Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Basi Mungu ni wa neema na rehema,Uponyaji wake hauchunguziki.
 
Nakumbuka miaka ya 2005 natokea babati naenda tarangire nilikuwa nimelewa sana nasukuma PUMA TD6 mvua ya hatar kuna vikona havieleweki hapo kati wanapaita kona S hahahah nikakutana na nusu mkate ka RAJU wahind flan waliokuwa na magari ya usafir babati, Jamaa akanibana kaganda katikati ya bara bara mbuuuuuula nakujakustuka naona naserereka pombe ikakata kwa muda mungu bariki tuligonga ngema ila Raju bofla kalianguka kabisa,
Ila sikomi napiga pombe na kuendesha ila tokea ile ajali nimekuwa makini sana nikilewa hata vipi wewe niweke tu kwenye staring nafika kabisa sema kushuka ndio kitendawili sasa
Kwann unahatarisha maisha yako namna hii
 
Me wakati naanza kujifunza gari mwaka 2003,nilikurupua gari yangu baada yakumaliza kuoshwa ilikuwa ISUZU JOURNEY MINIBUS, ,,,BASI BREAK ya kwanza nilimgonga mtu then nikaenda kuvaa Fensi ya mtu,,,,gari ilichakaa na jamaa alivunjika mkono na mimi mwenyewe nilizimia kwenye stering nikaenda kuzindukia lockup sina leseni wala chochote ,,, sitoisahau Ile ajali, ,,,,,,,,
Ikawajee mkuuuMaana hapo leseni huna si hela nyingi ilikutokaaa
 
Sisahau niligonga treka usiku mnene nilikuwa kwenye pikipiki nikajua pikipiki mwenzangu anakuja mbele kumbe trekta lina taa moja. Kuzinduka nipo peke yangu saa tisa usiku huku majeraha kibao mguu umeteguka maumivu makali na baridi balaa. Nikaisogelea pikipiki yangu kwa kujivuta nikaiwasha ikawaka nikapanda mwenyewe mdogomdogo hadi hospitali. Kufika mapokezi ndo nawekwa kwenye machela. Sitasahau
Aisee sasa waliokuwa wanaendesha trekta hawakukusaidia????
 
Tarehe 1/7
tabora hapa nipo napikipiki nazndesha mwenyewe mwendo wakawaida kabisa kutahamaki jiwe kubwa mbele yangu hapa na hapo aiseee nilitahamaki tu ...
Sikuelewa kilichoendelea nazinduka nipo home watu walenijalia nimeshonwa usoni nilipokuwa nimepasuka pia kuwekwa ma bandage kibao meno lawili yamekatika majeraha kibao.nastuka naqhangaa what happened wananipa uji nilishapigwa masindano ya hatari....
Ila sasa naendelea vizuri namshukulu mungu maana nilinusulika.....
Ajali sio mchezo
Kwamba ulitibiwa ukaruhusiwa kabla hujazinduka?
 
Uzi wa kijinga huu Sijapatapo kuona.

Ajali badala kumshukuru Mungu upo salama nyie mnatangaza hapa.

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliiondokewa na ndugu, jamaa, marafiki, watoto, wazee wao kwenye ajali?

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliolemaa maisha kwa ajali?

Huu uzi ufutwe, ni upumbavu wa hali ya juu kuuwacha hapa.
Huyu dada bhana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom