Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Wife yupo Dodoma huko serikalini, nafanya shughuli zangu DSM, tangu enzi za magufuli kuhamisha watumishi nikasema ninunue viwanja kadhaa, ashukuriwe Mungu vingine nilijenga na nilipata wapangaji wazuri, in the process kujenga vingine nikaja gundua kumbe ni viwanja hewa, vina double allocation. Kumbe pale jiji kuna vibaka wa ardhi hatari kuliko majambazi ya kutumia silaha haya tunayoyaogopa, Dodoma ni sehemu hatari sana kununua ardhi, tumepigwa tukio moja baya sana na wafanyakazi ardhi jiji, na kamishna wa ardhi Mkoa yule mfupi hana uwezo wowote kutatua mgogoro na ushahidi unaonyesha anashirikiana na Jiji hadi Mathew kamishna mkuu wapo pamoja. ni kama ile ya traffic police, anachukua rushwa halafu anaanza kuigawa kwa DTO, kwa RTO hadi kwa Mkuu wa traffic taifa.
naongea kwa uchungu kwa sababu nimekuja kugundua, walioniumiza sio raia, ni maafisa wa ardhi jiji kwa kushirikiana na kamishna wa ardhi Mkoa wa Dodoma. miezi 6 iliyopita nilienda Dodoma kufuatilia na nilionana naye,majibu aliyonijibu yalionyesha moja kwa moja yeye ndiye adui yangu. sijawahi kuona mfanyaazi wa serikali mwenye kiburi kama yule kijana. na sijaelewa anatoa wapi kiburi. kuna kipindi alikuja Waziri Jerry slaa nikaamini angesafisha wale watu, tutapata haki zetu, lakini alipoondoka tu mtu niliyemweka Dodoma afuatilie ananiambia kila kitu kimerudi kama mwanzo. hivi wafanyakazi wa ardhi mtamwogopa lini Mungu?
Kwanza kabisa, Sina hata haja ya kuomba Waziri wa ardhi afanye assessment ya wafanyakazi hao na kumwondosha kamishna wa mkoa Dodoma, kwa sababu najua hatafanya hivyo, hao viongozi wote wakichaguliwa, huwa wanawatumia haohaoo kutafutiwa viwanja na maeneo ya kupora. ni vitendea kazi vya mawaziri na viongozi. ndio maana wana kiburi na wanajua huwezi kuwafanya kitu.
Pili, Nimeweka hoja ili wale tulioumizwa na jiji pamoja na kamishna yule mwenye kiburi, tukutane, tutoe walau ushuhuda kupooza mioyo, na kupeana mawazo namna ya kuwakabili.
Tatu, Hatuchafui mtu, hatuonei mtu, ila walioumizwa na hawa watu, wanajua ninachoongea. ni maharamia wa ardhi wakubwa mno, wanamiliki ardhi mno, na wana kiburi mno kwa sababu uhamisho wa serikali kuja dodoma uliwafanya viongozi wengi wawatumie kupata viwanja, sasa ile kuwa na connection na wakubwa waliowatafutia viwanja kumewafanya wawe na kiburi kikubwa mno, na kweli, sisi raia tunaweza tusiwe na uwezo kuwafanya kitu.
kilichobaki tunawashitaki wa Mungu tu.