GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,902
- 10,503
Niliwahi kuchungulia kisima kipindi natambaa... wakati huo Bi mkubwa karudi kwao mwanza baada ya kugombana na mzee... mimi ndio nina miezi sijui mitatu.. miaka ya 70 huko...
Mama akiwa anasukana nywele kibarazani hana habari mimi natambaa kuelekea kwenye kisima cha maji kirefu kweli kweli...
Mama ananiambia alikurupuka kama mshale alikuja mbio akanidaka mguu huku niko nusu nje nusu ndani ya kisima... akawa anatetemeka huku anapiga kelele za kilio...
Alifanikiwa kunivuta akalia mno! Kesho yake alipanda gari kurudi nyumbani [kwa mumewe] ....
Ningekuwa nimeshakufa zamani!