Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Akishinda yeyote kwa HAKi ni sawa.. tatizo ni pale mtu anaposhinda kwa HILA na WIZi kinyume na matakwa ya wapiga kura

Kwahiyo unadai kura millioni zote zimeibwa.. eeeeeh.. zs nani haswa.. Rungwe au? Maana Lissu huyo hakuvutia wananchi.. zaidi ya kutembea kutalii na kuyojua kujinadi..


Chaguo la wananchi
Magufuli oyeeeee
💚💛💚💛💚
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.

Acha uongo..
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
mama D
Haya ndiyo mambo mnayoshangilia
 
Wakishinda wapinzani haki imetendeka, ila wakishindwa hakuna haki, tulia sindano iwaingie
Ni CCM wenyewe ndiyo walisema hata msipowapigia kura, wao lazima waunde Serikali rejea maneno ya Mama Samia na CCM kushinda ni lazima kwa sababu imeshika dola, rejea maneno ya Dr. Bashiru- katibu mkuu. Yapo maneno mengi tu ya kuambatanisha ili kuthibitisha kile wapinzani wanachoamini kuwa haki haijawahi kuwa upande katika chaguzi zote tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi!
 
Nilisema juzi humu sisi wananchi watanzania ni wapumbavu na matahira,kila kitu tumewaachia viongozi wa upinzani nao wamechoka maana hawapati sapoti yoyote kutoka kwa wananchi.

Hata leo hii tukabadilishiwa katiba tukapewa ya USA,kama Rais ni magufuli atafanya against ni hatutafanya chochote.

Ngoja tuungane na wenzetu waganda na Rwanda kuhalalisha upumbavu wetu wa kiafrika.

Mfumo wa vyama vingi ni mzuri, lakini hauna meno ya kutosha kumdhibiti Rais anayeamua kukiuka chochote. Bunge la vyama vingi, pamoja na kwamba ndilo lenye mamlaka ya kumdhibiti Rais, siku zote linatawaliwa na partisanship. Muda wote Rais anakuwa na allies wa kutosha kumlinda Bungeni kwa sababu ni wa kutoka chama chao. Na kumpiga chini President unahitaji baraka ya 2/3 ya wabunge. Kuipata hiyo kwenye Bunge la vyama vingi is practically impossible.

Tuliona hata Wamarekani walipojaribu kumpiga chini Trump; senators wa chama chake walikataa kumtia hatiani mchizi akanusurika! As a matter of fact, katika historia ya nchi yao, hawajawahi kumng’oa Rais wao kwa mtindo huo. Mmoja tu ndiyo aliamua kuachia ngazi mwenyewe kabla ya mashitaka dhidi yake kuanza kusikilizwa na Senate. Naye angekomaa pengine angechomoka kwa sababu hiyo hiyo ya partisanship.
 
Hiyo katiba mpya itapatikana vipi bila CCM kuwekwa oembeni kwanz?

Nionavyo ili CCM itoke cha kwanza System ya nchi iwachoke hapa nazungumzia TISS na JWTZ
Hao wawili hawawezi kuchoka wao wanapata stahili zao sio kama wengine
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Una tabia za kimalaya malaya
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
 
Chama Dola!!! Ujanjaujanja Tu Umesaidia Hili Zoezi
Haki Iko Kwa Mungu!!!
 
Kwa hiyo wakiwekwa wasio wateule wa rais tumemaliza tatizo?

Hao wabunge wa upinzani waliotoka upinzani na kwenda CCM walikuwa wateule wa rais?

Joshua Nassari alikuwa mteule wa rais?

Unahitaji kuwa mteule wa rais ili kurubuniwa na CCM?
In his idea ni kuwa ukiteuliwa na rais ni rahis kuwa manipulated. How?
Kama kauli alizotoa hapo nyuma mhe.rais. you can see no body anadhubutu kwenda kinyume na command zake. He can simply remove you kutoka kwenye hiyo nafasi if hutafanya anavyotaka yeye.
So ile chain ya wateule wa rais.. ukiacha mbali wabunge. Ile chain mpaka kwa wakuu wa wilaya ni copromised tayari.
 
Nipo mkuu.

Tutaelewana tu hata kule kwingine.My epistemology is consistent.

Contradiction ni pale wanaompinga Magufuli kwa kujikita kwenye maendeleo ya vitu (ndege, barabara, fyovers etc) badala ya maendeleo ya watu (afya, elimu), wao wenyewe wanaweka kipaumbele kwenye maendeleo ya vitu (katiba mpya) badala ya maendeleo ya watu (elimu ya uraia kuweza kutumia katiba hata iliyopo sasa).

Hii ni contradiction miongoni mwa wapinzani wa Magufuli wanaotaka kuanza na katiba mpya kama suluhisho la matatizo yetu.

Katiba mpya ni moja ya tool muhimu.

Lakini kama tool yoyote kwenye toolbox, ili tool iweze kuwa na tija, inabidi awepo mtu anayejua na anayethubutu kuitumia tool.
Yeah but kama huyu mtu anaitumia tool vibaya what should we do? I say tu modify hiyo tool.. ili anae itumia asiweze kuumiza wengine.. iwe effective only kutumikia wananchi but akitaka kuvuka mipaka iwe na limit asiweze.
 
Kwa Katiba na tume ya uchaguzi wa namna hii hata siku moja tusitegemee uchaguzi huru na wa haki. Na tatizo vyama vyetu vya upinzani hawana hata mbinu moja dhabiti ya kukabiliana na madhila haya. Tutabaki kulialia sana na ccm itaendelea kuongoza kwa mabavu.
 
Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Umejisahau mkuu.

Kwa hayo uliyoyaeleza hapo juu, sasa Katiba Mpya itapatikana vipi?

Hizi mamlaka ulizozitii katika uchaguzi huu utakuwa umeziondoa vipi ili upate hiyo katiba mpya?

Kwa mtu kama wewe, niseme tu kwamba hata "Pole" hustahili kupewa. Ni bora ungemezea tu ubaki na maumivu yako moyoni peke yako kwa kushiriki katika kulihujumu taifa lako.

Sikuonei kwa kukulaumu, lakini umeshiriki hujuma, halafu unatafuta kujikosha?
 
Niliwaza endapo hao waliotangazwa wangeanza uliwa mmoja mmoja nadhani ingeleta hofu sana hata yeye angeogopa na mtu pia angeogopa tangazwa kwa matokeo ya kufoji
 
Back
Top Bottom