Tuliowahi kukutana na wanyama wakali tukutane hapa!!

Pole mkuu umepitia magumu kiasi
Na mimi nipe pole...!!! Juzi kati nilienda kumtembelea anko, kijijini. Basi bwana, si unajua mambo ya shamba, kulikuwa na togwa ya kutosha. Anko alikuwa ameitengeneza togwa hiyo mida ya asubuhi. Kipidi hicho, sisi tulipenda shamba na wapwa zangu wengine. Tuliondoka 11.00 alfajiri na saa 5 ya asubuhi hiyo ndiyo tukarudi huku kijua kinawaka haswa. Kufika tu nyumbani, tukaikuta togwa. Basi kuiona togwa tu ! Nikainywa togwa kama sina akili nzuri ukizingatia nilikuwa nimetoka kwenye "jembe" na kijua kinawaka haswa.

Sasa sharti la kujaza togwa tumboni lazima upunguze maji mengine yaliyokuwa mwilini. Msalani, palikuwa mbali kidogo na nyumba na anko. Anko alikuwa amejitahidi kufuata mashari ya utengezaji wa "msalani". Upande mmoja bafu upande mwingine ndiyo msalani kwenyewe. Na jengo lenyewe la msalani lilikuwa kwenye maeneo ya miti miti. Kipindi hicho, miti yenyewe ilikuwa ndiyo inamalizia kupukutisha majani kutokana na jua kuwa kali kwa majira hayo ya mwaka. Hivyo, na hapo msalani jua lilikuwa linawaka kweli kweli. Kwa kuwa 'msalani' ulikuwa umeezekwa, palionekana kama eneo la kupumzika maana kuna kivuli cha paa. Usafi ulikuwa mzuri sana msalani hapo, hivyo harufu mbaya za msalani hazikuwepo.

Basi bwana! Na mimi na haraka zangu za kupunguza maji maji mwilini ili nikaongeze togwa nyingine, nilielekea msalani. Nikafika msalani, niikafungua mlango wa msalani na nikazama kwenye msalani huo huku nina kopo na kindoo changu cha maji. Wakati naingia kuna kitu kilinigusa sikioni ila sikujali sana nikadhani labda majani ya mti yanayodondoka na kwa kuwa kulikuwa na kiupepo kelekea upande huo. Kumbuka msalani huu haukuwa na paa refu na kulikuwa na uwazi kati ya paa na ukuta ulipoishia. 'Matundulizi' hayakuzibwa. Halafu kulikwa na kidirisha kidogo cha kuingiza mwanga. Nilipozama humo msalani, akili zote zipo kwenye togwa! Jamani nyie acheni tu!. Ndugu wasomaji, mkumbuke kuwa nina miaka kumi na tano sijaonja ' masanga' (nadhani neno linaeleweka kwa wadau au nao wameishakuwa wahenga) na sitegemei kuonja masanga; hivyo, nikisema akili zangu zipo kwenye togwa mnielewe tafadhali. Nisiwachoshe! Basi nikapunga maji yasiyotakiwa mwilini kwa wakati huo, nikamaliza kupunguza maji hayo ya mwilini hapo msalani na nikanawa kama ada.

Sasa nataka kutoka nje ya msalani, pale juu ya mlango nikaona kajitu kama unyasi mnene wa kijani kamening'inia. Kutazama juu zaidi kwenye matundulizi la aulah!!! Nyoka wa kijani mnene vya kutosha, nikamuona amejilaza pale. Akili iliyonijia ni kuwa, nyoka huyu anasumu kali akikugonga ni kwishiney!!! Kibaya zaidi yeye alikuwa kwenye nafasi nzuri kunishambulia. Yaani, nilikuwa nasikia watu wanasema ukikutana na chui nywele unahisi nywele kusimama ama kunyonyoka. Mimi nilihisi vyote ! Yaani nilihisi nywele kusimama na nilihisi nywele zinanyolewa tena kwa kipande cha chupa ya kioo iliyovunjwa...! Jamani acheni jamani ! Kama kawa ikaja akili ya kujiokoa kwa haraka, Aisee akili iliyokuja ni kawaza kutorokea kwenye kale kadirisha kadogo ka msalani! Kugeuza shingo, kuelekeza macho kwenye kadirisha...Balaa lingine...!!!! Kumbe kuna nyoka mwingine wa kijani kajilaza pale ila kichwa chake hakionekani! Pia yeye alikuwa mdogo kwa kipenyo cha 'kiwiliwili' chake....Yaani sasa nimewekwa mtu kati na na nyoka wa kijani wawili na niko msalani!!

Aisee! Ndugu msomaji ebu fikiria ! Mkumbuke vyumba vya msalani ni vidogo...!!! Silaha niliyokuwa nayo ni kopo na ndoo. Aisee, akili sasa ikabidi niamishie kwa huyu wa mlangoni! Nikamuangalia tena, naye akaniangalia!!! "Tukakutanisha macho"...Ninyi acheni tu...! Msiombe hii hali mkutane nayo! Sasa ikabidi ninyanyue taratibu ndoo na kopo langu usawa wa kifua tayari kwa kujihami. Nikaendelea kumtazama! Naye katoa macho..mwanzoni alikuwa anachezesha ulimi wake...akaacha.! Hapo sasa niko kwenye " defensive mode" maana wote wawili wameniweka mtu kati! Hapo hakuna tena akili ya kuwaza togwa!!!

Tuliendelea kutazamana na nyoka wa kijani wa mlangoni...yaani kadiri muda ulivyokuwa unasogea nikawa naona chumba cha msalani kinazidi kupungua ukubwa kwa kasi ya ajabu !!!Nikatamani niwe kwenye ndoto, kwamba muda si mrefu nitazinduka usingizini... Jamani nyie acheni tu haya mambo ya hatari ! Nikajitesti kama nipo kwenye ndoto kwa kujaribu kung'ata ulimi wangu, nikaumia; nikajua hapa nipo 'live na nyoka wa kijani' ...kwa kama dakika tatu hivi....mara nikaona huyo nyoka wa mlangoni anaelekea kwa yule aliyekuwa kwenye kadirisha kadogo...mimi sasa nikawa naelekea taratibu kwenye kona ambayo ipo mbali na kadilisha hako!!! Baadaye kumbe yule nyoka aliyekuwa kwenye kadirisha akamsutikia mwenzake!!! Akanyanyua kichwa...wakaanza kutishiana...mimi tayari nimeishapata upenyo wa mlango wa msalani...sikutaka kushuhudia kilichoendelea ...mbio...kurudi kwa " nyumbani mjomba!!! Kopo tupa kule kindoo tupa huko...!!!! Hizo mbio achaa....

He ! kumbe nimeandika maelezo mengi hivi! Nyie achaneni na nyoka!!

Kwa maelezo haya, tafadhali nipeni pole wana JF!!
 
Maisha mazuri ni general term na personal perception. Kuna mtu anaishi maisha ya kiporipori anaenjoy zaidi kuliko mtu anayeishi maghorofani sijui na ukisasa.So, wewe ukiona unafurahia maisha ya usasa upo sahihi, na mwingine akiona raha kufurahia uporipori yupo sahihi pia!

Life is all meant to enjoy buddy!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na siyo wote wanaishi mijini wanaishi vizuri pamaja na majumba ya kifahari, wengi wanalala nje, kwenye mabanda ya kukaangia chips.
 
Mwaka siukumbuki, miaka 38 mpaka 40 nyuma, bado nikiwa kijana mdogo, mimi na wenzangu watatu, tulienda kugema urimbo wa kunasia ndege.

Miti inayotoa ulimbo huo ni aina ya mvule, bahati mbaya mimi sikuwa na uwezo wa kupanda miti minene, na ile miti minene ilikua kwenye shamba lililosafishwa vizuri tu.
Kwakua mimi siwezi panda miti ya namna hiyo, nikauendea mti ambao ulikua ndani ya poli, ambao mimi niliuona naweza kuupanda. Wakati niko juu kule kwenye tawi moja, naendelea na ugemaji, nikaona sehemu ya kichaka ambacho kilikua kama umbali wa mita 100, toka mti niliokuwemo.
Kitendo kila cha kichaka kutikisika sana, ikanibidi niangalie nini kinachototikasa pale, wakati nikiendelea kufuatilia, bahati mzuri kwenye lile poli kuna sehemu iko wazi ardhi inaonekana.

Kuja kuangalia nikaona bonge la nyoka, mkubwa sana na ni mrefu mweusi, akielekea usawa wa mti uliko, nikapiga kelele za kuomba msaada kwa wenzangu, ila hakuna aliedhubutu kuja polini, maana hawajui nyoka yuko upande upi.
Mimi akili ikanijia haraka kuhama tawi lile nikahamia kwenye tawi, linalo kalibiana na tawi la mti mwingine, maana wakati ule tulikua na michezo ya kudandia miti kama komba wanavyorukia tawi lingine.
Nyoka aliendelea kusonga hatimae, akalifikia shina na kuanza kupanda kwa kuzinguka. Mimi nikiwa nimetulia kwenye lile tawi nililohamia, nione nini nia yake, alipofika juu, akanza kulifuata tawi ambalo mimi nilikuwemo.

Nilimsubiri afike umbali ambao niliukadilia, nikadondosha panga langu chini, nikarukia lile tawi la mti jirani, kwenye mti ule nilidanda kama mara tatu tu, tayari nikawa nimeshafika chini, nikaokota panga langu kwa haraka nikakimbia, nje ya poli, bila kumtizama nyoka anafanya nini.
Huu mkasi ni naukumbuka mpaka leo.
 
Aisee basi kumbe wengi tuliokulia Tabora tumekutana na majanga sana !! Mwaka 1991 mama yangu alikuwa mjamzito, siku moja usiku mkali kama saa 7 hivi alipata uchungu akihitaji kujifungua, mbaya zaidi kijijini hapo kulikuwa na mkunga mmoja tu wa jadi nae siku hiyo hakuwepo alienda kijiji cha mbali kidogo kutoa huduma na tarehe alizokuwa amekadiria kwa mama yangu hazikuwa sahihi....kwa hiyo tukalazimika kutoka usiku kwa baiskeli tumpeleke huko kwenye hiko kijiji alikoenda mkunga wetu ! Nilikuwa mdogo kwa wakati huo, baba akaniweka pale katikati ya baiskeli (kwenye mwamba tunaita), mama akakalishwa kwenye kiti cha nyuma(nako kiti ni chuma tupu..shida kweli kweli na uchungu anaosikia) mzee akaanza kupiga pedal, katikati ya safari taa ya baiskeli ikawa inazingua mwishowe ikagoma kabisa kuwaka ila mzee akapiga pedal kibishi tu, mwendo wa kama dakika 20 tukawa tumefika kijijini tukajitambulisha kwa vijana wanaolinda hicho kijiji wakatuelekeza alipofikia mkunga tukamfuata, mama akapokelewa akaanza kufanyiwa huduma. Sasa pale ndani kulikuwa kumejaa wanawake tupu na watoto wachanga so sisi tukafukuzwa tukaambiwa turudi kulala tutamfuata mama asubuhi pamoja na mtoto wetu pia tukaambiwa na vitu vya kuleta kutokea home. Tukasepa, ila kwa sababu taa ilikuwa haiwaki tena ikabidi mzee aombe wale vijana watupatie ulimbo ule unaoungua muda mrefu na ile miti inayowaka usiku tutumie kama torch, wakatupatia tukapaka ulimbo tukawasha mti wetu tukaanza kurudi kijijini kwetu huku mie nimeshikilia mti unaowaka then mzee anaendesha bike. Tumeenda tena kwa muda kidogo tyre ya nyuma ikapata pancha hivyo ikalazimu kusukuma baiskeli mdogo mdogo huku mzee ananipigia story za hapa na pale, huku tukiendeleza story nikampokea mzee baiskeli yeye akachukua mti unaowaka mimi nikawa nasukuma huku namsikiliza, mara ghafla tukasikia kama kitu kinakuja upande wa kushoto kwetu kwenye majani yale marefu ya porini maana njia nayo ni ile nyembamba sana ya kupita waenda kwa miguu au baiskeli tu gari haipiti so pembeni kunakuwaga na majani marefu makavu hivi....mzee kugeukia majani ghafla na moto wake anakutana uso kwa uso na CHUI ndo anataka kutokezea huko aingie njiani nyuma yetu....aiseee nilisikia baridi ya ajabu siku ile kuanzia miguuni mpaka kichwani, nikashindwa kufanya lolote, sio kukimbia, sio kujikojolea sio hata kupiga kelele nikabaki nashangaa tu!!!! Mzee alichofanya ni kusogeza mkono wake kwenye bega langu taratibu sana maana tulikuwa jirani sana, akanibonyeza begani then tukabaki tunamuangalia yule chui.... Chui akabaki anashangaa ule moto kama dakika 10 hivi then akageuka akasepa zake....sie tukakaa vile vile kama dakika 10 zingine ndo mbio zikafurumuka baba beba mwanae kichwani mbio ndefu tukaacha na baiskeli pale pale! Kesho yake tulimfuata mama kijiji kizima na mapanga, marungu, mishale na upinde zake na kila silaha iloweza kubebeka!
 
...Miaka inavyozidi kwenda wanyama wakali wanazidi kukimbia mbali na makazi ya watu hivyo kuwaona inazidi kuwa adimu.

Simba
Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa na wawindaji wenzangu 6 (nilikuwa mdogo kuliko wote) tulikuwa kambi poli moja Tabora vijijini. Tulikuwa tumewasha moto huku twapiga story. Hii ilikuwa ni baada ya kumuua nyati mmoja mkubwa, sasa kwa sababu ilikuwa jioni tulishindwa kumgawa na kusafirisha kurudi kijijini, so tuliamua kukaa kibanda cha nyasi kusubiri kukuche. Usiku tulilala kwa zamu ili kuzuia fisi wasiharibu kitoweo chetu.Usiku huo ilikuwa ni mwendo wa stori na kuchoma nyama!! Majira ya kama saa 3 hivi tulighutushwa na kelele za mwenzetu aliyekuwa kalala kibandani, kumbe Simba limemkamata mguu pajani na kuanza kuondoka nae, aisee tulimfukuza huku tunamtupia vijinga vya moto mpk akamuachia jamaa. Mpk leo yupo na alama ya meno ya simba pajani!

Chui
Yes, same kijiji, siku hiyo ulikuwa usiku wa mbalamwezi. Nikiwa nimelala usingizi mara nikasikia kelele za yowe la mwanamke. Haraka niliamka, nikachukua mkuki wangu na kutoka nje huku nikiwa na tahadhari. Kumbe kelele zilikuwa jirani tu, nilinyata kufuata yowe lile! Hatua chache tu karibu na ile nyumba nilikutana uso kwa uso na chui!! Aisee sio kwa jasho lile lililonitoka! Chui alikua keshaua mbuzi wapatao watano!

Nyoka!
Hii ndo ilikuwa balaa. Tulikuwa tukitoka shamba na mama angu jioni kama saa 11 hivi. Nakumbuka I was std 6. Mama alikuwa na kuni kichwani na aliniacha nyuma like mita 120-150 hivi na nilikuwa na gunia la mihogo kichwani na panga mkononi!
Ghafla bin vuu!akaibuka nyoka mkubwa kwa kasi, akasimama mbele yangu na kupuliza mate fuuuuu!
Nilitupa gunia huku nikijikinga kwa panga usoni! Kilichofuata ni mbio kali sanaaa ambazo sidhani kama hata Usain Bolt angenikamata! Sikumbuki ndala zangu aina ya Sky way zilidondokea wapi na muda gani! Mate yalinipata mgongoni kiasi na nilibabuka ka nimeungua na moto mkali!!


Weka kisa chako tukumbukie when life was real life!!
View attachment 1007643View attachment 1007644

Sent using Jamii Forums mobile app
hayo mate ya nyoka yalikupa maumivu? maana unasema yalisababisha uwe kama umeungua
 
Nikiwa mdogo kama umri wa miaka 7-10 watoto pale kijijini tulikuwa na michezo ya kuweka matope kwenye vichuguu halafu mnateleza na makalio . Vichuguu vingine vinakuwaga na mashimo ,Siku moja asubuhi tukiwa tunafunga mbuzi kama kawaida tukaanza mchezo wa kuteleza na tako toka kwenye kichuguu.

Sasa nilipopanda kwenye kichuguu nikakaa karibu na shimo kumbe kobra ndo anatoka shimoni ,kugeuka nyuma tukakutana face to face akanitemea mate machoni . Gafla nikawa naona giza halafu macho yanawasha kama nimemwagiwa pilipili kwenye macho,nikawa sioni wenzagu walinipeleka nyumbani .Kufika nyumbani mama aliniwekea mafuta (Samli ) kwenye macho yaani kupaka kwenye machoni .Nililala kuanzia saa tano asubuhi nimekuja kuamka saa kumi jioni macho yako mekundu yanaona kwa shida ,ila mda ulivyokuwa unaenda macho yakarudi kwenye hali yale ya kawaida kila kitu kikawa poa
 
Nikiwa mdogo kama umri wa miaka 7-10 watoto pale kijijini tulikuwa na michezo ya kuweka matope kwenye vichuguu halafu mnateleza na makalio . Vichuguu vingine vinakuwaga na mashimo ,Siku moja asubuhi tukiwa tunafunga mbuzi kama kawaida tukaanza mchezo wa kuteleza na tako toka kwenye kichuguu.

Sasa nilipopanda kwenye kichuguu nikakaa karibu na shimo kumbe kobra ndo anatoka shimoni ,kugeuka nyuma tukakutana face to face akanitemea mate machoni . Gafla nikawa naona giza halafu macho yanawasha kama nimemwagiwa pilipili kwenye macho,nikawa sioni wenzagu walinipeleka nyumbani .Kufika nyumbani mama aliniwekea mafuta (Samli ) kwenye macho yaani kupaka kwenye machoni .Nililala kuanzia saa tano asubuhi nimekuja kuamka saa kumi jioni macho yako mekundu yanaona kwa shida ,ila mda ulivyokuwa unaenda macho yakarudi kwenye hali yale ya kawaida kila kitu kikawa poa
vipi ulirudia tena huo mchezo.Mungu ni mwema hukuwa kipofu.Pole sana
 
Back
Top Bottom