sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 645
wadau tupo kama kawa,wale wazeee wa ipamba mpooooooooooooo?
Mgunya alienda kuwa Headmaster kigonsera akaharibu sahv yuko moshy ni mkuu wa college fulan hvWhat a NOSTALGIA!!! Mkubwa umenikumbusha mbali sanaaaaa. Mimi katika waalimu ambao sitawasaha ni mwalimu MGUNYA!!! Alikua akikubamba mitaa ya Ipamba hospital umekwisha!!! Kabla ya kukugaragaza anakuuliza "UNA KILO NGAPI WEWE?" Duh!! Enzi za Mpogole AKA DUDU, AKA Simba wa Tsavo! NOSTALGIA In deed....
Kwa wale 2liosoma miaka ya 2006/08 tulikuwa na bahati mbaya yaan ndan ya miaka minne wenze2 wanne walitutoka,sababu ni magonjwa km kuhara dam na kipindupindu.Niliumia sana mwenze2 m1 2lishiriki nae mahafali ya ku2agwa alikuwa 4m6 mwenzetu,then baada ya cku km mbili hv akafariki.Sitosahau pia 2lipofanya maandamano ya kumtoa mwenze2 aliyekamatwa ki2o cha police Ipamba,katika hali ambayo hatukutarajia 2livamiwa na wanakijiji waliokuwa na silaha km mishale,mapanga,rungu na kupelekea mwenzetu m1 kufarik na wengine kujeruhiwa.R.I.P kwa wote waliofariki,tunamshukuru mungu tuliotoka salama
Hilo siyo la kuuliza. Wanywaji walikuwa wanakwenda Banavanu, Msiwasi au Ipamba mpaka junction (kilometa 7 toka shuleni). Na wale wataalamu walikuwa wanakwenda kuwapiga stop wakina mama-muuza anapotoka nao sehemu kupeleka kilabuni au nyumbani kwake. Inapigwa ya chap-chap ikibidi nyingine inahifadhiwa kwenye gudulia la lita tano na kufichwa machaka hadi jioni kitu inaibukiwa. Ili wewmuuza uendelee kuipata hela ya wanafunzi lazima uwe na sifa ya kuwaficha wateja wako(wanafunzi) wanapokuja. Maana wakikamatwa suspension au kufukuzwa.Pia shule ilikuwa inamiliki kilabu cha pombe za wenyeji kwa ajili ya staff wake.Vipi ulanzi ulikuwepo kama wale wa malangali?
Sinagogi, kila jioni 1.00-1.30 UKWATA, halafu kuna ratiba ya IPYA.TYCS waliingia kanisani.THISDASO walitumia darasa fulani huku nyuma ya Mandela dom sasa wanakuita Mandela annex. Moja kwa moja, wewe O level ulifundishwa na Sanga ASK na A level ulifundishwa na Sanga N.Ulivipata vitisho vya Dudu na mnyoosho wa Contra. Bila kusahau kuibiwa na Pimbi.
Enzi za Marehemu Mpogole "DUDU"
Mkuu tulikuwa darasa moja! Usiuliuze combination ukaconnect dots
kabla ya kufanya mitihani nadhani ilikuwa May 1990, Dudu alikuwa anachechemea sana nami niliugua sana na ikagundulika nilikuwa na Appendecitis ikabidi nifanyiwe operation. Washikaji walikuwa wakija kunicheck wananiambia Mchungaji wewe uko kwenye selection lol! Nilikuwa naogopa sana, bahati akaja kufa yule dogo Vandu Makoko RIP!
inatia raha sana unapokumbushwa sehemu ulizopitia those days.....nilikuwepo hapa '93 to '96
nawakumbuka sana walimu wangu especially Mr Ugulumu(namheshimu sana,alinijenga sana kihesabu kwa kauli mbiu ya Mathematics is by doing!!!)Sanga ASK-geography,Mazege &mrs Mazege-Chemistry and Add maths resp,Kiondo-Biology,Sigimba-kiswahili....duhhhhh
kuna sister alikuwa anatufundisha kiinglishi alikuwa na matusi huyooooo dunia nzima(aliwahi kumuambia mtu kuwa una miguu kama ya mbu na akamuambia kama umekosa dekio si ungetoa li...r. lako uliburute lisafishe darasa, mimi aliwahi kuniambia wewe hujui kabisa kiinglishi najitahidi tu ili usiniongezee idadi ya Fs ila thanks God nilipata B ),mofuga alinifundisha Livestocking,tolley na wengine wengi kwa maana Tosa walimu tulijaaliwa walikuwepo wengi sana.
Secondmaster wetu alikuwa Contra...duh mzee alinichapa fimbo sita na kuniregister blackbook kisa nimesababisha mche wa mti kufa kwenye kiunga nilichopangiwa, wapambe sasa....!wakati mie nachapwa majirani wangu kwenye kiunga cha usafi wakasogea karibu na alipomaliza kunipa dozi akawageukia wao na kuwaambia kila siku nasisitiza mtu akikosea lazima mmuonye na akikaidi mtoe taarifa mbona hakuna aliyetoa taarifa ya kufa kwa mche huu? basi bana akawaunganisha kwenye kosa langu na kuwalamba stick sitasita pia na kuwaingiza blackbook na tukaongezewa adhabu ya kwenda maliasili mjini kununua mche mwingine kwa gharama zetu na muda wetu...mwe what a punishment!!!kosa langu lilirekodiwa kama ''destroying public properties'' i wish huyu jamaa angekuwa waziri mkuu labda public funds zingesalimika.....
sadly nasi tulimpoteza mwenzetu mmoja tukiwa 4m4,ilituuma sana.......
kuna mengi ya kukumbuka Tosa.....ntaenda tena kutembea na familia yangu....i like the place kwa kweli.