Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Pole sana mkuu, hii thread yako inanikumbusha ndugu na jamaa waliofilisika, nami kupitia wao nimejifunza vitu vingi sana katika maisha, kwanza nnaamini hakuna ajuaye kesho yake, pili kufilisika haina kesho, tatu usijivune ukiwa navyo(usiwadharau wengine), nne kuwa na nidhamu ya pesa(kimatumizi), tano epuka kukopa kiwango kikubwa cha mkopo na pia usiwe mwepesi kukopesha na n.k
 
Kufilisika maumivu yake yasikie tu acha yakupite bila kukugusa, Eeh Mungu naomba sisi vijana tuepushe na kikombe hiki in case ikatokea mazingira hatarishi katika utafutaji wetu wa riziki maana kwanza kibongo bongo jamii itakuchukulia kama wewe ni fala flani hivi failure uliyekosea target ya kile kizuri ulichokuwa umekipanga na hali hii itazidi kukuchanganya kama hujaishia kuokota makopo sijui!!! Noma sana.
 
Nilipewaga dola 100 zamani sana na danga limoja hivi aiseee kwa kipindi kile ilikua ela nzuri nikaja nikaila bila kuelewa imepita wap
Nikaja kupewa tena mil1 na hilo hilo danga zamani kidogo nayo haikufanya la maana
Nikaja nikapata danga lingine likanipa m2 nazo nimefanyia kazi haikuzaaa
Tangu wakati huo miaka imepita sitaki tena ela za madanga,nimeolewa na nina tafuta hela kialali
Msiwashangae kina wema hela za kudanga hata upewe bil 1 huwa zinayeyuka
Pesa za kuhongwa zina mikosi, kama ilivyo za wizi
 
Pole sana mkuu,hii thread yako inanikumbusha ndugu na jamaa waliofirisika,nami kupitia wao nimejifunza vitu vingi sana katika maisha,kwanza nnaamini hakuna ajuaye kesho yake,pil kufirisika haina kesho,tatu usijivune ukiwa navyo(usiwadharau wengine),nne kuwa na nidhamu ya pesa(kimatumizi),tano epuka kukopa kiwango kikubwa cha mkopo na pia usiwe mwepesi kukopesha,na n.k
Sure, very true mkuu, bless up.
 
Back
Top Bottom