Tuliowahi kusomesha Wachumba na hatujawaoa. Tukutane hapa

Kwa kiasi kikubwa bora hata wewe mtoa mada umepata hata mtoto na pia mwanamke ndiyo anayetaka muoane.

Ila kuna hawa wakuda wengine ndiyo tatizo. Tunajadili hivi, wao wanafanya hivi!
Nimecheka sana na hii comment.

Vichwa maji a.k.a vichwa panzi achaa kabisa..
 
Wakuu, hili sakata la kuwasomesha wachumba naona linafukuta kwa sasa.

Ninaamini tuko wengi tuliowahi kuwasomesha wachumba/girl friend na bado hatujawaoa sisi.
Tukutane hapa!!
Nitaanza na mimi binafsi.

Nilipokuwa chuo mwaka wa nne - 2006!
Nilikuwa na demu wangu yeye alikuwa anasoma kozi ya miaka mitatu!
Na wakati huo alikuwa mwaka wa kwanza tu!!

Ilitokea akapata mimba, niligoma asiitoe!
Alipoenda kwa wazazi wake Moro wakamkataa kabisa, na nilipoongea na Mama yangu akaonyesha nia ya kumsaidia, so ikapendekezwa akalelee mimba yake kwa Auntie wangu huko Lushoto.

Alienda huko mimba ikiwa na miezi 5 coz ilimsumbua kidogo hakuweza kukaa chuo kwa kipindi kirefu, nilikuwa nishamaliza chuo na bahati nzuri baada ya mimi kuhitimu nilipata kazi ya muda(Temporary)
kwenye kampuni moja hapo Kibaha...

So kila mwezi nilikuwa namtumia Auntie 120,000/= kwa ajili ya kumlelea mjamzito. na yeye pia nilikuwa namtumia kidogo, sikuwa na matumizi mengi kwa upande wangu. Mchumba alijifungua vizuri kabisa mtoto wa kike aliyefanana na mimi kila kitu.
Niseme tu nilikuwa nailelea ile mimba bila kuwa na uhakika kama ni ya kwangu.

Hadi mtoto alivyozaliwa ndio nikajiridhisha kuwa ni mimi(mambo ya chuo siyo ya kukurupukia) inaweza kushikishwa hivi hivi.
Baada ya kujifungua tu, haikupita miezi 6 girl friend akaomba kurudi shule. Bahati mbaya wakati anaacha ili akalee mimba hakuna aliyekumbuka utaratibu wakuahirisha masomo kisheria. So ilibidi aombe tena chuo upya na akabadili na kozi kabisa, akapata nafasi Chuo cha Stella Maris(Saut) Mtwara campus-
BAEd. alivyorudi kwa wazazi wake wakagoma kabisa kumsomesha tena coz hakupata mkopo kwasababu ya kuchelewa kuapply.

Wakati huo nilishapata kazi ya kudumu, so wazazi wake walivyokataa kumsomesha niliamua kufanya hiyo kazi, mtoto alirudishwa kwa Mama yangu. Mchumba akaenda zake Chuo wakati huo mtoto ana miezi 8 tu!!

So nikawa nalipa ada na matumizi mengine yoote yanayomhusu. Wakati wote huo nikiri kuwa sikuwahi kumtamkia au kutamka kwa mtu yeyote kuwa ndiye nitakayemuoa.
Hilo nililiweka kwenye akili yangu mwenyewe as long as nilikutana naye tu chuo.

Na alivyopata mimba hadi anajifungua hatukuwa karibu kivile kwasababu yeye alikuwa Lushoto mimi niko Dar. So we never had sex again, tulikuja kurudia mara moja tu wakati nampeleka Chuo Mtwara na ilitokea kwasababu siku hiyo tulilala chumba kimoja hotelini.

So ilibidi nianze kukubali tu kuwa ndio mke wangu, na alinizalia binti mmoja mzuri sana ambaye nilijikuta Nampenda sana sana.
Mtoto akanifanya niwe na ari kubwa zaidi ya kumuoa Mama yake ili tuishi pamoja.
Na pia huyu mchumba na Mama yangu walikuwa marafiki wakubwa sana.

So mara kwa mara Mama alikuwa ananiambia nisipomuoa huyo dada sitakaa tena nipate mwanamke. Maisha yanaenda bana mdada akamaliza miaka yake mitatu!! Kwa ada niliyokuwa nalipa mimi, ili happen tu mara moja semister yake ya mwisho mambo yaliniendea kombo, mjomba wake mmoja akamsaidia kulipa na haikuzidi laki sita na nusu...

Akamaliza chuo, ila kipindi chote cha likizo alikuwa anaenda kwa Mama yangu kwa ajili ya mtoto wetu, so alikaa pale karibia mwaka mzima ndio post zao za ualimu zikawa zimetoka, akapangiwa Sekondari huko Nzega.

Hela ya kujikimu+yakuanzia maisha na nauli nilimpatia mimi na nyingine nilituma yakuhonga sijui ni afisa elimu huko ili asipangiwe shule za vijijini, nilimpa kama laki tisa hivi nje ya nauli yake.
Nikiamini angeweza kupanga nyumba nzuri na kununua kitanda na godoro aanze maisha..

Tuliendelea kuwasiliana sana na week end moja nilimtembelea ili kujua maisha anayoishi walikuwa wanakaa na rafiki yake waliosoma wote Mtwara. Wanashare sebule lakini kila mtu na chumba chake.
Nilifurahia kweli mazingira waliyokuwepo.

Ule usiku alinishawishi sana nimruhusu akamchukue mtoto aje aishi naye, ila nafsi yangu iligoma kabisa kumwachia mtoto. So alivyoona mimi sielekei akaanza kumpiga Mama sound za kutosha, so Mama akawa anamuombea kwangu, nimruhusu akakae nae kidogo then amrudishe, hapo mtoto anakaribia miaka mitano na alikuwa anasoma pre-unit shule moja hapa Dar.

Msisitizo wa Mama ukanizidi nguvu akaja likizo moja akaruhusiwa kwenda nae kwa minajili kuwa atamrudisha.
So mtoto akaenda kwa Mama yake sikuwa na mashaka sana, nikijua kwasababu lazima amrudishe Dar ili aendelee na shule.

Likizo imekaribia kuisha nampigia Mama simu akamchukue mtoto au Mama yake amlete zikaanza story nyingine, oh! mwache tu hata huku kuna shule nzuri, so abaki amalizie hiyo pre-unit then la Std 1 atarudi Dar. Nilikuwa mkali sana, ila kwasababu ya Mama kukubaliana nalo, ikabidi nitulie tu, kumbe na Mama alikuwa upande wa yule Dada akiamini akikaa na mtoto itakuwa rahisi sana mimi kuhamasika kufunga nae ndoa.

Nilianza kuweka taratibu za kumuoa

Nilianza kuwa serious sasa kuwa nitamuoa. Nikaweka taratibu za kutuma wazee huko kwako, kwa ajili ya mambo ya mahari! Ila kila nikipanga inashindikana nafsi inagoma kabisa ikabaki kuwa ni leo ni kesho ni leo ni kesho mwaka ukakata.

Mawasiliano yakaanza kupungua, binti kipindi cha likizo akawa anagoma kumleta mtoto Dar, mtibuano ukaanzia hapo! Kuna kipindi alisema hana nauli, nikamtumia alivyoipata akasema sijui yuko zamu na kidato cha nne, so baada ya wiki mbili atakuja, akasahau kuwa alinitaarifu kuwa alisha sign likizo.

Wiki mbili zikaisha akaleta porojo nyingine ya kilimo kuwa alishaanza kilimo so akija mazao yake yataharibikia shambani.
Na kipindi chote hajawahi kuniambia kama anajishughulisha na kilimo.

Hadi likizo ikaisha hakumleta mtoto. Jumamosi moja baada ya likizo yake kuisha niliamua kumtaarifu kabisa kuwa nitaenda mimi Nzega kumwona mtoto, hapa lengo langu kuu lilikuwa ni kujua kwanini alishindwa kuja Dar.

Ebwana eeh nilifika nikakutana na team, binti ana kaa na watoto wengine kama watatu hivi wenye umri tofauti kidogo mmoja wa kiume na wawili wa kike. Wote bado wanasoma shule ya msingi.
Na wakati ninaenda alinitaarifu kabisa kuwa alipokuwa anakaa alihama, kwasababu aliona hawezi kukaa nyumba moja na yule rafiki yake.
Ila kipindi anahama hakuniambia chochote!!

Jioni tukitoka kwenda kukaa mahali mimi yeye na mtoto wetu.
Ili anieleze ni kwanini alishindwa kuja Dar, kichwani nilishapata sababu ni nani angewaachia hao watoto.
Na hiyo nyumba aliyohamia ni ya nani.
So akaanza kujieleza alishindwa kuja kwa sababu zile zile za awali.

Hamna shida! nikamuuliza hao watoto unaokaa nao ni wa nani?
Akaniambia ni wa rafiki yake ambaye wanafundisha nae (mwanaume) ambaye aliachana na mke wake, so alipooa mke mwingine ndio akawaombea hao watoto hapo kwake Mama yao akija atawachukua, nikamuuliza for how long yuko nao akaniambia ni almost 4months, Mama yao yuko machimboni huko so akirudi atawachukua. I feel terrible!!

Nikamhoji ni kwanini ulihama bila kunijulisha? Na ni kwanini alikubali kupokea hao watoto bila kunitaarifu? As long as wangeishi na mtoto wangu pia.
Hakuona sababu yakunitaarifu kuhusu hao watoto coz hakujua kama angekaa nao kwa muda mrefu.

Kuhusu nyumba, aliniambia ni ya rafiki yake, aliyomwachia wakati anaenda masomoni so halipi kodi, hiyo ya kwanini hakunitaarifu anadai aliona ni jambo la kawaida.

Niliwaza sana, nikaamua kutokwenda kulala kwenye hiyo nyumba nikachukua room hotelini, ni kalala ila mawazo yalikuwa mengi sana.

Niliplan kuondoka jumatatu.
So ile jumapili nilienda kwa yule rafiki yake kwa ajili ya stori mbili tatu.
Huyo rafiki yake alimfichia siri sana. Alichoniambia hawako tena pamoja kama zamani...so hajui what is going on.
Mchana alikuja tena pale hotelini na mtoto, nikamwambia amwandalie vitu vyake nitaondoka nae.
Coz wale watoto wa huyo Mwl mwenzake walikuwa ni wa Imani tofauti na sisi.

Alikubali kuwa angemwandaa, tukaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, gafla akaniambia mshahara anaopokea kwa sasa ni kidogo sana, kwasababu alikopa milioni 10 bank so anakatwa!! Nikamuuliza alikopa za nini? Akajibu ili awekeze kwenye kilimo na hata haikumlipa akapata hasara. Akawa ananiongezea mawazo kibao. Aliwezaje kukopa hela nyingi hivyo bila kunijulisha?

Nikaona ana washauri wengi wanao myumbisha.
Baada ya mazungumzo mengi akaondoka nikamsisitizia kuhusu swala la mtoto kuandaliwa.
Akaniahidi kuja nae stand asubuhi.
Nilienda stand asubuhi nikamkuta yuko peke yake bila mtoto.
Aliniomba sana nimpe muda amlete yeye mwenyewe Dar, na isingechukua muda likizo ya midterm angekuja nae.

Nilikasirika sana, na nikaamua kumwambia pale pale wewe endelea na maisha yako usinihesabie kuwa nitakuoa.
Baada ya hayo maamuzi hakuamini, but nilikuwa serious kwa mambo aliyokuwa anayafanya ali discolify kabisa kuwa mke wangu.
Mama alivyosikia alilalamika sana nikaamua kumpa sababu na yale niliyoyaona.

Mama alivyom'bana about 10m akamwambia alikopa ili anunue nyumba aliyokuwa anakaa, so ile nyumba sio ya rafiki yake, ilikuwa inauzwa tu akaamua kuinunua.
Na alifikiri endapo angeniambia nisingemruhusu kabisa kununua hiyo nyumba. I feel terrible!! Mama alinisihi sana nitengue maamuzi niliyoyafanya ila haikuwa rahisi.

Tukaachana rasmi, ishu ikawa mtoto kwasababu alikataa kata kata kumtoa, hadi akatishia kufanya kitu kibaya endapo ningeendelea kulazimisha, ndugu zake wakamuunga mkono, ana ndugu zake wanasheria so walikuwa wanampa kiburi cha kutosha.
Kilichouma zaidi akawa anaeneza uzushi alitelekezwa chuo, hatukumjali alidiriki hadi kusema ndugu zake ndio walimsaidia.

Akaniambinia kama namtaka mtoto niende Mahakamani. Sikwenda for the sake of my daughter.
And I promise my self hata kama sitamchukua bado nitaendelea kumsomesha shule nzuri.
And I do that to date.

Nilipata mwanamke nikaoa. And my life goes very well and successful
Ila mtoto unaye atake asitake so shida ni yanini??
Ila angalie asimbadilishe dini
 
Rudia ulichoandika sasa umesema unamtoto na mwanamke mmoja na huko aliko anaishi na watoto wengine halafu hao watoto ni dini ingine sasa ulitaka nikomentije kwa mfano
I got you.
Thats happened 2007.
My daughter now is in form one, a boarding school.
We are now very good friends
 
Ooh yes! Tulisoma na dada mmoja chuo alivua Pete ya ndoa akiwa second year na akabadili dini akaolewa na jamaa mwingine.
Mumewe wa ndoa alikuwa anakuja na mtoto pale hostel mabibo yule dada hataki hata kuwaona.

Walipo maliza chuo wakazaa motto mmoja ila Sikh moja isiyo na Nina yule second husband alipigwa risasi usiku na watu wasiojulikana dada akabaki mjane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ooh yes! Tulisoma na dada mmoja chuo alivua Pete ya ndoa akiwa second year na akabadili dini akaolewa na jamaa mwingine.
Mumewe wa ndoa alikuwa anakuja na mtoto pale hostel mabibo yule dada hataki hata kuwaona.

Walipo maliza chuo wakazaa motto mmoja ila Sikh moja isiyo na Nina yule second husband alipigwa risasi usiku na watu wasiojulikana dada akabaki mjane

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom