Tuliosumbuliwa sana na wagumu kina DMX kipindi kile tukutane kidogo tujikumbushe!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,171
2,000
Habarini, Muumba aendelee kuwaepusha na korona! amina!

Tumeshasikia sana na tunaendelea kusikia kuhusu 'dodo' huko mtaani na kuanza kulipwa kwa kodi kwa zile kaya maskini 500 huko tandale. hebu tutoke nje kidogo na wakongwe wenzangu tujikumbushe kidogo wale ambao tuliathirika na 'mgumu' DMX kipindi kile.

Nakumbuka Ruff Ryders anthem ilitusumbua hii kitu balaa, mtaani kwetu vijana kadhaa tulikuwa tunakimbia kwenda shule asubuhi huku tukiimba, hususani kile kibwagizo cha 'WHAT!'. sekondari niliwakuta wenzangu kadhaa walioathirika na huyu jamaa....'what's my name' ilikuwa habari nyingine na ilikuwa inapigwa mara kwa mara kwenye tv na kila ikipigwa vijana walikuwa wanaruka kwa furaha. wengine waliathirika hadi namna ya kuongea kidogo....fokafoka zikawa nyingiii na kujiita women haters, wakiwa wamehamasishwa na kile kitu 'what these b**** want!', aliyomshirikisha sisqo.

Karibuni tujikumbushe kidogo km mpo, kama nipo peke'angu tu poa vile vile!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom