Tuliomfitinisha Zitto na tuteme mate Chini: Tukumbuke mwisho wa Ubaya aibu!

Status
Not open for further replies.

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,608
2,000
Nadhani kwa wale miongoni mwetu ambao tulikuwa na misheni ya kumfitinisha na kuhakikisha tuna mchonganisha Zitto kwa kuwango kikubwa Kadiri iwezekanavyo, ni dhahiri kwmamba mkakati wetu haujafanikiwa vizuri hivyo ni bora tukauacha na kufanya mambo mengine ya kujenga nchi yetu.

Ni dhahiri kwamba miongoni mwetu tulijaribu kumpaka Zitto matope mwili mzima tukidhani tushamchafua na ataonekana hivyo, lakini tulisahau kwamba tulikuwa tunatumia udongo wa Dar es salaam, udongo wenye asili ya mchanga ambao ukikauka kidogo tu huachia wenyewe na kudondoka chini. na kumuacha muhusika na vijimchanga mchanga tu;Ndicho kilichotokea kwa wale tuliokuwa tukimchafua jamaa wa watu.

Hata hivyo sio lazima kuacha kuendelea kumchafua.Kama mtu ana dhamira ya dhati kutoka moyoni kabisa ya kuendelea kumchafua, anaweza kuendelea kufanya hivyo huku akijua malipo ya ubaya aibu!.Ni nani basi anayeweza kuizuia hulka ambayo mwanadamu kapewa na muumba wake ya "Free will"?

Kwa wale watakaoamua kuendelea kumchafua jamaa wa watu (kwa kuwa tu ! wamedhamiria kweli kweli) nawashauri safari hii wasimpake matope maana mbinu hii inaonekana haija fanikiwa kabisa.Chakufanya wampake maji yaliyooshea samaki wabichi huenda akabaki na shombo: Si unajua shombo la samaki!.

Wale wanaokubaliana na mimi kwamba kazi hii ya kuendelea kumfitinisha Zitto kwa sasa hailipi tena, nawashauri kuunganisha nguvu zetu kuwashawishi viongozi wetu wa kitaifa kujenga ofisi ya kisasa ya chama kwa ajili ya makao makuu.Chama kitatakiwa kutafuta kiwanja halafu kila mpenzi wa chama atatakiwa kufikisha tofali moja na sh 1000 eneo la kiwanja (mapendekezo zaidi yanaweza kutolewa), baada ya miezi miwili, ofisi ya maana kabisa itakuwa imepatikana.
 
mwa 4

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,392
1,250
zitto ni zaidi ya chadema wafanye yote lakini wataipata tu.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,608
2,000
Sasa hizo data wanazosema zinamuhusu zinatoka wapi?
mfano; mimi nasema wewe mwizi na data ninazo.wewe unasema je? wakati fulani za kuambiwa changanya na zako.Hata hivyo option ya kuendelea kumchafua jamaa bado ipo.Ujue duniani kuna machaguo na kila mtu huchagua njia ya kufuata kwa sababu zake na akili zake.Kwa hiyo wanaweza kuendelea vile vile wale wanaodhani inafaa na ni jambo la muhimu kuendelea.Uzuri wake ni kwamba wengi wao wanajua wanachofanya na wanafanya kwa makusudi.
 
Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Kumbe ulimfiti Zitto?

Sababu ya kumfiti ni nini mpaka leo hata mwezi haujapita unaanza kukiri ufitini mkuu?

Nenda Mwandiga kampigie magoti mkuu,

Mlaumuni Zitto kwakutojua siasa za nera,
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,608
2,000
Rubish, Ni kichaa tu ndio atakaeamini kuwa kuna mtu ni maarufu kuliko Taasisi anayoitumikia"!
unaonaje hili la mkakati wa kujenga ofisi ya chama ya kisasa sana! wapenzi wote wa chadema wakiamua kuonesha uzalendo wao na kila mmoja akatoa tofali moja tu na sh 1000, kwa wale walioko dar es salaam tu huku chama kikitafuta kiwanja safi; si tunajenga ofisi kali ya ghorofa tatu? unasema je kwa wazo hili mkuu?
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Nadhani kwa wale miongoni mwetu ambao tulikuwa na misheni ya kumfitinisha na kuhakikisha tuna mchonganisha Zitto kwa kuwango kikubwa Kadiri iwezekanavyo, ni dhahiri kwmamba mkakati wetu haujafanikiwa vizuri hivyo ni bora tukauacha na kufanya mambo mengine ya kujenga nchi yetu.

Ni dhahiri kwamba miongoni mwetu tulijaribu kumpaka Zitto matope mwili mzima tukidhani tushamchafua na ataonekana hivyo, lakini tulisahau kwamba tulikuwa tunatumia udongo wa Dar es salaam, udongo wenye asili ya mchanga ambao ukikauka kidogo tu huachia wenyewe na kudondoka chini. na kumuacha muhusika na vijimchanga mchanga tu;Ndicho kilichotokea kwa wale tuliokuwa tukimchafua jamaa wa watu.

Hata hivyo sio lazima kuacha kuendelea kumchafua.Kama mtu ana dhamira ya dhati kutoka moyoni kabisa ya kuendelea kumchafua, anaweza kuendelea kufanya hivyo huku akijua malipo ya ubaya aibu!.Ni nani basi anayeweza kuizuia hulka ambayo mwanadamu kapewa na muumba wake ya "Free will"?

Kwa wale watakaoamua kuendelea kumchafua jamaa wa watu (kwa kuwa tu ! wamedhamiria kweli kweli) nawashauri safari hii wasimpake matope maana mbinu hii inaonekana haija fanikiwa kabisa.Chakufanya wampake maji yaliyooshea samaki wabichi huenda akabaki na shombo: Si unajua shombo la samaki!.

Wale wanaokubaliana na mimi kwamba kazi hii ya kuendelea kumfitinisha Zitto kwa sasa hailipi tena, nawashauri kuunganisha nguvu zetu kuwashawishi viongozi wetu wa kitaifa kujenga ofisi ya kisasa ya chama kwa ajili ya makao makuu.Chama kitatakiwa kutafuta kiwanja halafu kila mpenzi wa chama atatakiwa kufikisha tofali moja na sh 1000 eneo la kiwanja (mapendekezo zaidi yanaweza kutolewa), baada ya miezi miwili, ofisi ya maana kabisa itakuwa imepatikana.

What a disgrace.....? ? ?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Lilambo

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
2,524
1,250
Mmmh wapeleke tofali wajenge ofisi mambo ya kumchafua Zitto n usee.... Wakitoa tu pesa wameliwa peleka tofali mwanacdm
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,751
2,000
.....Hata hivyo option ya kuendelea kumchafua jamaa bado ipo.......

Hapa panahitaji ufafanuzi. jamaa (nadhani ulimaaninisha Zitto) amechafuliwa vipi, na nani amemchafua, tukio la kuchafua lilitokea lini na wapi...!?
Ukinijibu haya, nitakuwa kwenye nafasi nzuri kutoa mchango wangu murua kwenye uzi huu. Lakini kama kusudio lako ni sichangie waweza kususia kujibu maswali yangu.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom