Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Nimejikuta nacheka tu yaani tumefanana mpaka kiasi cha pesa (cha kupokea baada ya makato) kasoro matumizi ya huo mkopo tu na pia mimi ndo kwanza makato yanaanza nna miaka saba mbele (bora wewe umemaliza)...

Mimi ilikuwa nipate kauwanja home centre lakini sijui hela imetumikaje mpaka leo siamini; tena huo mkopo uliniletea majanga mpaka nikafungua uzi hapa nakumbuka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu kwa kucheka utafikiri mazuri, hapo kwenye kutaja jina la benki pameniacha hoi
Kuna mshikaji ni mtu wangu wa karbu mwez uliopita kavuta mkopo benk flan hv,,,sasa now hana kila kitu,,juzi kati tupo nae mzgon night,,kaamshwa toka usingizin kakurupuka anataja jina la ile benki,,dah mkopo bila malengo ni shida tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa m1 alichukua kama mkopo benki moja sijui kiasi gani. Ananunua kiwanja kibaha akajenga kufika katika linta hela ikakata. Akakosa hata hela ya kodi alipopanga cz makato yalikuwa makubwa hakubalikiwa na kiasi cha kumtosheleza na alikuwa ameoa. Kelele za mama mwenye nyumba ikabidi mkewe akasirike arudi kwao Moshi. Yeye ikabidi ahamie kibaha hivyo hivyo. Sasa balaa hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa mtihani. Ikawa mtoro kazini. Anaenda Mara 1 au 2 kwa wiki kazini. Kesi za utoro zikazidi akasimamishwa kazi. Jamaa kapagawa. Maana hana kitu kabisa. Mkewe wameachana na naskia aeolewa na mtu mwingine. Naskia yuko bagamoyo analima vibarua.

Hahaha duh hiii kali kuliko


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
Yan Shekh hela ya mkopo unanunulia boda boda ya kutembelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, huu uzi unafundisha sana.

Kiufupi sana nisije tambulika kwa mafisi.

Enzi hizo nilikopa 500k nianzishe biashara, yaani ilipukutika bila kujua imeenda wapi. Ikawa ndo hela ya kula na kulipa pango. Nilichoweka bond kikapigwa mnada kwa hasara wahusika bado wakataka niongezee. Wee nkawa mkali coz ni kinyume na makubaliano.

Mkopo ni utumwa. Save pesa, au kopa kwa sababu maalumu.
 
Mwenzenu mi kabla sijachukua mkopo baba alinishauri niwe natuma pesa kwa ajili ya kupata kiwanja na ujenzi baadae, sasa kidume nikajipinda, kila mwezi nilikua natuma laki mbili na yeye aliniambia kiwanja kinauzwa M2. Sasa miezi ilikatika naulizia kiwanja najibiwa pesa hazijatimia hahaha ikabidi nimuulize mama, jibu ni kwamba "Pesa zinatafutiwa mchele ila kapanga akipata pesa atakuja kukufanyia maarifa" duh! Nilikata tamaa ya kiwanja ilikua mwaka 2013. Hiyo ya kwanza;
Ya pili, ilikua mwaka 2015 nilichukua mkopo wa M13, milioni 6 nilizivuruga sikujua hata nilitumia nini, zilizobakia nilimtumie baba aninunulie kiwanja na kupiga japo foundation. Na hapa niliula na chuya, alinunua kiwanja chenye foundation zilizobakia akamalizia nyumba yake nikaahidiwa deni kwamba atakuja kunilipa, ila baba ni baba siwezi kumdai tena na najua silipwi kala mali yake mwenyewe.
Mwisho kuna mpango mwengine nataka nije nifanye kwa siri halafu nine nikwambie, mpango wenyewe ni kuja kununua japo banda la M25 maana nikimshirikisha atakuja kunilamba tena.
Huyo baba yako natamani kumjua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepitia kwa makini sana michango ya wachangiaji wengi kwenye uzi huu.

Kutokana na uzoefu wangu na wachangiaji wengine, kukopa pesa ufanye biashara ikisimamiwa na ndugu au rafiki ni kujitakia kuishi kama shetani.

Watu hutofautiana uwezo na access ya kukopa. Wengine humu nimeona wanauwezo wa kukopeshwa million 10 wengine 20 na wengine mpaka million 200.

Kwenu nyinyi wenzangu tunaoweza kukopeshwa chini ya million 10, hakikisheni kama ndio kwanza tunanza kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara basi tubuni biashara inayoweza anza kwa mkopo ambao unaweza kuulipa kwa kipindi cha mwaka 1 tu deni liwe limeisha. Hii husaidia kupunguza ukubwa wa riba na hata ikitokea biashara imekufa muda wa kusota huwa mfupi sana.

Binafsi huwa na ndoto ya kuwa na mtaji wa hata million 50 lakini hujiambia biashara kubwa kiasi hicho sharti izaliwe na biashara nyingine ndogo niliyo ikopea kwa makato ya mwaka mmoja tu na si vinginevyo.

Kama hatuwezi kuanzisha biashara kwa makato ya mwaka mmoja tu basi hata tukikopa mapesa mengi ya kukatwa mika 4 biashara hiyo haiwezi fanikiwa.

Kama unataka kopa pesa kununua bodaboda ya biashara si kitu kibaya, ila jipime kwanza kama wewe mwenyewe utakuwa tayari kuipigia kazi in case madereva wanakusumbua alafu ukisha kuwa na bodaboda weka mashaliti magumu kwa dereva unayetaka kumkabidhi hasa juu ya upotevu kama itatokea.

Madereva wengi hupoteza bodaboda kizembe sana hivyo ni bora muandikishiane namna atakavyo wajibika kuilipa iwapo itatokea upotevu wowote ule na kama hajiwezi kabisa basi awe na mdhamini wake. Kumkabidhi mtu pikipiki bila mkataba ni sawa na kutupa pesa chooni.

Binasfi niko mbioni kwenda kopa pesa kununua bodaboda ya biashara lakini kama nitakosa dereva wa uhakika wa kumkabidhi mimi mwenyewe nitaingia barabarani kama ufanisi wangu wa kazi nilikoajiliwa utadhorota kutokana na mimi kwenda kazini nimechoka poa tu sito jali hilo maadam nisipopambana na hali yangu hakuna wa kunisaidia dunia hii.
Ulianza vizuri sana...ila huku mwishoni sidhani kama ulifikiri kwa usahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.


Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
This is so touching
Anyways as long as it didn't kill you
I believe your More stronger and Wise now.
Keep on fighting.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii D9 hii ilitaka kunipiga dole la kijambio...
Jamaa yangu alinishawishi sana nitafute 4.8 Millioni nijiunge package ya Gold+ ya D9.
Kwa mahesabu ni kuwa kila week nalipwa 170 USD, hivo kwa mwezi napata 630 USD (baada ya makato) ambayo ni zaidi ya 1.3 Millioni.
Hivo nilikua na uhakika ule mtaji wa 4.8 Millioni ningerudisha ndani ya miezi mitatu hivi na week mbili...

Nikaenda kuomba mkopo taasisi moja hivi, mkopo wa 5 Millioni. Marejesho jumla ningetakiwa kulipa 6.5 Millioni.
Mkopo ilikua nipate cku hiyo hiyo tatizo nilikua sina Salary Slip ya mwezi mmoja hivi, ikabidi niende kuifatilia kesho waniingizie mpunga.
Kesho yake niko njiani kupeleka Slip, nikaingia Jamiiiforums, nakuta uzi watu wanasema Danilo Santana CEO wa D9 amekamatwa na Polisi wa Brazil... Account zake zimekua suspended...

Kubabake, nikageuza kwanza kurudi ghetto. Jamaa wa mkopo kanipigia simu kishenz "Boss mbona hauji, si ushapata Salary Slip.. Wahi nakusubiri uweke signature hapa tukuwekee pesa yako"
Nikamwambia nampeleka mama yangu Kairuki nakuja kesho boss...

Nikasema ngoja kwanza nisikilizie hatma ya D9 kwanza...
Mpaka leo bado natembea na ile Salary Slip kwenye bag langu la Ofisini na bado sijajua D9 itarudi lini.
Kubabake leo hii ningelikua nakatwa mshahara kwa mkopo ulioyeyuka hewani.
we jamaa umepotea mno!
 
Back
Top Bottom