NGolo Kante
Member
- Feb 28, 2017
- 80
- 131
Mnamo Jumanne ya Tarehe 11 mwezi huu (Februari 2020) nilinunua kifurushi cha Internet kwa njia ya Tigo Pesa. Ndugu zangu wana JamiiForums yakapita masaa 24 bila ya kupewa kifurushi wala kupewa taarifa yoyote.
Nilichukua hatua ya kuwapigia Huduma kwa Wateja, nikajibiwa kifurushi changu kitawezeshwa baada ya masaa 24. Kwa hakika nilidanganywa.
Nikawa nikiwapigia simu kila baada ya masaa 24 lakini hakuna nilichosaidiwa zaidi ya kuambiwa nisubiri masaa 24 mengine na hadi leo hakuna nilichorudishiwa si fedha wala si kifurushi.
Huu mtandao umekubuhu kwa huduma mbovu lakini cha kushangaza sasa wamehamia hadi kuiba fedha za wateja.