Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Ungemwambia mzee aache upuuzi... hakuna mwanamke wa bure... mwanamke lazima alipiwe mahari hata kama ni simbilisi 1
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
 
Kweli wazazi wameweka kitega uchumi kwa mabinti zao acha wazekee majumbani huku tukiendelea kuwapa mimba wazalie nyumbani
 
Mimi hizo zote ulizo zitaja sisherehekei hata moja. Mimi nina sikukuu tatu tu basi kwa mwaka,nazo ni :

1. Kila siku ya Ijumaa kwangu ni sikukuu
2. Idd al Fitri
3. Idd al Adh'ha (Idd ya kuchinja)

Sasa maswali yako yanatakiwa yatokee katika hizo sikukuu tatu hapo juu.

Tanbihi : Hivi sahihi ni "Sherekea" au "Sherehekea" ?

Sasa mwamba ikiwa wewe umeamua kusherehekea hizo siku, na mwingine asipoziadhimisha kuna ubaya?

Siku ya uhuru ipo na inatambulika kama siku kuu, lakini haulazimishwi kuisherehekea, lakini pia kuwashangaa wanaosherehekea ni tatizo zaidi.

Kuna siku kuu kadhaa za kuadhimisha mambo/ matukio mbali mbali duniani, sio lazima kuzitambua au kuziadhimisha lakini kuheshimu na kuwaheshimu wanaozisherehekea ni uungwana. Ukizingatia haikuathiri au kukupunguzia kitu.

Unaposema siku ya wanawake ni moja na hizo zingine zote ni za wanaume, hiyo hoja unaona ina mantiki kweli?

Lakini kimsingi sijafikiria au kuwaza haya mambo ni magumu kiasi unataka kuyaweka hapa.
 
kuna mikoa hapo kaskazini wanaanzia M eti
Kama mwanamke atataja M sababu anahisi zawadi kubwa kama hiyo nawe unaona anastahiki sawa hakuna tabu..

Shida kubwa kwenye mahari ni wazazi ndio wekuwa watajaji wakubwa, oohh, sijui nimemsomesha, sijui hiki na kile mara hivi, anakurupuka tu kutaja milioni 4.
 
Huwa nafikiria kuoa bila kutoa mahari.

Namchukua, tunaishi kisela, baadae anazalishwa ndo inapita hvyo
 
Kama mwanamke atataja M sababu anahisi zawadi kubwa kama hiyo nawe unaona anastahiki sawa hakuna tabu..

Shida kubwa kwenye mahari ni wazazi ndio wekuwa watajaji wakubwa, oohh, sijui nimemsomesha, sijui hiki na kile mara hivi, anakurupuka tu kutaja milioni 4.
Kazi kweli kweli mkuu
 
Back
Top Bottom