Tuliosoma Shule ya Sekondari Tosamaganga tukutane hapa

Mkuu,

Hapo kwenye bluu, unanikumbusha jinsi alivyofariki kiajabu-ajabu kijana wa Mh. Horace Kolimba(RIP) aliyekuwa akiitwa VANDU MAKOKO. Kijana huyu aliyekuwa kidato cha pili wakati huo alifariki mapema 1990 wakati sisi tukiwa SIX, duu msiba huu ulitikisa Shule!


Mkuu tulikuwa darasa moja! Usiuliuze combination ukaconnect dots

kabla ya kufanya mitihani nadhani ilikuwa May 1990, Dudu alikuwa anachechemea sana nami niliugua sana na ikagundulika nilikuwa na Appendecitis http://www.google.co.uk/search?hl=e...e39IA8&ved=0CC4QvwUoAQ&q=appendicitis&spell=1 ikabidi nifanyiwe operation. Washikaji walikuwa wakija kunicheck wananiambia Mchungaji wewe uko kwenye selection lol! Nilikuwa naogopa sana, bahati akaja kufa yule dogo Vandu Makoko RIP!
 
Mnaficha majina balaa.... 2004 form 6 ndio nimetoka tosa,it was gud time
Akija Zitto, Mfulamagoha, Magesa S na Magesa mgombea ubunge, Masawe T, Mami, Aswile M na Aswile D wote tutawambia twanga salamu halafu endelea. Twendekazi kuizungumzia Tosa boys madogo baadaye wakaiita ya wagumu.
 
Mkuu tulikuwa darasa moja! Usiuliuze combination ukaconnect dots

kabla ya kufanya mitihani nadhani ilikuwa May 1990, Dudu alikuwa anachechemea sana nami niliugua sana na ikagundulika nilikuwa na Appendecitis ikabidi nifanyiwe operation. Washikaji walikuwa wakija kunicheck wananiambia Mchungaji wewe uko kwenye selection lol! Nilikuwa naogopa sana, bahati akaja kufa yule dogo Vandu Makoko RIP!

Rev, nakumbuka pole sana! Ila ukweli Dudu alitisha mno zaidi ya Kitisho chenyewe!!!!!
 
Tosa boys sio wapiga gitaa kama wa Pugu na Minaki.

Tosa huwezi kuifaidi kama
~hujaenda shambani na bustanini Idete
~hujatembea kwa mguu toka Tosa hill hadi Junction kwa miguu
~hujaenda kwa masista kununua "bans"
~hujaenda Msiwasi ground
~hujaenda half mile, the most luxurious place ever in the hill
~hujaenda power station hadi Ipamba

Kakuruvi, hebu ongezea ktk list.

Kuna kitu hapa niongezee wakati nipo Form V kila asubuhi vijana wa O level nilikuwa nawasikia ITV, ITV nikawanajiuliza kwani vipi? kumbe kule half mile kuna sehemu ukisimama unaona ndani mabweni ya wsichana wa Kalenga sec, sasa hiyo asubuhi wanaoga uchi na hali wakijua wanachunguliwa wao kwao ndio furaha, ili uwahi ITV inabidi uamke mapema na kigizagiza, jua likitoka tu ITV inazimwa. teh teh teh
 
Daa jamani mmenikumbusha mbali sana mwaka 1990. Ninaikumbuka Tosa yangu. Ninakukumbuka kule kweny atom. Na idete pia namkumbuka DUDU mungu amulaze mahali pema peponi ndiye aliyetufanya tuwe hivyo kitaaluma ndugu zangu.
 
Tunakuomba utuunganishe tuende tukaikarabati shule yetu Tosamaganga. Imetoa watu mhimu sana katika taifa hili .
 
Hii picha ni Tosa kwa upande gani? Najaribu kukumbuka inagoma!!

MKUU,

Hiyo barabara inayopanda kwenda juu, na watu wengi wengi wanapita ndiyo inayoelekea Tosa. Nadhani kwa mbaaali unaweza kuona paa za Tosa. Kifupi hapa ni majengo ya Ma-father.
 
MKUU,

Hiyo barabara inayopanda kwenda juu, na watu wengi wengi wanapita ndiyo inayoelekea Tosa. Nadhani kwa mbaaali unaweza kuona paa za Tosa. Kifupi hapa ni majengo ya Ma-father.

Jengo la mabruda!
 
aisee hizi picha wee acha tu, mnapakumbuka sinagogi nyie? si mlikuwa mnatuponda mawe wakati tunasali. huyu aliyeleta hii siredi barikiwa sana. mie nilikuwa pale tangu 1991-1997 yaani one to six nilipiga PCM nawakumbuka sana walimu wangu wale wazungu wakemia na yule mdada wa hesabu, halafu usipime fizikia alikuwepo ticha mmoja noma anapanda mpaka mezani ila nasikia alihamishiwa baraza la mitihani.
 
Yaani hapo mmenikonga sana tu... Nilikuwa Tosa tangu 2002-2004 may... Mkangwa anatoka na akaingia Mzee wa cigarette(CHARWE-Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake)... Mwenge ndio Home kwa Tosa.... Maisha Yale yana utamu wake jamani hasa ukifika Ipamba basii whaooo ukiwaona wanafunzi wa Nursing unaenjoy....

Hee Charwe alikuwa h/m Tosa?! Mnoko yule mzee, alikuwa akifundisha biology Pugu 90's.
 
aisee hizi picha wee acha tu, mnapakumbuka sinagogi nyie? si mlikuwa mnatuponda mawe wakati tunasali. huyu aliyeleta hii siredi barikiwa sana. mie nilikuwa pale tangu 1991-1997 yaani one to six nilipiga PCM nawakumbuka sana walimu wangu wale wazungu wakemia na yule mdada wa hesabu, halafu usipime fizikia alikuwepo ticha mmoja noma anapanda mpaka mezani ila nasikia alihamishiwa baraza la mitihani.
Sinagogi, kila jioni 1.00-1.30 UKWATA, halafu kuna ratiba ya IPYA.TYCS waliingia kanisani.THISDASO walitumia darasa fulani huku nyuma ya Mandela dom sasa wanakuita Mandela annex. Moja kwa moja, wewe O level ulifundishwa na Sanga ASK na A level ulifundishwa na Sanga N.Ulivipata vitisho vya Dudu na mnyoosho wa Contra. Bila kusahau kuibiwa na Pimbi.
 
Back
Top Bottom