Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Million 4 nazo ni pesa za kusimulia watu?
Kila mtu na level yake ndugu....

Kipindi hicho alitoka kumaliza tu chuo .... huoni hiyo hela ilikuwa kubwa? Sio ilikuwa kubwa tu bali ni kubwa sana tu kulingana na maisha yalivyo.... wapo wenye magenge madogo ya mboga unakuta mtaji haujafika hata elfu 30, na wapika maandazi mitaani je?

Pia unaweza ukawa na mtaji wa milioni 500 ukajiona upo juu wakati hiyo milioni 500 kwa mwingine ni upuuuzi tu.

Jua tupo tofauti kimaisha mwingine akipata 5000 kwa siku anajiona yeye ndiyo yeye kulingana na maisha yake na yupo ambae 1000 kwake ni mtihani kupata kwa siku...

Hatulingani kila mtu na level zake kimaisha.
 
Back
Top Bottom