamu.

Haya ni matokeo ya viongozi kujisahau na kujiona kwa vile ni viongozi wako juu ya kila kitu yakiwemo maradhi, ajali na vifo kitu ambacho siyo sahihi.

Watanzania badala ya kuwa wamoja wameparaganyika vibaya na umoja wa kitaifa uko shakani. Katika hali kama hii kila kundi linafurahia mabaya ya mwenzake na kuchukia mafanikio ya mwenzake.

Mwezi uliyopita nimeshuhudia WanaCCM wakitaka kumtenga MwanaCCM mwenzao ambaye binti yake ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama cha upinzani huko Rukwa. Hapo ndipo tulipofika/tulipofikishwa.

Hatuna wa kumlaumu, ni sisi wenyewe. Lakini hatujachelewa, tukipenda tunaweza kurekebisha hali hiyo, hatutaki basi acha twende wanavyotaka na tusilaumiane kila upande unaposherehekea au kununa kulingana na tukio.
 
Mimi nakuomba unisaidie kujibu hili swali moja tu, utajisikiaje pale utakapo ambiwa shetani amesalimu amri kwa Mungu, hakuna tena dhambi wala moto wa milele yaani hakuna moto wala adhabu za kaburi?
 
Kwani unavifahamu vitabu vingapi vinavyoelezea kifo?
Nimeweka wazi ili nijue andiko hata kama ni la kitabu gani halafu mjadala wa kuelimishwa uanzie hapo Israel inakuwaje kifo/mauti. Baada ya kujua kitabu ndo ntaanza kuuliza kwa kina kutegemea na kitabu husika na andiko lenyewe
 
Back
Top Bottom