Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Kuna siku nilienda kumsalimia bibi . Wakati wa kwenda nilipanda gari, nilishuka kituoni nikatembea kuanzia saa 9alasiri hadi saa 12 na nusu jioni(Sijui ni km ngapi)
Kesho yake tukaondoka saa 12 nasu asubuhi tukafika saa 4 asubuhi
Pia kuna siku nilitembea kutoka mnazi mmoja hadi ukonga banana. Ilikuwa 1987
Mnazi mmoja ukonga routr yangu ya kukimbia hii nyt kali
 
kuna watu huwa wanasafirisha mifugo kutoka mnadani mpaka mkoa mwingine..
mfano juzi kati nimekutana na jamaa wanasafirisha ng'ombe kutoka mnadani mpunguzi mpaka iringa kwa miguu wako wanne tu af ngombe ziko xa kutosha tu... Siku nikiwa sia mishe nataka niunge msafara for fun kupata experience tu
 
Rudia soma alichoandika. Amesema kuwa kama Marathon km 42 mtu anakimbia kwa Masaa mawili na dakika. 100km huyu mkimbiaji atakimbia masaa 6. Hapo tumeondoa vikwazo kama kuchoka nk.

Hakuna mtu anaweza tembea km 100 kwa siku
Hawa wanaosema wanatembea km 100 kwa siku ni waongo.kuna mtu alishindwa kutoboa km 200 kwa Baiskeli Iringa to Njombe.Iwe anayetembea kwa mguu atoboe km 100 siku moja?
 
Nipo Mkuki house muda huu nataka kutembea mpaka Tazara then Tazara to Mwenge.Nikifika Buguruni. Naingia Ben napiga bia mbili nasepa mpaka tabata relini napiga mbili nasepa mpaka Riverside napiga mbili naanza mdogomdogo kumalizia Calabash
 
mi sijui ni umbali kiasi gani lakini nilitoka ushashi ginery hadi lamadi ili nikale miwa ya bure kwenye shamba la mjomba wangu aliyekuwa akiishi huko...bahati mbaya sana nikakuta alishaliuza hilo shamba!!
 
Acha uwongo ndugu ukonga to mnazi1 km20 za wapi?? Zimezidi km 4 tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe utakua hata baiskeli haujawahi kumiliki
Screenshot_20200514-002518.jpeg
nahapo ni Ukonga had Kariakoo haujafika mnazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 2008 mpaka 2010 Ilikuwa kawaida yetu kutembea kutoka Bihawana secondary mpaka Dodoma mjini kwenda asubuhi na kurudi jioni. Bihawana secondary mpaka Dodoma mjini ni km 20 go and return ni km 40. Ilikuwaga ni kawaida kutembea Kwa miguu waliosoma Bihawana secondary wamenipata
Binafsi nimewahi kutembea umbali takribani kilometer 100.

Ilikuwa ni safari ya kwenda na kurudi na ilinigharimu siku moja ya kwenda na siku ya pili ya kurudi.

ilikuwa nimeelekea msibani na nilikuwa na nauli ya kwenda tu, kwa sababu nikapata company ya mtu ambaye hakuwa hata na hiyo ya kwenda tukaungana na kuanza kupasua pori mdogo mdogo.

Safari ilihusisha kupanda na kushuka milima, mvua ilinyesha na kukatika karibu mara nne ila hatukukata tamaa.

Ninajua watu wametembea kwa miguu umbali mrefu kwa sababu nyingi zikiwemo:
kukoswa nauli
kutafuta kazi
Kuepuka hatari
hakuna namna ya kusafiri
na sababu nyingine nyingi ...

karibu utujuze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom