Tuliowahi kukutwa na ushamba mara baada ya kununua gari kwa mara kwanza tukutane hapa

Mara ya kwanza kumiliki gari baada ya miezi miwili hivi mlango wa nyuma kwa abiria ukawa haufunguki kwa ndani, basi siku nimeenda kufanya service ya gari, nikamwambia ilo tatizo fundi, nikaona anatabasamu tuu alafu akasema ngoja ampigie fundi wa umeme, fundi kaja kachokonoa kiana mara mlango ukawa fresh, wakanitoa upepo kidogo. Daaahh nilipokuja kugundua shida ilibidi nicheke tuu.
Baby lock, mafundi magari ni sawa na mafundi electronics wanapiga hela za bure kutokana na watu wengi kutokuwa na ABC za vitu husika.
 
Mara ya kwanza, kabisa nipo zangu na Corola yangu, siku ya tatu tu, toka nimeletewa toka DSM!

Nikawa nimekaa ndani, nimefunga door na window zote, nakula kiyoyozi! Sasa kuna jamaa ni mtani wangu, akachukua maji akiwa kwa nje, akamwaga pale kwenye wind screen, aiseee,nilikwepa kama vile yanaingia ndani! Jamaa alicheka sana, akasema kweli wewe hizi mambo ni ngeni kwako.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mara ya kwanza,kabisa nipo zangu na Corola yangu,siku ya tatu tu, toka nimeletewa toka dsm!

Nikawa nimekaa ndani,nimefunga door na window zote,nakula kiyoyozi! Sasa kuna jamaa ni mtani wangu,akachukua maji akiwa kwa nje,akamwaga pale kwenye wind screen, aiseee,nilikwepa kama vile yanaingia ndani! Jamaa alicheka sana,akasema kweli wewe hizi mambo ni ngeni kwako

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ile nimefika destination sijaweka parking nang'ang'ana kutoa ufunguo, aisee nilipambana weeee ngoma haitoki, ile nagundua sijaweka parking kijasho tayar!

Next time nimewasha taa ya kumulika ndani, sijaizima wala nini nikafunga gar nkaenda kuangalia mpira. About two hour ngoma inavuta betri tu.

Kisanga kingine namaliza kupak nimetoa ufunguo, ile nazungusha steering kidogo tu, ngoma inajilock. Hapa kwanza nilikaa nkatulia nkapata wazo la kuingia google. Case solved.

After those, ushamba wa gari wote ukaishia hapo.
 
Jamani wale tuliokutwa na ushamba baada ya kumiliki gari kwa mara ya kwanza tulete visa tulivyokutana navyo hapa.

Binafsi baada ya kununua premio nilikuwa naiendesha huku nikiwa nimewasha handbreak kiasi kwamba mafuta yalikuwa yanaenda mengi Sana kwa kutembea huku nimeshika handbreak...

Je wewe ulikutana na ushamba gani?

Tiririka.

NB: Kama huna Hela za kutosha usinunue gari
Uwe na balance ya kama shiling ngapi ndio ununue gari au uwe na kipato cha shiling ngapi kwa mwezi na mwaka ndio ununue gari nijibu
 
Mimi na bro tuliiba gari ya mshua ilikua RAUM old model kipindi hiko ndio nyukwaaaa.... Tukawasha AC kali kufika kijitonyama play ground kuchungulia chini tunaona gari inavuja oil tukasema tumepasua sample.... Almanusura tuite fundi. Kumbe ni maji ya AC ndio yanatema. Bila kunusa yale maji tungeliwa na fundi.
 
Back
Top Bottom