Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Wabongo wengi wanataka walale alafu waamke kesho wakute wameletewa AMANI na Kigogo au Mange kimambi kwenye sshani.
Sio kweli...usiwadharau Watanzania kiasi hicho.

Tanzania ipo kabla ya Mange na Kigogo kuwepo pia itaendelea kuwepo baada yao hivyo hao wawili hawawezi kuwa tegemeo kwa mamilioni ya Watanzania.
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Dah!!!!,Mungu atakusamehe mkuu
 
Amewanyima tu hao wapinzani ajira ya ubunge, udiwani na hata huo Urais! Ila upinzani hauwezi kufa kamwe. Hata ndani ya hicho chama chake, upinzani na makundi yatendelea tu kushamiri.

Yaani tumerudishwa enzi za Mwalimu! Hovyo kabisa.
Mimi mwenyewe namchukia balaa huyu baharia
 
Majuto ni mjukuu. Sasa mmeturudisha kwenye utawala wa Chama Kimoja. Sio peke yenu. Hata mawakala wa vyama vya upinzani wamechangia haya

Magufuli atasema ameshinda ila CCM na TANZANIA kwa ujumla tumepoteza
Kweli kabisa,tumerudi enzi za Tanganyika na TANU
 
Katiba iliyopo watu wameshindwa kuitumia.

Magufuli kapiga marufuku mikutano kinyume na katiba.

Hiyo mpya mkipewa halafu akaivunja hivyo hivyo, mtafanya kipi cha tofauti?

Mimi naona katiba mpya ni muhimu, ila mara nyingi inafanywa kuwa kisingizio tu.

Katiba haileti mabadiliko. Watu ndiyo huleta mabadiliko.

Sasa kama watu hawana muamko, katiba mpya itasaidiaje?
Katiba mpya muhimu na ikiandaliwa vizuri itaelekeza namna ya kumwajibisha yeyote atakaeisigina bila kujali cheo chake. Katiba iliyopo ni dhaifu sana na udhaifu huo umejitokeza zaidi katika Awamu hii kwa sababu ya uongozi dhaifu katika mihimili yote mitatu ya Utawala ukilinganisha na Awamu zilizopita. Pamoja na mapungufu ya Katiba iliyopo, viongozi wa Awamu zilizopita waliielewa kama ilivyokuwa na kuheshimu viapo vyao walivyoapa kuitii hata mmoja wao aliridhia matakwa ya wananchi ya kuandaliwa Katiba mpya. Awamu hii inaendesha nchi kama hakuna kabisa Katiba walioapa kuilinda lakini bahari mbaya kutokana na udhaifu wake inawalinda wakiivunja maksudi au kwa bahati mbaya.
 
Amewanyima tu hao wapinzani ajira ya ubunge, udiwani na hata huo Urais! Ila upinzani hauwezi kufa kamwe. Hata ndani ya hicho chama chake, upinzani na makundi yatendelea tu kushamiri.

Yaani tumerudishwa enzi za Mwalimu! Hovyo kabisa.
Mkuu 'Tate', Pole sana!

Lakini hasira zisikuondoe akili mkuu wangu: Huwezi kamwe kusema kwa moyo safi kwamba "---tumerudishwa enzi za Mwalimu!"; huenda una maana yako nyingine tofauti kabisa!
 
Huu ujinga umefanyika maeneo mengi sana. Na policcm safari hii wamedhihirisha wazi namna wanavyotumiwa na bosi wao. Alichokisema yule OCD wa Hai, hakikuwa ni kitu cha kubahatisha.

Majibu yameonekana sehemu nyingi. Poleni wote mlio umizwa kwa kunyang'anywa ushindi wenu kibabe! Kisa kuna mtu mmoja tu alipiga marufuku wapinzani kutangazwa washindi.
Kweli mkuu kilipangwa kbs hicho,eti huwezi kushinda wew,huyo ni polisi anaongea hivyo,huu haukuwa uchaguzi
 
Kwani ulilazimishwa kushiriki huo uharamia.. !?? Pumbavu.
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
 
Kwa
Mimi nilitenda haki na CHADEMA /upinzani wameshindwa kwa haki mf kwenye kituo changu kura za urais ccm kura171,CHADEMA kura 36,ubunge CCM kura 151,CHADEMA kura 67 na vituo vya majirani zangu pia CCM imeongoza kwa gape kubwa tu nadhani kuna kitu upinzani wajipange vzr kukifanyia kazi hasa vijijini, wenzao ccm wanamtaji mkubwa sana huko, ukijumlisha na mbwembwe zingine kama TASAF na ugawaji wa nguo za chama yaani huwaambii kitu vijijini.

Sent using Jamii kwa LA kijijin hpna nilkuwa hko vijijini ilula maeneo ya isele na masukanzi nilichoshuhudia kwa macho yangu ni wizi wa wazi mawakala walikuwa wa CCM na chadema vingine havikuwa na mawakala ilipofika mda wa kula wa chadema alipotoka kwenda chooni kura zliletwa na mapoti tukijua chakula uchaguzi ulivyomalizika wakaanza kujisifia
 
Mkuu 'Tate', Pole sana!

Lakini hasira zisikuondoe akili mkuu wangu: Huwezi kamwe kusema kwa moyo safi kwamba "---tumerudishwa enzi za Mwalimu!"; huenda una maana yako nyingine tofauti kabisa!
Kwenye kipengele cha kuhusu demokrasia, niko sahihi bwashee. Mwalimu hakuwahi kuwa mtu wa kupenda demokrasia. Hata yeye mwenyewe huko aliko anatambua vizuri, kuna baadhi ya mambo alivurunda wakati wa Uongozi wake na mengine mengi tu aliyapatia.

Na ndiyo maana alifuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965, aliwashughulikia mpaka marafiki zake wa karibu mfano Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, nk. Kwa sababu tu walitofautiana kwenye baadhi ya mambo. Ni kipindi hicho cha Mwalimu, msemo wa " Zidumu Fikra za Mwenyekiti" ulitamalaki.

Na huyu wa sasa naye ana hulka hiyo hiyo ya kujiona yeye ni Alfa ma Omega! Mawazo yake ndiyo mawazo sahihi kuliko ya wengine! Na pia ndiye Mtawala anayeitendea haki ipasavyo Katiba ya CCM iliyotengenezwa wakati wa Mwalimu ya mwaka 1977! Inayomfanya Rais kuwa Imperial President, Chama kumiliki/kufungamana na vyombo vya Dola mfano polisi, nk.
 
Katiba iliyopo watu wameshindwa kuitumia.

Magufuli kapiga marufuku mikutano kinyume na katiba.

Hiyo mpya mkipewa halafu akaivunja hivyo hivyo, mtafanya kipi cha tofauti?

Mimi naona katiba mpya ni muhimu, ila mara nyingi inafanywa kuwa kisingizio tu.

Katiba haileti mabadiliko. Watu ndiyo huleta mabadiliko.

Sasa kama watu hawana muamko, katiba mpya itasaidiaje?

Alichokifanya Magufuli ni kuua huo Muamko wa kisiasa katika uongozi wake, hii ni pamoja na kukataza mikutano, kufunga wapinzani na kuwafungulia makesi, kuteka na kuua watu, assassination attempt ya Lissu n.k

Kipindi cha JK, muamko ulikuwa mkubwa sana, wapinzani walikuwa wanafanya mikutano mingi ya kisiasa. Ni enzi za JK mbunge anaweza kufariki, uchaguzi ukapigwa na mpinzani akashinda mfn. Nassari, Jimbo la Chacha wangwe, n.k

Sasa Magufuli kajengea watu uoga, yani now days ukiwa nyumbani mkianza kumjadili magufuli lazima mfunge madirisha kwanza.

Lkn pia, naona Upinzani unapaswa kujipanga upya. Kwasasa Mbowe hapaswi kuwa mwenyekiti, ni muoga sana, hana ujasiri wa Lissu au hata Lemma.

Upinzani unapaswa kuwa na kiongozi ambaye ni jasiri, asie muoga ili kuwajengea wananchi ujasiri vilevile.

Muamko wa kisiasa kwa wananchi hujengwa na wanasiasa walio jasiri, wakiwa waoga na wananchi huogopa

Mwisho, upinzani umeshindwa kutengeneza Dar.
Dar ndio kitovu cha siasa, na Nchi ipo hapa.
Upinzani ulipaswa kusimamisha Wagombane wababe na wenye ujasiri.
Imagine Dar ingekuwa na Wabunge kama Lemma, Sugu, Heche, Zitto ingekuwaje?
Sasa wabunge hao wapo mikoani, ambako huko wanategemea Kusikia Dar inasema nn.

Sasa jiji zima unasimamisha wagombea wamepooza, wasio na hamsha hamsha. Mdee kidogo ndo anajikongoja ila hana supports.
 
Hata hivyo Biblia inahimiza kutii mamlaka pia.
Lakini Petro na mitume walipoamuriwa kwa nguvu na baraza (Sanhedrin) wasihubiri tena kwa jina la Yesu walisema, "...Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu" (Matendo 5:29).

Naam, tunaamuriwa kuwatii wenye mamlaka kwa kuzingatia haki ya Mungu, lakini si katika maovu. Maana mwenye mamlaka juu ya wanadamu wote ni Mungu. "...kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu..." (Danieli 4:17).
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.

Ushasema tuheshima mamlaka za juu hiyo katiba nani ataipitisha wakati hizo mamlaka hazitaki katiba mpya.

Tusubirie ccm kwa ccm ndio watatusaidia kukitoa chama na kuleta katiba mpya lkn sio mtz wa chini
 
Acha mbwembwe, nimesimamia kituo kinaitwa Wankorongo, Lissu kapata kura mbili! Kubalini mmepigwa kichapo cha mbwa mwizi, laana ya Dr Slaa hii, mkome kukumbatia wapenda kufumuana mitaro!
Ulipataje hiyo kazi ya kusimamia uchaguzi? Kwa hiyo hata kama kituo kimoja kapata kura 2 ndio iwe Tanzania nzima?
 
Back
Top Bottom