Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Niliwahi kuchungulia kisima kipindi natambaa... wakati huo Bi mkubwa karudi kwao mwanza baada ya kugombana na mzee... mimi ndio nina miezi sijui mitatu.. miaka ya 70 huko...

Mama akiwa anasukana nywele kibarazani hana habari mimi natambaa kuelekea kwenye kisima cha maji kirefu kweli kweli...

Mama ananiambia alikurupuka kama mshale alikuja mbio akanidaka mguu huku niko nusu nje nusu ndani ya kisima... akawa anatetemeka huku anapiga kelele za kilio...

Alifanikiwa kunivuta akalia mno! Kesho yake alipanda gari kurudi nyumbani [kwa mumewe] ....

Ningekuwa nimeshakufa zamani!
 
Duuh
nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma nilikua napenda Sana kuogelea asa mshua mkali sana hataki tutoke njee asa kunasiku nikapata time ijumaa
Nikapitia kwenye bwawa pekeangu bhasi nikaona hapa hakuna wakunisemelea duuuuh!!!!!!!!!!!?????
Nikaona sio kesi nikajirusha kwenye maji mzeee
Mungu alikua Na Mimi maana sikua Na MTU wala mwenzangu ila kumbe Kwa mbali alikuepo baba mmoja akiwa analima asa kumbe alipoona nimerukia kama mbuzi akajua tu huyu mtoto hajui ndo kuwahi
Kati huo nimejititia kitambo sana nimekunywa vikombe vya maji kama vyote sikujua hata nyumbani nimefika vipi ila ninachokumbuka
MPAKA LEO SITAKI KUJUA KUOGELEA KWA JINSI YOYOTE HATA KUOGA MVIVU
Pambafuu ungekufaa wewe...
 
Niliwahi kuchungulia kisima kipindi natambaa... wakati huo Bi mkubwa karudi kwao mwanza baada ya kugombana na mzee... mimi ndio nina miezi sijui mitatu.. miaka ya 70 huko...

Mama akiwa anasukana nywele kibarazani hana habari mimi natambaa kuelekea kwenye kisima cha maji kirefu kweli kweli...

Mama ananiambia alikurupuka kama mshale alikuja mbio akanidaka mguu huku niko nusu nje nusu ndani ya kisima... akawa anatetemeka huku anapiga kelele za kilio...

Alifanikiwa kunivuta akalia mno! Kesho yake alipanda gari kurudi nyumbani [kwa mumewe] ....

Ningekuwa nimeshakufa zamani!
Duuh maza ikabdi arudi kwa Mzee... Ilikuwa njia ya kuwarusidha pamojaaa kazi ya Mungu bhanaa
 
Niliwahi kuchungulia kisima kipindi natambaa... wakati huo Bi mkubwa karudi kwao mwanza baada ya kugombana na mzee... mimi ndio nina miezi sijui mitatu.. miaka ya 70 huko...

Mama akiwa anasukana nywele kibarazani hana habari mimi natambaa kuelekea kwenye kisima cha maji kirefu kweli kweli...

Mama ananiambia alikurupuka kama mshale alikuja mbio akanidaka mguu huku niko nusu nje nusu ndani ya kisima... akawa anatetemeka huku anapiga kelele za kilio...

Alifanikiwa kunivuta akalia mno! Kesho yake alipanda gari kurudi nyumbani [kwa mumewe] ....

Ningekuwa nimeshakufa zamani!
Daah aisee pole yake mama yako
 
Nimejaribu kuwaza mama aliumwaje tumbo la uzazi kwa presha hii dahunaeza blid siku si zako
 
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.

My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.

Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui).

Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.

Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?

Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa.

Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
Pole ccy but hao (kumbi)×2 wasipo kaushwa vizuri yale mafuta yao ni lazima uendeshe tuuu tena vizuri! Nnaexperience yake kidogo but siwez acha kamwe kuwakula jmn.. utamu wke na chungu wake naujua
Go ahead ujaribu tena siku nyingiiine et
 
Mwaka 2017 April niko zenji, nilikua napenda nazi mno. Nikanunua moja ya 500 nikaenda kibalazani nikala weeee mpaka ikaisha.
Si nikajisahau kama nina vidonda tumbo, usiku wacha nianze kuumwa tumbo.. tumbo limejaaa kabisa, nashindwa kupumua vizuri. Jamani haya maumivu ya tumbo sijui kama kuna mwingine yashamtokea...Maana siku ile nililia kama mtoto mwisho wa siku nilianguka kwenye korido natoka choni..Nikazimia! Nilitapika kila kitu hapo hapo. Niliumwa sana siku iliyofuata.

Hili tumbo hua sijui lilikua linaletwa na nini maana mwaka huo huo tena mwezi wa Tisa niko Dar nilikunywa Soda tu ya Fanta likanishika. Kama kawaida nilianguka Wakanipeleka Hospital nikawekewa Dripu 4 ndio ikawa pona yangu. Naichukia Nazi mpaka leo
Pole baby, kwa hiyo hata chakula cha nazi huli?
 
Mungu hua anatulinda sana kwakweli!
.
.
huu uzi umepita muda lakini ngoja na mimi nishee kidogo yangu!
.
.
nina matukio mawili ambayo kiukweli niliona kaburi hili hapa.
.
.
la kwanza miaka ya nyuma kuna zile dawa za malaria zilikua zikiitwa chloroquine kutokana na uchungu wake walizipaka rangi ya blue na utam kidogo kwa juu.
.
.
nilipokuwa na umri wa miaka kama minane hivi nilikuwa nahimizwa sana kulala mchana, sasa katika harakati hizo siku moja baada ya kuamka nikaona kopo la chloroquine, kwa mawazo yangu nilijua ni pipi, nikazichota nyingi nikazitupia mdomoni..
.
.
kwa uchungu wa zile dawa ukisha zitafuna huwezi zitema basi yale mate nikayameza.. dawa ikaanza kuingia.. macho yakanitoka povu likajaa mdomoni hatimae nikaanza kukata roho 😂😂😂
.
.
katika kutupa tupa miguu niiache hii dunia kwa bahati mama akasikia akamwambia sister mkubwa kuna kitu kimeingia ndani kakifukuze,
.
.
sister kuja alitoka mbio mama mama njoo mwone kindikinyer, mama kufika kuangalia pembeni ananiona ndo nipo kwenye hatua za mwisho.. alikimbia kuomba maziwa kwa mzee maajabu akaambiwa hawezi kupewa kama hajaenda na hela!
.
.
mama alilia lakini wapii!! huku mimi mpaka na miguu nimeshaacha kurusha, bahati nzuri akaja kuna mwalim akasema ukichukua yai bichi na mkaa ukamnywesha atatapika pia..
.
.
basi nikapewa nikatapika walau nikawa nimeponea hapo.
.
.
miez michache baadae yule jamaa aliekuwa akiuza maziwa wakati akicheza ngoma alidondokea mkuki ukamchoma vibaya, utumbo ulitoka nje kwa bahati mbaya watu wakaushika kwa mkono, kitu kilichosababisha baadae uoze, alipelekwa KCMC lakini miezi mitano baadae alifariki! (hua namkumbuka katika sala zangu na mola amlaze pema peponi).
.
.
kila nikikumbuka nawaza nikivyo isogelea kaburi
 
Daaah pole san.

Kumbikumbi nimewala san, nadhan usichokijua ww ni kwamba kumbikumbi hawaliwi hivihivi na ukiwala ivoivo bila chchte basi ule kdg san, ukizidisha kitakupata ulichokipata siku hiyo.

Mm binafsi kuna siku nikiwa mdg nlikuwa naumwa malaria. Bahat mbaya sikupelekwa hospitali kwa sabab ziko mbali na tulipokuw tunaishi ni kijijini san.

Asbh km kawaida wazee waliondoka kwenda shamba, mm huku nyuma nikazidiwa, nilianza kuharisha san na kutapika. Baada ya muda niliishiwa nguvu, nikaendelea kufanya vyote palepale. Mama aliporud saa sita kupika alinikuta niko hoi san, ndipo ikawa hamna namna zaid ya kupelekwa hospitali.

Mzee baba ukawa umetulia unashusha tu
 
58 Reactions
Reply
Back
Top Bottom