Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Binafsi nilighairi kutoa mahari kubwa baada ya kukuta watu walisha desilt ,mali yenyewe haikuzidi 500,000 gharama zote na ndoa siwezi funga na mtu sijamkuta virgin na Kati ya hizo 200,000 ni nauli maana ni mkoa A na J
 
Inapendeza, hata hao wanawake waolewe pia na wanaume wawili au watatu ikipendeza wa4, kwani kuna shida pahala!
Kama wewe ni Mwanamke jaribu kuolewa na Wanaume watatau au wawili kisha uje kutoa mrejesho.

Unatakiwa uwe unafirikiria kwanza kabla ya kuandika, mnafikiri haya mambo yametokea tu kusikojulikana au hakuna sababu na hekima ya kuwa kama hivi yalivyo ?
 
Shida ipo kwenye asili maana mwanamke hawezi kuolewa na wanaume wanne maana atateseka kwa kuwa hata akipata uja uzito ni vigumu kujua ni wa nani kati yao. hata kama ataamua kuwazalia kwa zamu bado hataweza maana kila uzao ni lazima apumzike miaka miwili hadi mitatu sasa huyu wa nne atazaliwa lini.

Kingine mwanaume ana sifa ya kumiliki siyo kumilikiwa (ni asili imeamua) angalia hata wanyama. Suala la Mwanamke kulala na wanaume wanne kwa wakati mmoja linawezekana kibiashara kama mwanamke huyo ni Kahaba, lakini kwa ndoa halikubaliki, Hata angekuwa Kaka yako anaingia kwenye ndoa ya mke mwenye wanaume wanne usingemuelewa.
Watu wengi hawajui ya kuwa haki huchaguliwa na maumbile.

Kadhalika hawajiulizi kwanini haya mambo yako hivi kama yalivyo ?
 
Goli 3 mkononi na mahari ilitolewa m 3, ndo maana nimesema hizi ishu ni ngekewa tu
Maana ya mahari ni zawadi anayo zawadiwa binti/mwanamke toka kwa aliyemridhia. Maana yake jukumu hili ni la yule muolewaji, kama mwanamke amekuridhia na anakupenda kweli hawezi kutaja mahari kubwa namna hiyo au mfano wa hayo. Katika utajajwi wa mahari huwa kuna tatizo mara nyingi muhusika hashiriki kwa asilimia zote.

Sasa hukuona ukakasi kumtajia mwenza wako kiwango hicho kikubwa cha mahari ?
 
Unaposema siku ya wanawake ni moja na hizo zingine zote ni za wanaume, hiyo hoja unaona ina mantiki kweli?
Hoja ina maana. Kwanini hukuweka tamko "maana" kwenye tamko "mantiki" ? Au umelitumia kimazoea ? Sababu hujaliweka mahala pake tamko hilo.
Lakini kimsingi sijafikiria au kuwaza haya mambo ni magumu kiasi unataka kuyaweka hapa.
Hapa sijaelewa unakusudia nini ? Au umemaanisha nini ?
Kuna siku kuu kadhaa za kuadhimisha mambo/ matukio mbali mbali duniani, sio lazima kuzitambua au kuziadhimisha lakini kuheshimu na kuwaheshimu wanaozisherehekea ni uungwana.
Naomba unionyeshe usahihi wa haya uliyo yaandika.
Siku ya uhuru ipo na inatambulika kama siku kuu, lakini haulazimishwi kuisherehekea, lakini pia kuwashangaa wanaosherehekea ni tatizo zaidi.
Kadhalika hakuna aliyelazimishwa, ila kuwashangaa lazima tuwashangae sababu kufanya kwao au kusherehekea kwao ni sawa kutofanya na kutosherehekea.

Swali la msingi, huwa unafanya mambo ili mwisho iweje ?
Sasa mwamba ikiwa wewe umeamua kusherehekea hizo siku, na mwingine asipoziadhimisha kuna ubaya?
Kwa yule asiyehusika nazo hakuna ubaya.
 
Hoja ina maana. Kwanini hukuweka tamko "maana" kwenye tamko "mantiki" ? Au umelitumia kimazoea ? Sababu hujaliweka mahala pake tamko hilo.

Hapa sijaelewa unakusudia nini ? Au umemaanisha nini ?

Naomba unionyeshe usahihi wa haya uliyo yaandika.

Kadhalika hakuna aliyelazimishwa, ila kuwashangaa lazima tuwashangae sababu kufanya kwao au kusherehekea kwao ni sawa kutofanya na kutosherehekea.

Swali la msingi, huwa unafanya mambo ili mwisho iweje ?

Kwa yule asiyehusika nazo hakuna ubaya.

You are right Sir!
 
Maana ya mahari ni zawadi anayo zawadiwa binti/mwanamke toka kwa aliyemridhia. Maana yake jukumu hili ni la yule muolewaji, kama mwanamke amekuridhia na anakupenda kweli hawezi kutaja mahari kubwa namna hiyo au mfano wa hayo. Katika utajajwi wa mahari huwa kuna tatizo mara nyingi muhusika hashiriki kwa asilimia zote.

Sasa hukuona ukakasi kumtajia mwenza wako kiwango hicho kikubwa cha mahari ?
Tamaduni hazifanani, kwetu mahari inapangwa na wazazi/walezi upande wa kiumeni, halafu pia kabla hajafika home alishajipanga kutoa m 4-5 kwahiyo hiyo aliyotajiwa ilikuwa ni chini ya matarajio yake

Kutajiwa kiasi hicho inategemeana na msukumo/presha ama uhitaji aliokuwa nao muoaji hata kwa laki 3 angelipa na ningeridhia, ila yeye alipenda hivyo na Mimi nikawaambia walezi kiwango Cha kucheza nacho
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizobaki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Suala la idadi ya wake wa kuoa nadhani li wazi kwamba MKE MMOJA, MUME MMOJA. Zaidi ya hapo ni uzinzi na uasherati tu. Ndio Maana Mungu alipomuumba Adam, hakumuumbia wanawake wanne, alimuumbia Eva (Hawa) kama mke pekee. I bet GOD knew better.
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
Nitamuiga huyo Mzee wakati namuoza mwanangu.
 
Tamaduni hazifanani, kwetu mahari inapangwa na wazazi/walezi upande wa kiumeni, halafu pia kabla hajafika home alishajipanga kutoa m 4-5 kwahiyo hiyo aliyotajiwa ilikuwa ni chini ya matarajio yake

Kutajiwa kiasi hicho inategemeana na msukumo/presha ama uhitaji aliokuwa nao muoaji hata kwa laki 3 angelipa na ningeridhia, ila yeye alipenda hivyo na Mimi nikawaambia walezi kiwango Cha kucheza nacho
Upo sahihi kabisa, mtu anaposema M3 ni kiwango kikubwa lazima aseme ukubwa huo ameufanya kwa ulinganisho upi, kuna baadhi ya watu waliojaliwa ukwasi fedha kama hiyo ni ya kuishia Bar (yaani anaweza kuiingiza kwa siku) wakati sisi wengie huo ni mshahara wa miezi saba.

Kuhusu mila na tamaduni pia upo sawa maana hata Uislamu umebeba mila na tamaduni za kiarabu, Ukristo pia umebeba baadhi ya mila za kizungu. Sasa kwa kuwa dini hizi zimetokea huko ni lazima zibebe mila na tamaduni zao maana walikuwa na mila zao kabla ya dini hizo kuja kwao na hata manabii walioazaliwa huko walilelewa na kukulia katika mila hizo.
 
Shukrani sana kwa kuongezea hapo, Kuna wanaume wako serious sana na haya mambo si swala la ukwasi ni moyo wake tu yeye alitaka kunipa heshima hiyo, na mie nisingevunga kuikataa
 
Suala la idadi ya wake wa kuoa nadhani li wazi kwamba MKE MMOJA, MUME MMOJA. Zaidi ya hapo ni uzinzi na uasherati tu. Ndio Maana Mungu alipomuumba Adam, hakumuumbia wanawake wanne, alimuumbia Eva (Hawa) kama mke pekee. I bet GOD knew better.
Chief! MUNGU hajawahi kuweka ukomo wa idadi ya wanawake wa kuoa, aliliacha suala hilo mikononi mwetu, ndiyo maana baadhi ya mitume waliotangulia walioa wanawake zaidi ya mmoja na hatujawahi kusikia kuwa wameenda motoni. Hizi sheria za mke mmoja na wake wanne ama kutokuoa/kuolewa kabisa (Mapadri na Masista) zimewekwa na binadamu, MUNGU hausiki nazo (maana hajawahi kutunga sheria, bali alitoa AMRI KUMI).

Hata Waislamu sheria ya kuoa wake wanne ilipigiliwa misumari baada ya Mtume Muhamad S.A.W kwenda zake (hakuwahi kuweka ukomo). Uzinzi ni kitendo cha kufanya ngono nje ya ndoa bila kujali umeoa/umeolewa au kapera.
 
Suala la idadi ya wake wa kuoa nadhani li wazi kwamba MKE MMOJA, MUME MMOJA. Zaidi ya hapo ni uzinzi na uasherati tu. Ndio Maana Mungu alipomuumba Adam, hakumuumbia wanawake wanne, alimuumbia Eva (Hawa) kama mke pekee. I bet GOD knew better.
emoji125.png
emoji125.png
emoji125.png
Chief! MUNGU hajawahi kuweka ukomo wa idadi ya wanawake wa kuoa, aliliacha suala hilo mikononi mwetu, ndiyo maana baadhi ya mitume waliotangulia walioa wanawake zaidi ya mmoja na hatujawahi kusikia kuwa wameenda motoni. Hizi sheria za mke mmoja na wake wanne ama kutokuoa/kuolewa kabisa (Mapadri na Masista) zimewekwa na binadamu MUNGU hausiki nazo (maana hajawahi kutunga sheria, bali alitoa AMRI KUMI).

Hata Waislamu sheria ya kuoa wake wanne ilipigiliwa misumari baada ya Mtume Muhamad S.A.W kwenda zake (hakuwahi kuweka ukomo)
Shukrani sana kwa kuongezea hapo, Kuna wanaume wako serious sana na haya mambo si swala la ukwasi ni moyo wake tu yeye alitaka kunipa heshima hiyo, na mie nisingevunga kuikataa

Shukrani sana kwa kuongezea hapo, Kuna wanaume wako serious sana na haya mambo si swala la ukwasi ni moyo wake tu yeye alitaka kunipa heshima hiyo, na mie nisingevunga kuikataa
Hakika Amekuheshimisha!! Nawe pia una deni la kuhakikisha unamtunzia heshima yake kwa kumbebea mimba na kumzalia watoto lakini pia uhakikishe hao akina Baba wa watoto wako wa mwanzo wasije kupasha kiporo (maana baadhi ya wanaume tunapenda mtelezo)
 
Chief! MUNGU hajawahi kuweka ukomo wa idadi ya wanawake wa kuoa, aliliacha suala hilo mikononi mwetu, ndiyo maana baadhi ya mitume waliotangulia walioa wanawake zaidi ya mmoja na hatujawahi kusikia kuwa wameenda motoni. Hizi sheria za mke mmoja na wake wanne ama kutokuoa/kuolewa kabisa (Mapadri na Masista) zimewekwa na binadamu MUNGU hausiki nazo (maana hajawahi kutunga sheria, bali alitoa AMRI KUMI).

Hata Waislamu sheria ya kuoa wake wanne ilipigiliwa misumari baada ya Mtume Muhamad S.A.W kwenda zake (hakuwahi kuweka ukomo)

Hakika Amekuheshimisha!! Nawe pia una deni la kuhakikisha unamtunzia heshima yake kwa kumbebea mimba na kumzalia watoto lakini pia uhakikishe hao akina Baba wa watoto wako wa mwanzo wasije kupasha kiporo (maana baadhi ya wanaume tunapenda mtelezo)
Asante kwa ushauri na tahadhari nzuri, nitazingatia, Sina kawaida ya kula kiporo hivyo kuwa na amani
 
Mnaleta utani,mnawajua wasukuma? Hao ndio wanaongoza kutoa mahari kubwa but na kuzaa aisee wanazaa ni shida
Usukumani hawanaga utani na suala la mahari kabisa,hasa binti akiwa mweupe,mnaweza kuposa wanaume hata 4 mnapadiliana dau mwenye mahali kubwa zaidi ndo anapewa mke
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom