venance7
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 554
- 1,636
Hili kosa la kutuma sms kimakosa nahakikisha sitalirudia tena.
Nakumbuka niliwahi kumtumia mama yangu mzazi sms ambayo ilikuwa inatakiwa iende kwa demu fulani hivi , bahati mbaya ikaenda kwa B. mkubwa. SMS yenyewe ilikuwa ni zile za kulazimisha kuomba show (sex); niliandika SMS yenye maneno mazuri mno, halafu ile sijaangalia vizuri, nikaituma hapohapo ikaandika "sms delivered". Daah! macho yalinitoka balaa. Haikupita dakika mbili mama anapiga simu na alikuwa mtu wa dini kwelikweli; simu inaita jasho linanivuja nawaza nimdanganye nini.
Kuna SMS zingine hata kama mzazi anajua mwanangu amekua sasa, lazima zitakutia aibu. Nikapokea simu mama anasema "Mwanangu nini sasa hiki na wewe? Maliza masomo yako ya chuo kwanza, mapenzi yapo tu kila siku , ngono zitakuua baba"
Ile fedheha siwezi kuisahau kabisa.