Tuliowahi kuwa na pesa za mboga na baadaye zikaisha, maisha yalikuwaje?

chumanile

JF-Expert Member
May 20, 2018
296
327
Ama kwa hakika M/Mungu anatupigania haswa kwa maana wezetu waliopo katika sehemu mbalimbali wanaishi kwa hofu kubwa sana kutokana na hili janga la Coronavirus.

Kiukweli maisha yanaenda mbio sana, na changamoto ni nyingi mno, ambazo kila mtu anakutana nazo. Inawezeka wewe uko vizuri hujui haya magumu ya wengine rakini inaweza ukatoa ushuhuda kwa vile umeona mtu akipigika, kunyanyasika, kukosa haki zake nk.

Binafsi nilishawa kupigika miaka kadhaa iliopita baada ya kufilisiwa na bank. Kiukweli niliishi katika maisha ambayo hayana mfano wake. Katika maisha yangu sikuwahi kuona mtoto wangu akivaa soski imetoboka, kiatu kimechanika hakifai, yunifom imechakaa hata nguo ya mfungwa ina hafadhali. Njoo kwenye mlo, hatari tupu. Ilifika hatua nikawa hata mkate wa siku sipati, Watoto wanakula visivyo heleweka ampaka wakazoea.

Aisee nilipigika sio poa. Madeni ndo usiseme, kila kona nadaiwa, bili ya maji, umeme, usafi, ada ya watoto ya madrasa, nk.ilifika hatua nikaona sasa nakimbia mji yapo mengi mno nikikumbuka natoka na machozi rakini nilijipa moyo na kuamini haya ni mapito. Nilisimama mwanaume nikainuka nika simama na maisha yanaendelea.

Je, wewe ulipitia magumu yapi ambayo yalikufanya kujuta na kukusa raha ya maisha?

Je, kipi kilikuumiza zaidi katika mapitio hayo ya msoto?

Kipi kikikupa moyo na kujiona nitashinda majaribu haya?

Je, kwa sasa hari ikoje kimaisha?

KUPITIA UZI TUJIFUNZE KUTO KATA TAMAA NA TUAMINI SHIDA HUMPATA KIRA MTU. TUPE SOMO, ULIIVUKAJE KATIKA MSOTO HUO?
 
Hakika tangu nimefanyiwa vigisu kazini napigika mno mpaka sasa, Halafu huyo Mzee/boss aliyenifanyia vigisu naye katemwa.

..ingawa alinipigia simu na kuniomba radhi sana kwamba alichonifanyia ni kitu kinamtesa kila siku.-nikamwambia mimi wala sijawahi mchukia coz najua Mungu ndio mtoa riziki.

Juzi kati mwezi wa NNE mwishoni kanipigia simu ananiomba nauli mke wake aende kwao Bukoba...nilijiskia vibaya mno japo alinifanyia unyama wa hovyo sana.

...MTU mwenye connection tafadhari ninusuru na hili balaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom