Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,563
2,000
Nilichojifunza mimi,usikope ili kununua kiwanja au kujenga nyumba ambayo haizalishi bali kopa na wekeza kwenye kitu kitakachokuwa kinazalisha ili mkopo ujilipe wenyewe
Shida ipo hapo kwenye kuweza kubuni kitu ambacho kitazslisha pesa ili deni lijilipe lenyewe unaweza anzisha shughuli ikafa ukiwa hujapata hata mia. Si rahisi kupata mkopo wa kujenga na kumaliza nyumba hapohapo na kuanza kupata mpunga kutokana viwango vyetu vya mishahara. Hata hivyo yote kwa yote ni kujaribu ukipata changamoto unajifunzia mumohumo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,563
2,000
Baada ya kuchoka mishahara ya wahindi niliamua kujiajiri, nikawa nafanya biashara ndogondogo maisha yanaenda, nilikuwa nachukia Mikopo Sana, baada kuingia Kwenye biashara hukuhuku nikaona bora niingie Kwenye vikundi vya wanawake pamoja na Vicoba, nilikuwa na Vicoba vitatu na vikundi vinne vyote nilikuwa na vihudumia naweka tu Pesa sikopi.

Baada ya story za Mikopo za wanachama wenzangu Sasa na Mimi nikaona acha nikope bank nifungue biashara yangu moja ya uwakika nikakopa mil 10 marejesho miaka mitatu, Pesa yote niliingiza Kwenye mzunguko wa biashara mwaka wa kwanza marejesho yalienda Safi Kabisa mwaka wa pili matatizo yakaanza biashara zikafa nikabaki na shamba la korosho na msimu Kama mnavyojua mwaka kwa mwaka. ikawa ikifika tarehe ya rejesho nakopa Kwenye kikundi napeleka bank ikafika wakati vikoba vyote vitatu na vikundi mpaka wanachama wananidai Huku rejesho bado halijaisha la bank.

Nikavuna korosho nikasema Pesa Itanisaidia kupunguza madeni, mwanaume niliyekuwa naye akanishauri usilipe Pesa yote madeni zungushia biashara Huku unalipa madeni kidokidogo. Pesa nikampa mpenzi tuzungushe biashara akanidhulumu ikafika wakati sina hata mia mfukoni marafiki wote wamenikimbia bank nadaiwa, kila kona na madeni Sina kazi Sina biashara nilala ndani Kisa madeni ya watu ya riba mitaan sitaki kukumbuka nilisota nakusota. Ndugu Zangu ikabidi wajichangishe kulipa Mkopo WA bank iliyobaki maana ilibaki miez michache niliiweka dhamana viwanja vyangu viwili. Wakaona bora wanisaidie kuliko vipigwe mnada wakati nilibakisha kidogo.

Hii Mikopo mingine ya vikundi, vikoba na mitaani watu walinidai mpaka walikaa kimya na kuchoka maana Sina kitu Niko mweupeeeee. Baada ya kuumalizika Mkopo WA bank nikauza kiwanja kimoja nikalipa lipa madeni ya mitaani nikabakiza Pesa kidogo nikaaza na moja biashara

Sasa hivi sitaki kusikia Mikopo, vikoba Wala vikundi maana kwa wanawake wengi humo Ndio Huwa Chanzo cha matatizo na wahanga ni wengi maana humo watu wana ushawishi wa ajabu, Kama Sina najua Sina ila Sina Deni na mtu kuliko huna alafu udaiwe utatamani ufe kwa muda. Mikopo inaumiza .
Ufe kwa mda alafu baadae ufufuke au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,563
2,000
Financial literacy ni jambo muhimu sana. Mikopo ni mitamu asikwambie mtu, ila kulipa ni kuchungu kupita maelezo.

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia ili usije kulia. Ni mkopo wa kiasi gani? Unarudisha kwa muda gani? Riba yake ni kiasi gani? Ni riba ya aina gani?

Vijana wengi sana wanaumizwa ni mikopo hasa hasa ya magari. Unakuta kijana kachukua mkopo 12m, interest 24% per annum. Mkopo wa miaka 3. Wengi hawapigi hesabu kujua ni kiasi gani watalipa mwishoni, kila mwezi etc. Mkopo kama huu, mwishoni mtu atalipa jumla karibu 20ml, by that time ki Alteza kimeshakufa na kimemtia gharama za kutosha.

Mkopo unahitaji umakini mkubwa, usijekuta unalia.
Ila mikopo mingi ukiangalia sana mwisho wa siku unaezakuta riba ni zaidi ya ile inayosemekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,563
2,000
Mm sijawahi kukopa na sitokuja kukopa unajua sababu gani mm ni loan officer wa miaka miwili nadai mpaka mdaiwa akiniona anahisi amemuona Israel mtoa roho yani mda wa ku recovery madeni nadai mpaka najihis kujiogopa yani Kama unatakaa kupungua mwili kwa stress njoo nikukopeshe alafu usilipe unizungushe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anayetaka kukonda bila mazoezi inabidi aje kwako kukopa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chemagati

Senior Member
Apr 3, 2018
122
250
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
pole sana hii ya bodi 15% imeongeza maumivu
 
Top Bottom