Tuliowai kupata Supplemental kwenye final exam za UE/IE tukutane hapa

Nilipata supp ya business law first year nkachomoa chaap ..nkapata supp ya audit second year third year management chupu chupu nidakwe wakatuongezea marks nikaponea mdomoni ...aisee Supp n tamu san kama unazijulia !disccssn za supp mnakutana wote vilaza mnaelekezana ad raha , ambao hawajawai pata supp nadhan kuna k2 kama wamekikosa sana ktk elimu ya chuo
Mkuu vilaza tena!!!!!.....
 
thread ya waliosoma mpk Chuo Kikuu.... bahati nzuri Mimi kule VETA hakunaga hayo makitu yenu!
 
Mkuu sijakuelewa hapo kwenye tamrini (cousrework ) Yaan Ulipata 34 out of 40 Halafu Ue ikawa na marks 100 Yaan maswali 5@20 sasa ukijumlisha Na zile 40 mbona marks zinazidi. MSAADA
Technical supplementary zipo mkuu
 
Nilipataga supp moja third year semester ya Mwisho.. Ilikua supp ya Audit. Nilipata stress maana naogopa Sana shule halafu miaka yote nimecheza mwaka wa tatu ndo nikala supp halafu sijui naichomoaje.
Uzuri ni kwamba ile supp tulipata karibia 75% ya tuliokua tunasoma hilo somo. Kuna mkaka nakumbuka alikuaga anafundisha review classes za CPA nae akashikwa kwenye supp.
Kuna mwalimu alikua anataka kunizoea sasa alivyojua Nina supp akataka kutumia chance anile halafu akaniombee kwa mwalimu mwenzie kwenye supp nichomoke. Nikamwambia Niko radhi kurudia mwaka ila sio kubadilishana mwili wangu Na supp. Nikajiapiza kutoomba msaada kwa mwalimu yoyote yule nitaifanya supp Na nitachomoa.
Siku ya kwenda kufanya supp Na nilivyo Na allergy Na masomo ya kuandika niliandika nilivyochoka nikabeba vitu vyangu nikakusanya pepa nikaondoka. Nikampigia bf wangu kumtaarifu mwakani narudia mwaka maana sina uhakika wa kufaulu. Hapo nimetoka kwenye pepa hata lisaa halijaisha.
Japo nilishazoeleka kutoka wa kwanza kwenye mitihani huu walijua imekula kwangu maana ulikua ngumu hatari. Nashukuru Mungu nilipita salama maana ile supp hata nikilala nilikua naiota. Nikawa nawauliza rafiki zangu ambao hamna semester inapita hawajahudhurua September Conference waliwezaje kukaa kwa amani wakati wakiwa Na supp mbili Na zaidi maana Mimi moja tu ilinikondesha

ungesoma course yeyote ya udsm au faculty of commerce mzumbe wewe. ungejua kama sap sio kitu cha kushangaza... walimu wote wanajua wanafundisha vichwa wa sekondari.. so pepa zinakazwa mwanzo mwisho
 
Mkuu sijakuelewa hapo kwenye tamrini (cousrework ) Yaan Ulipata 34 out of 40 Halafu Ue ikawa na marks 100 Yaan maswali 5@20 sasa ukijumlisha Na zile 40 mbona marks zinazidi. MSAADA
C.work ni 40 alafu UE ni 60 total ni 100.
Lakini marks amvazo utapata kwenye UE itazidishwa na 0.6.
Inamaana kama kuna maswali 5 UE na marks kwa kila swali ni 20, then marks utakazopata uta zidisha na 0.6.
Mfano ukapata 100 kwenye UE nilazima izidishwe na 0.6 ambayo jibu litakua 60, then una plus na C.work yako.
Hitimisho.
C.work 34
+
UE 86/100
Total 85.6

Usipo elewa ina bidi uombewe.
 
dhu! Mkuu rudi shule ukasome tena hesabu mpaka nimeona aibu, una aibisha jina la iyo Id yako
 
dhu! Mkuu rudi shule ukasome tena hesabu mpaka nimeona aibu, una aibisha jina la iyo Id yako
Nitarudi shule.
Inawezekana system ni tofauti.
Kwetu sisi.
C.work ni 40
UE ni 60
Total ni 100
Lakini UE maswali ni 5 yenye 20 marks kila moja, ina maana ukipata yote ni sawa na 100, lakini kiuhalisia sio 100, coz tayari nyuma una marks za c.work. so, kama umepata 100 kwenye UE nilazima izidishwe na 0.6 na jibu lita kua 60, then hiyo 60 ndio ina jumlishwa na c.work uliyopata.
Mfano C.work nimepata 34
UE nikipata 100 ita zidishwa na 0.6 ambayo ni sawa na 60, then hiyo 60 ina jumlishwa na 34 ya c.work hapo nitakua nimepata 94.
Hesabu tuachie sisi.
 
unasikitisha sana mkuu, unasoma chuo gani?
 
unasikitisha sana mkuu, unasoma chuo gani?
Elewa mkuu.
Kwani 100*0.6=?
Kwa msaada tu, jibu ni 60.
So, C.work yangu ni 34.
34+60=94
Hiyo ni system yetu.
Na UE maswali haya pungui wala hayazidi 5 na 1@20 marks. (Ni mfumo wa chuoni kwetu).
Hata ukipata 70 out of 100, hiyo 70 itazidishwa na 0.6 na jibu lake ndio lina jumlishwa na C.work yako.
So, nimekosea wapi, nisaidie basi.
 
Apo ulipo weka 0.6 fanya iwe 0.14 hadi 0.2 alafu jumlisha 34 ya c.work, kwenye mtihani nilikua najua swali la jumla 20% mengine nilikua sijui pia sijui kama nilipata lote
a: 0.14*100=14
14+34=48

b: 0.2*100=20
20+34=54
Ila mkuu, mi nadhani system itakuwa tofauti.
Kama nilivyosema mwanzo, C.work ni 40 alafu UE ni 60.
Then UE mswali huwa ni 5 tu 1@20 marks.
Ina maana mtihani wa UE uta onyesha 100 marks but zinazotakiwa ni 60 marks only, then una plus na c.work yako. So, kama umepata zote 100 marks kwenye UE, na only 60 marks zinahitajika, ndio maana nazidisha kwa 0.6 *100 ili niipate hiyo 60 inayo hitajika.
Na hata kama umepata 70 out 100 bado tita zidisha kwa 0.6 ili tupate marks halisi ambazo zita jumlishwa na C.work yako.
KAMA BADO SIELEWEKI TUVUMILIANE, SI UNAJUA WAZEE WA KUMEZA, CHENGA KIDOGO CHALI.
KILA LA KHERI MKUU.
 
Niliwahi kuwa na supp 2 na special 6 jumla 8 na zikachomoka vizuri..

Mjini njoo na akili zako..
 
a: 0.14*100=14
14+34=48

b: 0.2*100=20
20+34=54
Ila mkuu, mi nadhani system itakuwa tofauti.
Kama nilivyosema mwanzo, C.work ni 40 alafu UE ni 60.
Then UE mswali huwa ni 5 tu 1@20 marks.
Ina maana mtihani wa UE uta onyesha 100 marks but zinazotakiwa ni 60 marks only, then una plus na c.work yako. So, kama umepata zote 100 marks kwenye UE, na only 60 marks zinahitajika, ndio maana nazidisha kwa 0.6 *100 ili niipate hiyo 60 inayo hitajika.
Na hata kama umepata 70 out 100 bado tita zidisha kwa 0.6 ili tupate marks halisi ambazo zita jumlishwa na C.work yako.
KAMA BADO SIELEWEKI TUVUMILIANE, SI UNAJUA WAZEE WA KUMEZA, CHENGA KIDOGO CHALI.
KILA LA KHERI MKUU.
nadhani haujamwelewa anachomaanisha.

yaani mtihani wa UE una marks 100. maswali 5@20 marks.

yeye alikuwa anajua moja tu la marks 20.

tukisema alipata hilo tu lote ana 20

20 x 0.6 = 12

jumlisha na CW 34

34+12= 46

na hapo inawezekana hilo swali la marks 20 hakupata lote
Ultimate au nakosea
 
ni sawa mkuu swali la maandishi kupata lote sio rahisi bora hesabu unaweza kupata lote
 
Asee watu mmesoma kwa raha yaan semister 1 masomo 6?? Sie semister ikiwa na masomo machache ni 9 tena hio semister inakuwa ya bata hatari bt mostly semister ilikuwa na modules 12 mpka 13 so kwa mwaka ni modules 24 &26 kwhyo kukuta watu wana sup zaidi ya 10 ilokuwa kawaida sana... shkamoo wana DIT alumn

Kimoko hajambo?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom