Tuliowahi kupitia jandoni, tohara, mafunzo na changamoto zake tukumbushane enzi zako unakumbuka nini?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Tuliowahi kupitia jandoni, tohara, mafunzo na changamoto zake tukumbushane enzi zako unakumbuka nini?

Mimi ni mmoja wa vijana tulipotia jandoni nakumbuka enzi hizo Kilimanjaro hususan sisi Wachaga tulikua na utamaduni huu sana wa vijana kwenda jandoni

Utaratibu ulikua ni kila kijana akipata tohara basi ule mwezi mmoja au zaidi anaokua yupo ndani basi anafundishwa mambo kadhaa kuhusu yeye na kujitambua, elimu ya uzazi, heshima na utiifu.

Kwa Wachaga majando yalijengwa migombani au maporini, ambapo migombani, majani ya migomba maturubai na matawi ya miti yalitumika kutengeneza jando la vijana na chini walilalia majani ya migomba yalotandazwa chini na ikiwa wanahitaji godoro wanaweza wakaweka na godoro juu

Huu utamaduni bado upo
Maandalizi yalikua kama ifuatavyo:---

NAENDELEA
Maandalizi ya ujenzi wa jando yalifanyika siku moja kabla ya vijana hawajapata hiyo tohara

Kisha wakishajenga jando, sasa wataitwa wataalam wa tohara ambapo Mzee wa hiyo kazi atakuja au hata daktari atakuja atawafanyia vijana tohara na akishakamilisha basi huko nje shangwe na vigelegele husikika ambapo Wazazi wanafurahia mwanao kupata tohara na kuona sasa kijana wao sasa kakua

Na mara nyingi sana ilikua ni vijana kuanzia miaka 8 mpaka 18

Na rika zuri ilikua ni wale waliotimiza miaka 10 hadi 18 hapa ndo walikua wanapewa mafunzo vizuri kabisa

Na ilikua ni kila jando wanafanyiwa vijana zaidi ya wawili na mara nyingi wanakua ni vijana wawili ambapo kitendo cha kufanyiwa tohara pamoja kinahesabika kuwa ni undugu wa damu mshaunganisha na hapo ni urafiki na udugu hadi kifo inakua tayari ni mtu na patner wake (ukhoo) kwa kichaga

Huyu anakua ni ndugu yangu kabisa maana kitendo cha kufabyiwa tohara pamoja naye inaonekana ni kana kwamba mmechanganya damu na tayari huo ni urafiki w maisha kwa shida na raha

Nitarudi kuendelea kuelezea sasa wanachofundishwa ninini haswa,vyakula, kukabidhiwa fimbo,siku ya jungu, kuoga mtoni,kuchoma jando etc na siku ya kutoka,na pia suala la wanawake kutoruhusiwa kwenda kwenye majando ya wanaume
 
KWINGINE hakuna kuoga maji safi,ni kupakwa tope zito mwili mzima kipindi chote cha jando/tohara. Unawekewa mwangalizi kukuchunga dushe lisidinde,likidina unagongwa enka miguuni ili dushe lisinyae,lengo ni lisipasukepasuke na kuanza upya kupona.Changamoto nyingine ni kutahiriwa bila kupigwa sindano ya ganzi,hayo maumivu ni balaa usiombe utahiriwe bila ganzi,halafu kisu chenyewe cha kienyeji.
 
Vichapo pia vinatembeaga utafikiri mpo chuo cha mafunzo (jela),hasa Kama hujui lugha yenu vizuri maana mafunzo yote ni kwa kilugha chenu.

Msosi sasa asubuhi chai kila mtu themos yake na iishe fast ukiremba remba unakula stick za kufa mtu saa nne uji wa ulezi kila mtu sado mwendo ni ule ule akuna ni cha ya Moto wala Nini ukinyanyua sado unatakiwa uiweke chini ikiwa nusu ukinyanyua Tena inatakiwa iwe imeisha

Hiyo saa nane ugali mkubwa mithili ya kichuguu yaani mnatakiwa mpige fast hakuna kuremba usiombe utapike utakula na kwambia sisi mmoja wetu alitorokaga night kali acha tu
 
Nilijua haya mambo Kilimanjaro hayapo Hongereni sana. Kwa sasa imekuwa ngumu sana hizi kambi za jando kufanyika na sjui kama zipo.
Nakumbuka jando yangu ilikuwa na Vijana 16, tuliwekwa camp siku 3 kabla ya mtiti wenyewe wa kuvua sweta ukawa siku ya Jumamosi. Tulielekezwa kwenda na Shuka 1, Panga, Manati na Mkuki lkn pia kila mmoja alipaswa awe ameshamwandaa msimamizi wa mikono yake. Kazi ya kwanza tulianza kwa kutengeneza Uzio kuzunguka nyumba ambayo tuliandaliwa kukaa kwa siku zote. Hivyo baada ya kuripoti tulionyeshwa eneo tukaambiwa ikifika saa 11 jioni uzio uwe tayari, hapo hatuna Matete, hatuna kamba, hatuna mirunda nk nk. Kazi ilianzia hapoooooo unyama unyama tuuuu zaidi ya depo ya mgambo.
Mengine yaliyoendelea tuliambiwa habari za jandoni zinaishia jandoni hazivuki mlango wa Uzioooo.... ovva.
 
Nilitolewa nyuzi bila ganzi,Nadhani hakuna rangi sikuacha kuiona. Sipati picha watu waliokatwa bila ganzi 😓😓
KWINGINE hakuna kuoga maji safi,ni kupakwa tope zito mwili mzima kipindi chote cha jando/tohara. Unawekewa mwangalizi kukuchunga dushe lisidinde,likidina unagongwa enka miguuni ili dushe lisinyae,lengo ni lisipasukepasuke na kuanza upya kupona.Changamoto nyingine ni kutahiriwa bila kupigwa sindano ya ganzi,hayo maumivu ni balaa usiombe utahiriwe bila ganzi,halafu kisu chenyewe cha kieny
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom