Tuliowahi kuwa mubashara kama Waalikwa IPP Media( TV na Redio) tukutane

clion dismas

Senior Member
Aug 6, 2017
185
170
Wanabodi
Habari za leo hii, bila ya kuwachosheni ninawaomba ndugu zangu tujadili faida na umuhimu wa nafasi hii yakuwa mubashara kwenye kampuni hii ya mwendazake Reginald Mengi.

Ilikunufaisha vipi na ilikujenga namna gani katika hali zote kulingana na mada uliyokuwanayo? Na kwa wale chipukizi wengine wanaodhani hawawezi kuwa mubashara IPP media unawapa ushauri gani?

Lakini mwishowe bila ya mwendazake Mengi, unadhani ungepata matokeo chanya zaidi ya kile unachokifanya kwa sasa?

MIMI BINAFSI(CLION)

Nilikuamubashara kwenye kipindi cha kumekucha kishindo, nilikua na dakika 30 na Maulid Kambaya mwaka jana mwezi wa 8. Mada ilikua inasema "NAFASI ZA AJIRA KWA WAHITIMU". Kipindi hiki urushwa asubuhi.


Nakumbuka kwa ufupi nilidodosa mambo yafuatayo:-

Wahitimu tunamaliza wengi sana kila mwaka zaidi ya laki moja ma serikali ya Jamhuri inaweza kuajiri wahitimu 30,000 tu na kwa ujumla sasa takribani laki tano na ushee kati ya watu milioni 50 ndio wameajiriwa na serikali kwa wastani(probability) ya 0.01, yaani kwa lugha nyingine kwa kila watu 100 kwa sasa wanaoomba kazi ni 1 tu anayeweza kuajiriwa.

Kwa lugha nyingine pia kuna mashirika na makampuni binafsi. Wanaisaidia sana serikali katika kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wetu ingawaje bado hawawezi kupata nafasi wote.

Sasa wale ambap hawako serikalini wala taasisi binafsi wafanyeje?

Nilizungumza yafuatayo:

1. Watambue karama zao na vidole gumba vyao ambavyo Mungu kawabariki kwavyo na waviendeleze hivyo. Hapa namaanisha ya kwamba, una kitu cha utofauti ndani yako ambacho hata bila ya elimu yoyote ile kinaweza kusapoti maisha yako. Mathalani, kipaji cha kuchora, kutangaza habari, kuimba, kupika, kuandika hata kuongea tuu. Unaweza kutumia vitendea kazi vichache tuu kama kwa wachoraji, kuna mambo mengi sana kwenye jamii yanayoenda ndivyo sivyo unaweza kutoa ushauri wa kuyasahihisha kwa kutumia ubunifu wako na ukaufikisha ujumbe kwa wengi na kuchochea mabadiliko huku ukiingiza hata kiasi fulani.cha kusukuma maisha yako kupitia mitandao ya kijamii inayofikiwa na wengi sana.

Mimi nilitoa mfano, nilipokua chuoni mwaka wa pili wa masomo yangu(electricla engineering) nilianza kusoma diploma ya human nutrition ambayo nilihitimu na kuniwezesha kuandika kitabu cha afya lishe, "MUNGU NA UPONYAJI KATIKA MATUNDA NAFAKA NA MBOGAMBOGA". Kitabu hiki nilikiprint kwa bum na kukiuza nikiwa mwaka wa tatu kwa kila nakala niliiuza kwa shilingi 10000/= za kitanzania ilihali hadi kinakamilika nilitumia 3400 tu. Gharama zilikua mb(data) na laptop yangu. Chuo changu kilinitunuku best award certificate kwa kazi hiyo na kuwahamasisha wengine wafanye kama mimi mwanafunzi mwenzao.

Lakini pia kwasababu nilitambua Mungu alinipa karama Mbalimbali pia niliweza kutengeneza muziki na kurekodi cd(mimi ni mtunzi na mwanamuziki). Jambo hili nililifanya tangu mwaka wa kwanza chuoni nalenyewe lilinibust sana kwa kutumia bum lilelile.

"Nilitamatisha kwa kuwaambia vijana kiujumla ya kwamba, maisha ya leo ni ya changamoto nyingi. Hawana budi kuonyesha kile walichonacho kama chachu ya kuwavutia wenye pesa kuwekeza kwenye karama zao. Lakini pia niliwaambia wasisubiri ajira ambazo hazifaamiki zitakuja lini, watengeneze ajira kwa kutumia changamoto zilizopo kwenye jamii. Kwa ufupi niliwaambia, huwezi kusomeshwa na serikali kwa fedha nyingi ikiamini utakuja kuwa mkombozi kwa wale ambao hawakufanikiwa kupata nafasi kama yako alafu unapomaliza elimu yako unakuwa mzigo mzito kuliko ambao hawajpata elimu kama yako. HILI UDHIHIRISHA ULISOMA KWA KUKARIRI ILA SIO KUKOMBOLEWA KIFIKRA".
Cliondismas.png
Clion dismas.jpg

KWAKWELI NILISHAURI MENGI SANA KWA DAKIKA ZILE 30 NA MUDA HAUKUTOSHA. MKIPENDA KUONA VIDEO YANGU YA ITV NITAWAPA LINK YA YOUTUBE.

KARIBUNI TUJADILI
 
Uko vizuri kijana,je uliuza nakala ngapi? Sasa hivi umejiajiri kwenye nini?

Nilizalisha nakala 100 kwa mara ya kwanza, zote ziliisha ila Mungu nilimpa sehemu yake(1/10 ya vitabu 100 na sadaka pia).
Soft copy zinauzika hadi sasa online kupitia " UWARIDI APP". Zaidi ya yote, mwaka jana nimetoa toleo la pili na uuzaji wake Mungu anausimamia. Kama uko Dar unaweza kwenda maktaba ya taifa ukasoma kazi zangu hizo.
Maktaba ya taifa imenipa ISBN na nina hati miliki.

Pesa haijawahi kutosha hivyo wekeza maeneo mbalimbali. Hii ni sehemu ya maisha yangu ingawaje si maisha yangu.
 
Malumbano ya hoja mada ilikua inahusu kuhusu bajeti ya nchi inayopangwa je inamaliza changamoto katika mwaka husika?! Pia katika kipindi cha vijana na utandawazi etc. Kwa ufupi itv nimehudhuria sana Malumbano ya hoja na haswa mada za uchumi na siasa
 
Hongera ndugu. Sasa tuelezee, imani yako katika mada hizo ilikua wapi? Pia mahudhurio hayo yalikuathiri namna gani? Wengi hatupati muda wakufatilia vipindi hivi tunaweza kujifunza kitu hapa.@ zongwale @ taecoltd
 
Back
Top Bottom