Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,669
- 40,917
Hili jukumu la ku keep time nilipewa rasmi nikiwa darasa la tano.
Ilikuwa kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuwa kiranja wa elimu toka darasa la 6 mpaka namaliza la Saba.
Changamoto kubwa ilikua ni kuamka asubuhi kugonga kengele ya kushikisha namba.
Kengele za kumaliza vipindi inakufanya kila Mara uangalie muda.
Kipindi hicho nakumbuka nilikua na saa moja matata sana zile za kubonyeza
Sasa baada ya kupata Hilo jukumu mzee baba akaona aniunge mkono kwa kunipatia zile saa zenye kutumia mshale.
Sikuhiyo ya Tukio nakumbuka niliivua saa na kuiweka mfukoni; ile naitoa kumbe ilikua ipo juu chini nikahamaki nikajua ni saa 8 mchana kumbe ilikua saa sita; nikagonga kengele ya kwenda nyumbani ; watu wote wakatoka madarasani wakati vipindi vikiendelea ilikua taharuki ya aina yake.
Changamoto za Utime keeper hizo.