#COVID19 Tuliopitiwa na wimbi la 3 Mwenyezi Mungu akatuokoa tukutane hapa

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
2,131
1,808
Habari Wana JF wenzangu.Kama kichwa kinavyo jieleza.

Kwa wale tuliopitiwa na wimbi la 3 na Mwenyezi Mungu akatuokoa tubadilishane mapito na Aina ya tiba tulizotumia na zika tusaidia .
Binafsi nililala kitandani kwa takribani wiki 3.

Hali ilianza Kama utani,baridi Kali Kisha homa Kali halafu ikafuatiwa na maumivu ya mwili mzima. Baada ya Hapo ikaja Kubanwa mbavu lakini sikohoi Wala sikuwa na mafua.Cha ajabu nilicho kihisi Ni makohozi kuziba bomba ya kupitisha hewa kooni.

Kipindi hiki nilipelekwa hospitali nikapata vipimo lakini hakuna ugonjwa ulio onekana katika vipimo hivyo, nikapewa AZUMA, CIPRO NA PARACETAMOL. Kiukweli hizo dawa hazikunisaidia kabisa nikalazimisha kutumia dawa za asili kama

1.Limao

2.Tangawizi

3.Kitunguu Swaumu

4.Basil Tea

Baada ya siku 3 za matumizi ya tiba hiyo hali yangu ikarudi kuwa ya kawaida na sasa naendelea vizuri.
 
AZUMA ya siku tatu ndio iliyofungua hayo mapafu. Hizo dawa zimeokoa wengi na hili janga.

Pia Paracetamol, vitamin B Complex kuleta hamu ya kula, PedZinc, na matunda kwa wingi.

All in all mponyaji mkuu ni Mungu.
Hakika Mkuu.NAMSHUKURU MUUMBA WA ARDHI,MBINGU,VILIVYOMO KATI YA MBINGU NA ARDHI.KWA KUNIOKOA HALI HAIKUWA NZURI
 
AZUMA ya siku tatu ndio iliyofungua hayo mapafu. Hizo dawa zimeokoa wengi na hili janga.

Pia Paracetamol, vitamin B Complex kuleta hamu ya kula, PedZinc, na matunda kwa wingi.

All in all mponyaji mkuu ni Mungu.
Azuma tena vipi inatibu covid?
 
Back
Top Bottom