Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,029
2,128
Wasalaam ndugu zangu.

Kuna hii mikopo inayotolewa kwa njia ya mitandao nadhani wengi wao tumekopa huko. Sababu wana ushawishi mkubwa mnoo wa matangazo yao

M-pawa nilianza kukopa tangu nipo chuo nasoma nilikua nakopa boom likitoka nawalipa alafu nakopa tena nikafikisha hadi 79,000 deni lao, baada ya kumaliza chuo nilishindwa kuwalipa pesa yote hivyo nikalipa kidogo hadi deni likabaki 48,000

Mwaka jana mwishoni nikakopa branch kwakua walikua wana nishawishi kwa matangazo yao ila tatizo mkopo wao ulikua haupandi unaishia 23800 pamoja na riba nimelipa mara tatu.. nikaona niachane nao hivyo deni nnalo la 23800

Nikahamia tala. Hakika tala kwenye kupandisha pesa kila unapo lipa deni wako vizuri na wanapanda kwa 20,000 kila unapo rejesha mkopo wako... Nilikua nalipa deni lao kila baada ya siku tatu nikajikuta pesa imefika hadi 193,000 kwa week mbili na nusu...

Tatizo kwa sasa sina pesa ya kuwarejeshea hao jamaa... Pesa ninayo ipata inaishia kwenye matumizi yangu ya kila siku na pango la nyumba...

Je! Hao jamaa watanifanya nini maana wameanza kunitumia meseji za vitisho.. sijui nitaorodheshwa kama mdaiwa sugu hao m-pawa na deni lao lina miaka zaidi ya mitatu..... Hawa wengine wanasema nitajiharibia CV ya mikopo..

Sina mpango wa kuwalipa Sasa kulingana na hali yangu ya uchumi ila nikipata pesa nzuri nawalipa wote kwa pamoja.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa unakopa mwenyewe tena unapokua na tatizo kwenye kurudisha unauliza endapo hautalipa watakufanya kitu gani?

Sasa marafiki zako na jamaa zako si hakuna anaeweza kukukopesha kwa mwendo huo? Bora uwe unalipa kidogo kidogo kuliko kuweka azimio kwamba hauta walipa.
 
Pesa unakopa mwenyewe tena unapokua na tatizo kwenye kurudisha unauliza endapo hautalipa watakufanya kitu gani?
Sasa marafiki zako na jamaa zako si hakuna anaeweza kukukopesha kwa mwendo huo? Bora uwe unalipa kidogo kidogo kuliko kuweka azimio kwamba hauta walipa.
Hujanielewa... Nimekosa pesa ya kuwalipa kwa sasa ila nikipata watapata pesa yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: cmp
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom