Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Hivi ni kweli kuwa watu wote tunaopenda mabadiliko tulitakiwa tupige magoti mbele ya Lowassa na kumuunga mkono? Watu wote ambao tulikuwa tunaunga mkono upinzani kwamba tulitakiwa alipotangazwa Lowassa na alipoungana na kina Kingune na Sumaye, Masha na wengine sote tulitakiwa - ili kuonesha kuwa tunamaanisha kweli tunataka mabadiliko - basi tuunge mkono. Na kama kupinga basi tulitakiwa tupinge kimoyo moyo tusipinge hadharani?
Kwamba, kwa vile tuliikosoa CCM - na wengine bado tutaendelea kufanya hivyo bila kuangalia nyuso zao - basi tulitakiwa (ili kupata uhalali mbele ya wengine) tumkubali Lowassa , makuwadi wake (natumia neno kuwadi jinsi wao wanavyotumia neno wasaliti kututaja tuliomkataa Lowassa) na tuimbe sifa kwa kuzungurusha mikono "Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko"?
Hivi ina maana sasa hivi wapinzani wa kweli na wenye mawazo ya kweli ya kuleta mabadiliko ni wale waliompokea na kumuuza Lowassa kwa wananchi kiasi kwamba yeyote aliyeenda kinyume cha Lowassa basi amekuwa msaliti wa "mabadiliko yale".
Hivi hawajui kuwa Watanzania walichokataa siyo mabadiliko yaliyoahidiwa bali yaliyoshuhudiwa? Sasa leo wenzetu inaonekana katika kilichoitwa "mahaba" hawajakubali kabisa walifanya makosa na matokeo yake wanafikiria wengine wote tulikosea kumkataa Lowassa na makadokado yake isipokuwa wao? Wanatushangaa kwanini hatukupiga magoti na kutoa sadaka za sifa kwenye madhabahu ya Lowassa.
Well, jibu langu ni rahisi tu. Kila mtu anaishi kwa ukuu wa dhamira yake. Wenzetu mliamini Mabadiliko ni Lowassa na bila ya yeye haiwezekani kuwa na mabadiliko sisi wengine tuliamin mabadiliko yanwezekana hata bila Lowassa.
Sasa kosa letu hapa nini? Kwamba tulitakiwa kama tunampinga Lowassa basi tusijioneshe waziwazi kwa vile tuliipinga CCM ambayo Lowassa alikuwa ni mmoja wa waumini na mtumishi wake wa muda mrefu? Kama wenzetu mmeamua kutetea mabadiliko yale ya Lowassa kiasi kwamba hamtaki au hamko tayari kuona mabadiliko tuliyoyapigania sisi wengine yanawezekana na yanafaa kwa taifa sioni tatizo; ni haki yenu na ninaamini wala haipunguzii uzalendo au utu wenu kama Watanzania. Naamini, mmefanya hivyo mkiwa na nia na moyo safi wa uzalendo -hata kama umepotoshwa!
Na sisi wengine tuna haki hiyo hiyo ambayo wengine mnafikiria kuwa ni himaya yenu; tuna haki ya kuchagua upande ule ambao tunaamini katika dhamira safi unawakilisha mabadiliko tuyakatayo. Katika hili hatuna wa kumwomba radhi au kujipendekeza kwake.
MMM