Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

nilidhani nipo pekeyangu :D:D, nikajua hadi nifanye usajiri wa dole gumba ndipo watamaliza kuhakiki lakini hamna kitu.
 
Kila siku wanabadili namba. TALA kuweni wapole nitawalipa soon, mambo bado hayajakaa poa
Screenshot_20190607-105511.jpeg
 

Attachments

  • Screenshot_20190607-105511~2.jpeg
    Screenshot_20190607-105511~2.jpeg
    70.4 KB · Views: 26
  • Screenshot_20190607-105511~2.jpeg
    Screenshot_20190607-105511~2.jpeg
    70.4 KB · Views: 18
Ujumbe wao kwangu suku ya leo.

''Unajua kabisa umekiuka masharti ya mkopo wa TALA kwa kukaa muda mrefu bila kulipa lakini bado hukamilishi mkopo huu, hii ni kama unafikiri kuna siku tutaacha kukudai,ukweli ni kwamba tutaendelea kukupa taarifa kila siku huku hatua nyingine zikiendelea kuhakikisha tunakufuatilia kiundani, miamala yako, mawasiliano yako, na kuhakikisha unapatikana haijalishi ni lini, hakikisha unalipa leo deni lako la TALA kabla hatujakufikia kwani hatutakuwa na huruma''
Hamjui ni kosa kisheria kumdukua mtu bila kibali kutoka mamlaka husika na je mnafahamu kunakitu kinaitwa risk management je mmezingatia haya kabla hamjaanza hii biashara?

Ushauri acheni kuwatisha watu na sms zenu mtajaingia kwenye tuhuma kusababisha vifo visivyotarjiwa kwa watu. Anzisheni taasisi ya mikopo kama zingine na mlipe madeni #kodi ya serikali ndo muwe na haki ya kudai wadeni wenu
 
Habari wana jamvi wenzangu, hivi karibuni kumeibuka wakopeshaji wengi wa mitandaoni, wakiwemo hawa marafiki pendwa wa TALA.

Lakini kinyume na matarajio yao kume kuwa na wimbi kubwa la wakopeshwaji ambao wana yakimbia madeni yao au hata kubadili simu kabisa.

Sasa kitu cha kushangaza mimi mwenyewe nimejikuta nikiwa muhanga wa jambo hilo na hasa baaada ya kupata taarifa nyeti kutoka kwenye jukwaa humu kwamba jamaa wana kwepa kodi ya serikali, hivyo nikaona kumbe hawa jamaa sio waaminifu ngoja na mimi nijaribu kukwepa deni lao ili wajaribu kuangalia ni kwa kiasi gani serikali inaumia kwa kitendo chao hicho cha kukwepa kodi pia.

Lakini pamoja na yote wame kuwa wakinitumia sms kwamba tutakufuata hapo ulipo kama usipo lipa hela yetu leo, kitu ambacho hawajakifanya kila itwayo leo, je nikweli wana ubavu wa kunifuata mpaka home au kwa kazi?

Mlowahi kufuatwa tupeni mbinu na namna bora ya kukabiliana na maswali yao kama wanavyo sema kwamba watakuja na madalali wa yono.
Acha uoga
 
Hawa jamaa walinikopesha kule branch 20,000/= Tala 30,000/= shida yao wanatuma message za vitisho utadhani niliwalazimisha sasa nawatangazia rasmi kupitia JF kuwa nawashukuru kwa kunipa hii elfu 50 (jumla) na kwakuwa mmenivunjia heshima kwa kuniita tapeli hampati hata mia.
Nawasilisha.
Ndani ya maandishi yako nimesoma na nikaelewa tu kwamba kwasasa hauna hiyo pesa ya kuwalipa hao Tala..teh
 
Mimi tala wananidai 36, kiukweli nilikiwa na mpango wa kuwalipa mapema tu hata kama hawakopeshi tena ila issue ndo kama hizo sms za vitisho na udhalilishaji wanatuma usiku na mchana na mchana.
 
Hawa jamaa walinikopesha kule branch 20,000/= Tala 30,000/= shida yao wanatuma message za vitisho utadhani niliwalazimisha sasa nawatangazia rasmi kupitia JF kuwa nawashukuru kwa kunipa hii elfu 50 (jumla) na kwakuwa mmenivunjia heshima kwa kuniita tapeli hampati hata mia ili nihalalishe jina mlilonipa.
Sijaribiwi mimi.
Nawasilisha.
Kaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom