Tuliokwishafiwa na wapendwa tukutane hapa, na ambao bado tunaomba maoni

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,463
Ebu tuambie umefiwa na nani? Unayachukuliaje maisha bila huyo mpendwa wako binafsi nilimpoteza baba, na sikuwahi kufiwa na mtu yeyote katika familia, baada ya baba nimeanza kuelewa maana ya kufiwa, maana ya kuondokewa na mpendwa.Lakini pia nimeimarika sana (more strong) moyo umekuwa imara zaidi kufiwa kunaweza kusaidia ukafanya mambo magumu ambayo usingeweza kuyafanya awali.

Kwa ambao hawajawahi kufiwa tupeni uzoefu wenu/ maono yenu juu ya waliofiwa wakati ndo nimepata taarifa ya kuondoka kwa mzee, dada mmoja ambaye hakuwahi kuepirince kufiwa alimwambia wife ananiogopa, she see me differently kwakuwa sina mzazi nikanote ni mtazamo wa nitakavyo kuwa labda kwa watu baadaye au!But naona kawaida hadi leo ni mwaka.

That is my new experience
 
Nilipokua na umri wa miaka 14, niliwahi kuota mama amefariki. Nikaanza kupata wasiwasi kuwa yaweza tokea kweli. Nikamfuata mama na kumuuliza, ukiota kitu kibaya unapaswa kufanya nini? Akaniambia unapaswa kusali kukemea ulichoota. Na hicho ndicho nilifanya. Nilisali. Haikupita hata mwezi, mama akafariki kweli. Nilijisikia vibaya. Nikaona katika watu ambao hawapendwi na Mungu mimi wa kwanza. Nimesali lakini hajataka kusikia maombi yangu!!! Ilinichukua muda mrefu kuondoa mawazo hayo ya kuchukiwa na Muumba.
 
Aise mambo mengine unaweza mkosea Mungu maana yanagusa adi kwenye ncha ya moyo , ila naamini Mungu hashindwi na jambo uko sawa sasa
Pole sana ndugu
 
Sio wote waliao msibani kwamba wameguswa na msiba husika, ndani ya mioyo ya wengine upo uchungu uliopitiliza wa kuwapoteza wapendwa wao
 
nameless girl ata mm kila nikiotaga kitu lazima kitokee zilifululiza ndoto za baba yangu nikawa nazikemea na kila cku namuombea maisha marefu lakin haikupita mda sana akafariki had nilimkosea mungu wangu ina maana maisha marefu niliomuombea ndo yale? sa hv mwaka sasa
 
Kila hali ni vile mtu unakubaliana nalo na kukabiliana nalo.

Walezi wangu waliponichukua nikiwa na miaka 10 baada ya kufiwa na wazazi,walidhani ntasumbua sana na kupata shida kuzoea ile hali kwasababu nilikuwa nimeingia maisha mapya. Ndokwanza nilikuwa jasiri hadi huwa namshukuru Mungu hadi leo nimekuwa mtu mzima nilishakubali hali yangu nina furaha na amani maishani mwangu.
 
Hongera mpendwa
 
Nilipokua na umri wa miaka 14, niliwahi kuota mama amefariki. Nikaanza kupata wasiwasi kuwa yaweza tokea kweli. Nikamfuata mama na kumuuliza, ukiota kitu kibaya unapaswa kufanya nini? Akaniambia unapaswa kusali kukemea ulichoota. Na hicho ndicho nilifanya. Nilisali. Haikupita hata mwezi, mama akafariki kweli. Nilijisikia vibaya. Nikaona katika watu ambao hawapendwi na Mungu mimi wa kwanza. Nimesali lakini hajataka kusikia maombi yangu!!! Ilinichukua muda mrefu kuondoa mawazo hayo ya kuchukiwa na Muumba.
God is doing everything for a purpose,kwahiyo sio kuwa Mungu alikuchukia.
 
Yesu amefufuka katika wafu na tunasubiri aje kufufua wazima na wafu

Kifo ndio njia pekee ya kuelekea kwake na kuelekea katika maisha mapya tuliyohaidiwa na mungu baba ambapo watenda dhambi hawatafufuliwa bali ni wale wenye mapenzi mema.

Nb.Kama wewe ni mwenye dhambi basi ukifa nafsi yako ndio basi tena imepotea na haitafufuliwa tena maana Mshahara wa dhambi ni mauti
Kwa hiyo watenda dhambi mtakufa milele??
Hii mpya kwangu.
 
Nilipokua na umri wa miaka 14, niliwahi kuota mama amefariki. Nikaanza kupata wasiwasi kuwa yaweza tokea kweli. Nikamfuata mama na kumuuliza, ukiota kitu kibaya unapaswa kufanya nini? Akaniambia unapaswa kusali kukemea ulichoota. Na hicho ndicho nilifanya. Nilisali. Haikupita hata mwezi, mama akafariki kweli. Nilijisikia vibaya. Nikaona katika watu ambao hawapendwi na Mungu mimi wa kwanza. Nimesali lakini hajataka kusikia maombi yangu!!! Ilinichukua muda mrefu kuondoa mawazo hayo ya kuchukiwa na Muumba.
Pole sana girl,
Natumaini sasa unampenda muumba wako, umeifuta ile dhana ya zamani.
 
Wafiwa huwa wana athirika kwa mambo yafuatayo hasa:

1. Kumkosa mtu waliekuwa wanampenda katika familia - hapa inategemea vipi huyo marehemu alikua akipendwa na familia mfano baba mpole mwenye mapenzi na familia yake atakua tofauti na yule aliekuwa hajali familia.

2. Pengo la kiuchumi / kijamii atakaloacha marehemu -mfano akiwa ndio mtu alie kuwa analeta matumizi au mtu aliekuwa anaangalia familia na nyumba vizuri kama mama wa nyumba

3. Matatizo ya kifamilia yanayofuatia baada ya kifo - familia kusambaratika, ugomvi wa mirathi n.k
 
Haaaswa!!!!
 
Nilipokua na umri wa miaka 14, niliwahi kuota mama amefariki. Nikaanza kupata wasiwasi kuwa yaweza tokea kweli. Nikamfuata mama na kumuuliza, ukiota kitu kibaya unapaswa kufanya nini? Akaniambia unapaswa kusali kukemea ulichoota. Na hicho ndicho nilifanya. Nilisali. Haikupita hata mwezi, mama akafariki kweli. Nilijisikia vibaya. Nikaona katika watu ambao hawapendwi na Mungu mimi wa kwanza. Nimesali lakini hajataka kusikia maombi yangu!!! Ilinichukua muda mrefu kuondoa mawazo hayo ya kuchukiwa na Muumba.

nameless girl ata mm kila nikiotaga kitu lazima kitokee zilifululiza ndoto za baba yangu nikawa nazikemea na kila cku namuombea maisha marefu lakin haikupita mda sana akafariki had nilimkosea mungu wangu ina maana maisha marefu niliomuombea ndo yale? sa hv mwaka sasa

Poleni sana wapendwa. Inasikitisha. Wakati mwingine inategemea tunaombaje au mahusiano yetu na Mungu yakoje. Lakini pia pale inapobidi mapenzi ya Mungu kutimizwa basi hakuna namna.
 
Msiba unaisha kwa jirani tu, siyo kwako. RIP my dear father and my beloved mother. Sitachoka kuwakumbuka na kuwaombea. Mlikuwa ni wazazi wazuri na marafiki wema kwangu.
 
sitosahau 7 feb 2015, ilikuwa 14 feb mzee wangu sijamuona wiki nzima yuko mochwari tu siku hyo ya tarehe 14 naona magar msafara kuna moja lina msalaba et mtu ambaye sijamuona wiki nzma tayar yuko kweny jeneza daa inauma sana , niliangalia lile gar had nikatakadondoka sema kuna mtu alie kuwa akiniangalia hakuwa mbal ,

namshukuru mungu now nimezoea ata nikimkumbuka huwa silii tena kama mwanzo labda nipate shda afu hamna wa kunisaidia afu ukianza waza tena angekuepo angekusaidia yeye
 
Kifo ni asili ya kila kiumbe chenye pumzi kwamba kila nafsi ijiandae kwa safari hii ya ghafla inayokufikia bila kupenda wala kuikwepa.ni jambo jema kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki ingawa sisi hatuwaoni ila roho zao zinatuhisi kila tunachofanya na zinasononeka ikiwa hatuwakumbuki kwa kutilia ubani na kuwatolea sadaka ya chakula kwa maskini.sadaka ndo itamfanya awe na amani huko aliko sababu sadaka haiishi mda wake
 
Back
Top Bottom