lugendosisty
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 219
- 102
ahsante kwa kutuwekea hii kitu hapa jamvin......nimekumbuka mbali sana hasa kitimoto ya pale IPAMBA.
Sawasawa nimekosea,nilivyomwelewa guide tulipoenda kalenga,alizungumzia mapigano karibu na ipamba,lakini inaonekana siku zote nilikuwa misinformed au sikuilewa hadithi....I know now!! haibani sana.Acha kudanganya watu hapo penye nyekundu.
Kwanza Mkwawa hakumuua Zelewisky aka Nyundo kwa mikono yake, bali aliuliwa na majeshi ya Mkwawa.
Pili, Nyundo aliuliwa eneo la Lundamatwe karibu Ilula (mpaka leo mnara wa kaburi lake upo just about 20 mts away from Moro-Irg road). Lundamatwe kuna umbali mkubwa sana hadi Tosa.
Tatu, mapigano yaliyohusisha mlima huo (kabla haujaitwa Tosamaganga) kati ya Mkwawa na wajerumani siyo zamu hiyo aliyokuwepo Nyundo.
Naweka sawa tu, tuendelee na mada.
Usisahau SELECTION.Mkuu Kakaruvi,
Asante kwa Kunikumbusha juu ya Tosa Hill, binafsi nakumbuka yafuatayo:
* Nilikuwa pale toka 1988 hadi 1990,
* Nilikuwa nachukua PCM, darasa langu lilikuwa PCM 3,
* Nilishawahi kutembea mara nyingi sana toka njia panda lami (Tanangozi) hadi Tosamaganga,
* Nakumbuka Dansi lililopigwa pale Iringa Girls (Feb-1990) kwaajili ya kukusanya fedha za kujenga madarasa ya F5 na F6, duu ilikuwa balaa kwani TANCUT Almasi, ndo walitumbuiza pale!
* Nakumbuka Mwl. Pimbi(nick name) huyu alikuwa Mwl wa O-level, na alikuwa mnoko mno hasa kwa A-level,
* Nakumbuka pia CONSTANT (fimbo sita), ulikuwa ukiambiwa constant basi ujue ni bakora sita!
* Mwisho, nakumbuka Quarter Mile na Half Mile.
* Headmaster Dudu Mpogole(RIP), alitisha kama Ukoma!!
Duh!! Umenikumbusha mbali. Ilikuwa ikifika Ijumaa jioni mnafanya mchango. Jumamosi anatumwa mtu kwenda Msiwasi au Ipamba kununua kitimoto, nyanya na vitunguu. Ngoma inakuja kukaangiwa msitu wa nyuma ya PCM block (ambalo pia kulikuwa Biology Lab) au ule wa chini ya nyumba ya h/master. Ngoma inaletwa bwenini imekwisha ungwa ama mnaishukia na bonge ya sima ya ugali huko huko kwa msitu utafikiri wapasua mbao misituni.ahsante kwa kutuwekea hii kitu hapa jamvin......nimekumbuka mbali sana hasa kitimoto ya pale IPAMBA.
kakakuruvi daaaaaaa umenikumbusha maana nilikuwa hapo 2004/2006 EGM boy///////////////////////////////////////////////////
Du jamani nami mumenigusa, nilikua hapo 1986-1988, namkumbuka mwl mgunja, da jamaa alikua anacharaza viboko ni balaa, kulikua na mwl mrusi wa physics [velichko] jamaa kumbe lilikua shushushu lilipewa notice 24hrs likarudishwa kwao, aisee mdau hongera kwa kumbukumbu nzuri. Hii picha ya pili hapo juu[ hapo assembly] kama sikosei ni mwaka 1988, John vocent mnaemzungumzia sio yule kipanga wa hesabu ?
Tosa boys who were Dudu's sons, mnakumbuka ile habari ya kuwa Dudu alikuwa anakula watoto wake (mwanafunzi) kila mwaka?
Mnakumbuka jamaa alivyokuwa anatisha?