Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.

Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
Pole Sana mkuu
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!
dah Big Chawa
 
Habar wapendwa humu JF

Bila kupoteza muda katika pulukushani za maisha kuwa magumu kuna wakati unaona the only solutions ni kuchukua mkopo katika taasisi za fedha mbalimbali ili kufungua ofisi nyingine itakayokuingizia kipato zaidi.

Ila cha kushangaza sasa unakuta tunaangukia pua na maisha kuwa tete zaidi ya hapo nyuma ilivyokuwa.

Mfano ni mimi; 2013 nilikopa 5 milions kwenye benki ya NMB kwa muda wa miaka 4 ambapo nilipanga kufungua biashra zangu mjini ili sister angu ndio azisimamie huko town basi nikaongea nae akanipa michongo yake ya biashara za mahindi zinavyomlipa anatoa mahindi Dodoma anapeleka Dar.

Akaniambia mimi nitakuwa napata laki 300000 kila atakapouza mzigo at the same time my capital remains costant. Mimi nikachukulia kama biashara ndio hivyo basi nitatengeneza pesa ndefu ndani ya muda mfupi sababu ndani ya mwezi anaenda kufunga Mzigo Mara 3.

Nikamtumia 4.5 milions kwa akaunti na ile laki tano kama kawa nikaitia kibiriti na Toto's za mjini nkajua after 1 week ntaanza kupokea pesa zangu za faida. Hapo salary nlikuwa napokea 190000 net baada ya makato yote.

Kumbe nae sister ndio kawa tycoon wa mjini anazitumbua pesa tu na vibwana vyake mpaka na kuja kumpigia sim vipi mbona kimya hunitumii ile pesa yani amelewa haezi hata kuongea.

Nikampigia kesho yake eti akaniambia aliibiwa pesa yote na hapo alipo amebakiwa na laki 3 tu na ndio anataka alipe kodi ili asifukuzwe kwenye chumba alichopanga. Nilikaaa chini bado nusu nilie ila nikajikaza kiume namshukuru Mungu nlikuwa sina mke wala mtoto.

Maisha yakawa magumu zaidi loan board walipoanza kunikata nikawa sasa kutoka 190000 nkawa napokea salary 135000 na madeni yalikuwa yameniandama sana sikuona raha ya kufanya kazi sababu nlishidwa kumsaidia mtu yeyote nyumbani sio baba wala mama wala ndugu yeyote.

Mungu sio wewe wala mimi; mwaka huu deni likaisha na namshukuru Mungu naishi maisha ya furaha na mwaka huu nitaenda nyumban kuwasalimia since 2012 sijawahi kwenda kabisa.

Kwa wale mliochukua mikopo jamani kuweni makini na yale mtakayoenda kufanya msije mkachanyikiwa mkatamani kujinyonga kama mimi.

Pole kwa yakioyokukuta

Binafsi haijawahi nitokea nikikopa nafanyia swala husika ambalo nilikusudia kabla sijakopa na si vinginevyo.
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!

Alafu pesa ya Mkopo taam sanaa dah acha asikwambie mtuu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Story kama ya kuchekesha lakin usiombe uwe kwenye kipindi kama hicho.

Ushauri wangu usichukue loan kwa kutegemea unaenda anza biashara mpya.

Usichukue pesa alaf utengeneze office

Usichukue mkopo ukafunga harusi.
 
Kama huna source nyengine ya kupata huo mtaji wa biashara, au kutengeneza ofisi, au kuolea (mahari na sherehe) kwanini usichukue mkopo kama fursa hiyo unayo? Au ndo mtu ajichange laki mbili zake mpaka zitimie milioni 5 - 10 ndo aanzishe biashara?
 
UZI HUU UMENIKUMBUSHA MIAKA MIWILI ILIYOPITA DAAAAAAAH:

Mikopo Mikopo Mikopoooooo.
Mikopo ni moja ya janga kubwa kwa watumishi wa serikali walio wengi, hasa Wanajeshi/Askali police/Walimu n.k

Mfanyakazi mwenzangu alikua na demu wake mtamu kiac chake walikua wanaishi pamoja Kama mtu na demu wake, kwa bahati mbaya wote wajedaaaa. (Ni nadra Sana kukuta wajeda/askali police kuoana labda walimu ndio wengi wanaweza vumiliana)

Katika kuishi huko wakakubaliana baada ya muda flani wafanye mchakato wa kuoana, ktk mipango yao mingi waliokua wameiweka pia kujenga nyumba lilikua lengo lao pia. Wakashauriana wakazama bank, jamaa akakopa 25Mill na demu nae kachukua Kama 17Mill.

Pesa ya demu akaunua Gari then Pesa ya mshikaj wakajenga nyumba kwenye Kiwanja Cha demu, bac wakawa wanatembelea gari kutoka home kwenda kazin na wakat mwingine wakipishana shift bac mmoja ataenda na gari mwingine anarudi nalo then anapoenda kulipoti kesho yake anampa mwenzie gar hvyo hvyo maisha yakawa yanaenda.

Bana weeeee baada ya makato kunoga na mshahar ushakua mchache pande zote na walisha zoea maisha flan ya Bata sanaaa. Demu akaanza kuzingua mala asilale ndani akiulizwa na mshikaj anamwambia alikua Lindo la usiku Sasa uzur wake jamaa anajua ratib zao zikoje so kufuatilia kiundan kumbe demu anatoka na Mkuu wa kikosi, wakat mwingine mkuu wa kitengo Cha siraha, aaaaaah mshikaj aliumia Sanaaa, akaja mchana demu wake, bwana weeee jibu alilopewaa ni kwamba hana pesa ya kumtunza hvyo awe mpolee.

Mshikaj akapanic, akamdunda Dem weeee zilichapwa humo ndani vunja vunja kila saman iliyokua mbele yao, mwenyekit wa mtaa ndo kuitwa kua watu wanauana huku nae akafurumshwaa Cha kushangaza mshikaj akatimuliwa pale nyumban Mana alichanwa kua Ile c nyumba yake cox Kiwanja hakina jina lake.

Mshikaj ikabid awe analala zake kambini mtaan kushakua sooo na ndio mwanzo wa kuzidisha kunywa pombe akawa mlevi mzuri tu. Kandri cku zilivyokua zinakwenda washkaj wakawa wanampump kua amlambe risasi manzi coz haiwezekan yeye atumie mkopo wote kujenga nyumba mwisho wa cku apolwe kila kitu, wengine wanasema amalizane na wakuu zake, jamaa akawa mgumu kureact. Cku 1 akatonywa na washkaj zake kua manz wako analiwa ndani ya nyumba aliyojenga yeye kua mara nyingi Gari ya boss wake (boss mdgo) inapak pale home.

aaaaah aaaah jamaa kwann asiende kichwa kichwa yaliyomkuta humo ndani alichezea kichapo Cha kwenda mbele mpk kulazwa, Basi koz issue ilikua inamhusu boss wake wakaifumbia kikosini lkn jamaa alipampiwa na masela baada ya kutoka hosp jamaa cku hyo kawa Lindo kwann asitumia Bunduki yake kumteka Boss wake
Weeee kambi nzima wakadata na wengine kufurahia (lkn yule boss pale kambini watu wengi hawampendi cox anapenda sana Chini za wenzie, so macopro wengi walifurahia lile tukio la mshikaj kumteka jamaa) boss hakupigwa risasi Ila alichezea kichapo heavy kutoka kwa mshikaji na kutelekezwa, bac cox Ile issue ilikua inafahamika kambini kua boss mkubwa na mdgo wanakula manzi ya copro na hata makopro wanawake waliopo kambini wengi walikua wanarubuniwa kimapenzi hasa na huyu boss mdgo, kilichofanyika ni boss mkubwa (mzee wa kambi) ni kuwahamisha kambi wote (copro na boss mdgo) ili wasije uana ingawa copro alipata kifungo Cha muda kambini kabla hajaondolewa Mana ulikua utovu wa nidhamu wa Hali ya juu na Boss mkubwa akawa amejihalalishia kumla manzi mzo kiulaiiini mana mwanzo alikua anajifichaficha.

Washkaj wanasema mshikaj kawa Cha pombe Mara mbili ya alivyokua kambi ya mwanzo.

Hapana chezea mkopo wa miaka 7 aisee.
 
Huu Uzi una visa vitamu vyenye kufundisha na kufurahisha Sana

Kitambo hiko jf was jf
 
Inasikitisha sana mkuu.
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!

UZI HUU UMENIKUMBUSHA MIAKA MIWILI ILIYOPITA DAAAAAAAH:

Mikopo Mikopo Mikopoooooo.
Mikopo ni moja ya janga kubwa kwa watumishi wa serikali walio wengi, hasa Wanajeshi/Askali police/Walimu n.k

Mfanyakazi mwenzangu alikua na demu wake mtamu kiac chake walikua wanaishi pamoja Kama mtu na demu wake, kwa bahati mbaya wote wajedaaaa. (Ni nadra Sana kukuta wajeda/askali police kuoana labda walimu ndio wengi wanaweza vumiliana)

Katika kuishi huko wakakubaliana baada ya muda flani wafanye mchakato wa kuoana, ktk mipango yao mingi waliokua wameiweka pia kujenga nyumba lilikua lengo lao pia. Wakashauriana wakazama bank, jamaa akakopa 25Mill na demu nae kachukua Kama 17Mill.

Pesa ya demu akaunua Gari then Pesa ya mshikaj wakajenga nyumba kwenye Kiwanja Cha demu, bac wakawa wanatembelea gari kutoka home kwenda kazin na wakat mwingine wakipishana shift bac mmoja ataenda na gari mwingine anarudi nalo then anapoenda kulipoti kesho yake anampa mwenzie gar hvyo hvyo maisha yakawa yanaenda.

Bana weeeee baada ya makato kunoga na mshahar ushakua mchache pande zote na walisha zoea maisha flan ya Bata sanaaa. Demu akaanza kuzingua mala asilale ndani akiulizwa na mshikaj anamwambia alikua Lindo la usiku Sasa uzur wake jamaa anajua ratib zao zikoje so kufuatilia kiundan kumbe demu anatoka na Mkuu wa kikosi, wakat mwingine mkuu wa kitengo Cha siraha, aaaaaah mshikaj aliumia Sanaaa, akaja mchana demu wake, bwana weeee jibu alilopewaa ni kwamba hana pesa ya kumtunza hvyo awe mpolee.

Mshikaj akapanic, akamdunda Dem weeee zilichapwa humo ndani vunja vunja kila saman iliyokua mbele yao, mwenyekit wa mtaa ndo kuitwa kua watu wanauana huku nae akafurumshwaa Cha kushangaza mshikaj akatimuliwa pale nyumban Mana alichanwa kua Ile c nyumba yake cox Kiwanja hakina jina lake.

Mshikaj ikabid awe analala zake kambini mtaan kushakua sooo na ndio mwanzo wa kuzidisha kunywa pombe akawa mlevi mzuri tu. Kandri cku zilivyokua zinakwenda washkaj wakawa wanampump kua amlambe risasi manzi coz haiwezekan yeye atumie mkopo wote kujenga nyumba mwisho wa cku apolwe kila kitu, wengine wanasema amalizane na wakuu zake, jamaa akawa mgumu kureact. Cku 1 akatonywa na washkaj zake kua manz wako analiwa ndani ya nyumba aliyojenga yeye kua mara nyingi Gari ya boss wake (boss mdgo) inapak pale home.

aaaaah aaaah jamaa kwann asiende kichwa kichwa yaliyomkuta humo ndani alichezea kichapo Cha kwenda mbele mpk kulazwa, Basi koz issue ilikua inamhusu boss wake wakaifumbia kikosini lkn jamaa alipampiwa na masela baada ya kutoka hosp jamaa cku hyo kawa Lindo kwann asitumia Bunduki yake kumteka Boss wake
Weeee kambi nzima wakadata na wengine kufurahia (lkn yule boss pale kambini watu wengi hawampendi cox anapenda sana Chini za wenzie, so macopro wengi walifurahia lile tukio la mshikaj kumteka jamaa) boss hakupigwa risasi Ila alichezea kichapo heavy kutoka kwa mshikaji na kutelekezwa, bac cox Ile issue ilikua inafahamika kambini kua boss mkubwa na mdgo wanakula manzi ya copro na hata makopro wanawake waliopo kambini wengi walikua wanarubuniwa kimapenzi hasa na huyu boss mdgo, kilichofanyika ni boss mkubwa (mzee wa kambi) ni kuwahamisha kambi wote (copro na boss mdgo) ili wasije uana ingawa copro alipata kifungo Cha muda kambini kabla hajaondolewa Mana ulikua utovu wa nidhamu wa Hali ya juu na Boss mkubwa akawa amejihalalishia kumla manzi mzo kiulaiiini mana mwanzo alikua anajifichaficha.

Washkaj wanasema mshikaj kawa Cha pombe Mara mbili ya alivyokua kambi ya mwanzo.

Hapana chezea mkopo wa miaka 7 aisee.
Bro hii issue naijua mwanzo mwisho naweza kukutajia mpaka vikosi walivyotoka
 
Ila nishawahi Ingia kwenye mahusiano na mwanajeshi hawa watu ni vichomi
 
Back
Top Bottom