Mzee Wa Kale Kabisa
JF-Expert Member
- Mar 25, 2018
- 2,600
- 4,265
Kama ulikuwa ndio unaanza, ulilima hekari nyingi sana.. Pole mkuuMimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu. Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.