Tuliokuamini na kukutetea kwenye janga la Corona umetuangusha. Nimepoteza rafiki na ndugu kwa janga la Corona. Serikali chukueni hatua

Ni dhahiri kuwa kwa sasa Rais John Pombe Magufuli anajionyesha kuwa katika uongozi wake,suala la majanga na uhai wa wananchi wake hayana vipaumbele.Kwake ni pesa na kuona uchumi unakuwa.Rais wetu tofauti na matarajio yetu,amelinganisha uhai na thamani ya pumzi ya watu wake na uchumi wa nchi,kwake Uchumi kwanza uhai baadae.

Huyu sio Rais ambaye kwa sasa unaweza kutoka mbele ya wafiwa na wahanga wa corona na kuwaeleza kuwa ni Rais wa wanyonge, hata mara maja, abadani haitawezekana kwa sasa. Ni kama mkubwa wetu huyu kayaweka maisha ya watu wake rehani na kuutazama kwanza uchumi na pesa.

Kuna malalamiko mengi juu ya ubovu wa huduma za afya katika sehemu walizotengewa wagonjwa wa COVID-19,anatumia mpaka magazeti ya serikali kueneza propaganda kuwa vifaa tiba vimejaa kila mahali, ukweli ni kuwa, huko Mnazi Mmoja, Amana na Mwananyamala wahudumu wa afya ni kweli wanawakimbia wagonjwa sababu na wao wanaokoa maisha yao kwa kukosa PPE.

Watu wanakufa,watu wanaambukizana na kwa kweli wengine wanaangamia kwa sababu ya kauli za Rais na matendo yake.Hali ni mbaya ndugu zangu,tusisikilize propaganda.

Sasa bila shaka kila mtaa umeanza kukumbwa na vifo vya Corona,juma la jana,familia ya rafiki yangu waliuguliwa na mzee wao kwa ugonjwa wa Corona,wakatoka nyumbani kwenda hospitali ya jirani ya Palestina,huko wakawaambia waende Amana,kufika hapo wakaambiwa wanatakiwa kwenda Buguruni kwa Mnyamani ndio kuna kituo kinashughilikia,kufika Buguruni wakaambiwa waende Mloganzila maana ndio watapata haduma.

Safari yote hiyo mgonjwa hana huduma yoyote,walipofika Mloganzila wakaambiwa hawana huduma yoyote,katikati ya bumbuwazi mgonjwa akafariki bila matibabu,na baadae serikali kuuchukua mwili na kuuzika kwa madai kuwa wamechukua sampuli za maiti na kuona maambukizi,familia nzima sasa ipo karantini.

Ummy Mwalimu na Serikali,iseme sasa,na iseme tena,kwanini kila mahali wagonjwa wanakataliwa??Wagonjwa wetu tupeleke wapi?

Habari mbaya kwangu,na ngumu sana,ni kumpoteza rafiki yangu wa muda mrefu,mwanafunzi wangu na comrade wangu mcheshi,huyu alikuwa rubani wa ndege za TANAPA ambaye amepoteza maisha kwa janga la corona na hayupo hata katika kundi la watu waliotangazwa kuwa wamekufa na ugonjwa huu.Huyu ameondoka na watu kadhaa nyuma yake ambao walimbukizana.Na hao watu wameambukiza wengine...Hali ni mbaya na bado serikali inashindwa kutoa sauti ya kimamlaka kuonyesha kuwa hali ni mbaya.

Marehemu huyu(nahifadhi jina lake) siku kadhaa nyuma tuliwasiliana akienda kuhuisha mambo yake ya leseni za urubani na vibali kadhaa pale mamlaka ya Usafiri wa Anga,na baadae kuwa na training nje ya jiji la Dsm wakiwa na mwenzake na watumishi kadhaa wa mamlaka,maanake alikutana na watumishi hapo mahali,hao watumishi wana familia zao,na hao sehemu ya familia wana jamaa zao wengine makazini na mitaani.

Naambiwa sehemu ya ofisi za Mamlaka hizo watumishi wapo karantini sababu waligusana au kuchangamana na marehemu rafiki mpendwa na mwenzake.

Kwa hali hii,bado serikali imejaa vitisho,haizuii misongamano,haiuzuiii mjii wa Dsm kusongamana katika bars,kumbi za starehe na mikusanyiko mingi.Mji upo wazi kusambaza magonjwa mikoani kwa jina la "Kukuza Uchumi".Huu ni unyama gani?Tunawaza pesa juu ya uhai?

Mgonjwa mmoja wapo kule Rukwa,alitokea Dsm kwa njia ya ndege ya ATCL,akapanda ndege mpaka Mpanda na akasogea mpaka Sumbawanga,hapo kaacha ugonjwa kuanzia kwenye ndege,Mpanda hadi Sumbawanga,maanake alichangamana na abiria wengine,alioambukiza ndio wenye dalili na walio hoi,maanake tamaa za uchumi na pesa,zinafanya tunarusha ndege toka Dsm kwenda Mpanda ili ipeleke ugonjwa ukasambae vijijini kwa masikini na wanyonge.Hao Emirates na wengine walifunga safari sio kwamba hawajui pesa,wanajali uhai wa watu wao.

Hizi ni dalili mbaya za kiuongozi,huu ni uuwaji usiokuwa wa moja kwa moja au ni tuseme wa moja kwa moja.Ni ukosefu wa utu na upendo kwa watu ulioapa kuwalinda ukiwa na katiba kuume na kitabu cha dini kushoto.Wewe baba badilika,okoa watu wako...hiyo ndio kazi tuliokupa kwa njia ya kura.

Sasa ni kama hata data zinapikwa,watu wengi wanakufa,tumeanza kupoteza hata wahudumu wa afya ambao ni askari wetu wa mstari wa mbele...Watumishi wa afya wameanza kufa kwa maambukizi ya kukosa PPE!

Serikali ipo,inaaminisha tutapona kwa mvuke,ni labda kweli,lakini kwanza ilipaswa tuwaambie watu wetu kuwa hali ni mbaya,kukiri kuzidiwa na ugonjwa huu sio udhaifu wa kiuongozi bali ni uimara wa kiuongozi,hii ni kwasababu unawapa watu wako taarifa iliyo kamili na bora.

Sasa barakoa zilizothibitishwa na mamlaka za viwango zinakosa wateja,sababu Rais kaongea hadharani kuwa haziaminiki sababu zinaweza kuwa na virusi.Kazi hii sasa imeachiwa kwa machinga na mafundi cherehani,ambao sasa wanachonga barakoa zisizo thibitishwa ubora wake na mamlaka yoyote.

Si mbaya kuwa na barakoa ya kitambaa,lkn ni hakika kuwa wataalamu wanaeleza kuwa haizuii virusi kwa kiwango hicho zaidi ya kuzuia vumbi tu,lkn haya yote ni sababu ya kauli ya Rais ambayo ina mamlaka ndani yake.

Katika masoko,makanisani na misikitini bado watu wanajazana...Hali ni mbaya,na kwa sababu kwa siku kadhaa serikali imeanza kutaja tu wanaopona kwa idadi kubwa,hatutaji tena vifo,tukidhani kifo ni aubu,kumbe kwa mantiki ya ugonjwa huu wanaopona hata wakiwa 1000,lazima tulie na aliyekufa mmoja,sababu uhai na utu wa mtu una thamani isiyofananishika.Kila mahali sasa watu wamelegeza kufuata kanuni za afya na kujikinga wakiona kuwa wataugua na kupona.

Kuusema ukweli juu ya ugonjwa huu si kuleta hofu,ni kuelezea ukweli na uhalisia wa madhara ya gonjwa hili.Kuficha data sio sifa za uongozi bora,bali ni sifa za uongozi mbovu unaouwa watu wake kwa kufanya "Massaging of data"

Toka mafichoni Rais,wewe ni Amiri Jeshi mkuu,kaa mstari wa mbele...Umekuwa ukivaa magwanda kuonyesha u mwanajeshi,sasa onyesha kwa vitendo...Njoo mbele baba njoo,wasisitize watu wako kuwa hali ni mbaya.

Mikoa iliyoathirika kama Dsm,si lazima uifunge,ruhusu magari ya mizigo na chakula kuingiza na kutoa bidhaa kupeleka mikoani.Hii itasaidia kupunguza maambukizi.

Huwezi kuelewa bandiko hili,mpaka sehemu ya ndugu au jamaa yako afe kwa ugonjwa huu katika mazingira ambayo kuna uzembe mkubwa kutoka kwa watu tuliowapa dhamana...Hii ni ujinga,ni ajabu sana kwanini watu wanashindwa thamini maisha ya watu na wanaona pesa ni bora zaidi.

Zile tambo zote na mikakati mliyotutambia kuwa hii ni serikali mpya,mbana zimefifia??Okoa maisha ya watu wako,pesa makaratasi.
Mkuu Barafu pole sana. Umeandika kwa uwazi na hisia pia hukupunja.
Naungana na kauli na ushauri wako.
 
Serikali ilishapoteza mweleeo kuhusu janga la corona, ndio maana hata taarifa zake kwa sasa ni za kupika na za kuvizia! hali ni mbaya mbaya. Hili lilikuwa wazi tangu mwanzo kutokana na kauli za mkuu7 kuhusu ugonjwa huu na namna walivyotoa upotoshaji kwa wananchi hasa rc wa dsm kama kawaida yake!
 
twende taratibu.maana wabongo kwa maneno hamjambo.

funga dsm,funga mwanza,funga arusha.upate watu milioni 15,toa watu milioni 3 wanaojiweza,wabaki milioni 12 wanaohitaji msaada.

bila kusahau factor no moja,kwamba uzalisha hamna baada shughuli za uzalishaji kufungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa Dar mwanza arusha na zanzibar hawafiki m 15. Dar ina watu ml. 6. Mwanza wapo 2. Arusha tuseme hawazid 2 na zanzibar 1.2. Hawa ni watu ml 11.2. Sasa hapa tusema matajir wapo ml 2.5 na mido class ni ml.3.5 hawa ni wafanyakaz nk. Sasa kuna wale kaz na kula cku hiyo hiyo hawazid ml 4. Hawa wengi watakuwa vijijin na kwenye maslum mijin. Unapiga hesabu ya mwez. Wanapewa chakula sio chakushiba ni cha dharura kwa cku 30. Nakumbuka nikiwa mdogo kulitokea kipindupindu huko moshi. Waliweka lockdown mzee. Hakuna kijiji hiki kuvuka kijiji kingine. Mahitaj yote baloz alikuwa anaandikiwa anapeleka kwa duka la kijiji tunagawiwa mahtaji ya lazima. Na masikin hawana gharama kubwa kiivyo. Sasa hatar ya kutokufanya hivyo ni kutokujua hii hali itaenda mpaka lin na inazid kubust. Yaan ni sawa na kuacha kumsomesha mtoto kwa kusingizia ada ni kubwa. Mzee gharama ya huo ujinga utakaotokea huko mbelen ni kubwa kuliko ungejifunga tu na kumsomesha.
 
Duh...Mkuu Kitali, kama ni kunidharau kwa ku zero in nidharau tuu, ila pia asante kwa nondo kali za kushiba kwenye bandiko lako.

Corona ina kinga kwa kuizuia isikuingie ila ikikuingia haina dawa!. Pona yako ni uwezo wa kinga yako ya mwili kuproduce antigens to fight the virus, lakini kama una issues za PB, Kisukari, Aids, Heart Disease, Pneumonia, TB, au uko kwenye ugonjwa mwingiine wowote ambao uko under heavy medication kiasi cha kumaliza uwezo wa mwili wako kutengeneza antigens, hata watu wajifunge vipi kukutibia, hata ufungiwe the latest ventilators, lazima uchomoke!.
P
Bro hii nchi kuendana na mastress ya maisha ni vigum sana kwenye watu wenye umri wa miaka 40 kwenda juu wakiwa 30 ukakosa hapo 15 ambae hana ugonjwa kabisa mwilin mwake. Tunashida sana na tukipata tunazitumia vibaya mpaka tunajenga ugonjwa. Mi nimezaliwa maisha ya chini kabisa na nimefanya karibu shughuli zote ngum so nimeitembea karibu nchi hii yote mijin na vijijin. Aisee watu wana shida na nyingi ni za kusababishiwa tu. Unakuta mtu kawekwa mahali hatimiz wajibu wake mpaka apigiwe kelele wee ndio anachukua hatua. By the time anakuja kuchukua hatua ashaacha athar zitakazoichukua jamii miaka 10 mpaka 30 kuzisolve. Hebu fikiria kwa kuficha tu taarifa sahihi tunaenda kuwekwa kwenye blacklist huko nje ukisafir coz hatuaminik tena. Watalii itawachukua muda kuja tena maana hawapat kile kilicho sahihi on time. Kuna jamaa nimemueleza hapo chin kuwa wakat tukiwa wadogo kuliibuka kipindupindu kijijin. Nakumbuka tulipigwa block down ila ckumbuki kama ilikuwa ni nchi nzima au la ila ninachokumbuka ukiwa na mahtaj mtu mmoja kila familia anaenda kuyaandika kwa baloz nae anapeleka kwa duka la kijiji so tulikuwa tunapata mgao wa yale ya lazima sio shibe. Huruhusiw kwenda kijiji kingine au kutoka kwenu. Kulikuwepo mogambo by that time.
 
Mkuu sasa imeanza bungeni na kwenye Cabinet,labda tutaelewana kidogo
Kuna wakati Mungu huwatetea watu wake kwa namna ya ajabu, Nebkadneza alikuwa hodari, jasiri na KATILI, hakusikiliza mtu.

Lakini ulifika ukamilifu/peak ya kiburi, alijikuta akila NYASI kondeni.
Ndipo alipokiri kuwa yupo Mungu wa Israel anayetawala.
Alirudi enzini mwake akiwa MNYENYEKEVU.

Tanzania tunapitia wakati mgumu mno, haturuhusiwi kushauri, kukemea wala kukosoa ISIPOKUWA kusifu na kuabudu.
Jambo hili siyo jema hata kidogo.

Kuna wakati Mungu alitaka kufuta waisrael ambakishe Musa na uzao wake, lakini Musa alimkosoa Mungu kwa kusema.
SOMA HAPA

( 10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Kutoka 32:10

11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
Kutoka 32:11

12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
Kutoka 32:12)

HUU NI USHAURI MUNGU ALIPEWA NA MUSA

"Ukiwaangamiza watu hawa, mataifa watakucheka kuwa kwanini uliwatoa Misri uje kuwaangamiza jangwani?"

Ushauri wa Musa ulibadili hasira ya Mungu.

Hapa Tanzania hashauriwi mtu, hapokei ushauri, anasema yeye ni Jiwe kweli kweli. Hii sio sawa, watu hatupewi kila kitu bali huwa tunakamilishana kwa kushauriana..huwezi kujua kila kitu hivyo kushauriwa ni muhumu.

NALENGA KUSEMA NINI?
Kila kitu hutokea kwa sababu maalum, hatujui kwanini kuna mtu anashupaza shingo zaidi ya Farao!!!!
Huenda Corona imebeba WOKOVU wa Mtanzania.
Kivipi?
Namna gani?
Itakuaje?
Sina majibu muda utaongea...ninaomba uzima na ninawaombea na wana jf wote tushuhudie mwisho wa sakata hili.
Mungu atusaidie Watanzania tumetingwa kweli kweli.....kwako mzee barafu
@slary slip
johnthebaptist
@wakudadavua
faiza foxy
cariha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati Mungu huwatetea watu wake kwa namna ya ajabu, Nebkadneza alikuwa hodari, jasiri na KATILI, hakusikiliza mtu.

Lakini ulifika ukamilifu/peak ya kiburi, alijikuta akila NYASI kondeni.
Ndipo alipokiri kuwa yupo Mungu wa Israel anayetawala.
Alirudi enzini mwake akiwa MNYENYEKEVU.

Tanzania tunapitia wakati mgumu mno, haturuhusiwi kushauri, kukemea wala kukosoa ISIPOKUWA kusifu na kuabudu.
Japo hili siyo jema hata kidogo.

Kuna wakati Mungu alitaka kufuta waisrael ambakishe Musa na uzao wake, lakini Musa alimkosoa Mungu kwa kusema.

"Ukiwaangamiza watu hawa, mataifa watakucheka kuwa kwanini uliwatoa Misri uje kuwaangamiza jangwani?"

Ushauri wa Musa ulibadili hasira ya Mungu.

Hapa Tanzania hashauriwi mtu, hapokei ushauri, anasema yeye ni Jiwe kweli kweli. Hii sio sawa, watu hatupewi kila kitu bali huwa tunakamilishana kwa kushauriana..huwezi kujua kila kitu hivyo kushauriwa ni muhumu.

NALENGA KUSEMA NINI?
Kila kitu hutokea kwa sababu maalum, hatujui kwanini kuna mtu anashupaza shingo zaidi ya Farao!!!!
Huenda Corona imebeba WOKOVU wa Mtanzania.
Kivipi?
Namna gani?
Itakuaje?
Sina majibu muda utaongea...ninaomba uzima na ninawaombea na wana jf wote tushuhudie mwisho wa sakata hili.
Mungu atusaidie Watanzania tumetingwa kweli kweli.....kwako mzee barafu



Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu,nimeupenda sana mtazamo wako.Umeandika vizuri sana na umejenga hoja kwa umahiri sana.Asante kwa mchango wako na kwa kuniongezea maarifa ya namna wafalme wenye kiburi waliathibiwa
 
Mkuu Barafu, kwanza pole sana kwa kufiwa na rafiki rubani wa Tanapa. Pia kwa incident ya kifo cha Mzee wa jirani aliyekosa huduma hadi kupoteza maisha na familia yake kuingizwa karantini.

Tangu kuingia kwa janga la Corona, elimu ya kinga imeenezwa sana, ila kwa upande wa msimamo na kauli za rais wetu, kuna watu hawajamwelewa ukiwemo wewe.

Watanzania tuko wa aina tatu
1. Kundi la kipato cha juu na watumishi wa umma, matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili ndilo kundi pekee ambalo wanaweza kuishi kwenye lockdown. Hawa wako wachache nchi ikiamua kufanya lockdown, wataendelea kulipwa even by doing nothing, na wataninua mahitaji yao yote na kujifungia ndani. Hawa ni watu wenye magari yao na wanaweza kununua mahitaji yote supermarkets. Kwenye kundi hili, they've made money and now, they use money work for them.
Yaani wanapesa ambapo wanaweza kukaa na kuitumia pesa kuwafanyia kazi. Kati ya watu milioni 50 ya Watanzania, kundi hili lina watu 10% ambao ni watu milioni 5.

2. Kundi la pili ni watu wa kipato cha kati, the working class, hawa ni wafanyakazi waajiriwa, wazalishaji mali na wafabiashara wa kati. Hawa wanafanya kazi, wanatoka jasho ndipo wapate pesa. Ikitokea lockdown hawa uzalishaji utasimama, biashara zitasimama, uchumi utatikisika na the working class watapoteza kazi, hivyo hawawezi ku survive kwenye lockdown. Hawa they work for money to live, yaani wanafanya kazi na kuvuja jasho kutafuta pesa ili waitumie hiyo pesa kuishi na kuendesha maisha yao. Ikitokea lockdown hawawezi kufanya kazi na hawawezi kupata pesa hivyo hawawezi kuishi. Kundi hili lina 20% ya Watanzania ambao ni watu milioni 10.

3. Kundi la mwisho ni kundi la watu wenye kipato cha chini, hawa they live hand to mouth, kundi hili ni kundi la wakulima, wafugaji, wavuvi na wafabiashara wadogo ambao ili waishi lazima wawahudumie, makundi yale mawili, kukitokea lockdown, kundi hili ndio most hit, watakufa njaa inabidi wagawiwe chakula, kundi hili lina 70% ya watu milioni 50, ambao ni watu milioni 35. Hawa they don't make any money, they only struggle to survive.

Uamuzi wa rais Magufuli wa no lockdown una lengo la kuzuia kuporomoka kwa uchumi wetu sio ili to make money but kuzuia watu wetu wasife njaa, kama ni kufa kwa kakolona heri wachache wafe kwa Corona, kuliko kufanya lockdown na kuua wengi kwa njaa.

P
Uganda kuna ripoti yoyote ya mtu aliyekufa njaa nakuamini mkuu ila hoja yako haina mashiko


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa upande wa urais kwa uchaguzi wa 2020, due to the political landscape ya the political playground ya siasa za Tanzania, Magufuli hana mpinzani wala mshindani, kwenye urais, Magufuli is the one and only, na the overall is CCM as usual.

Hapa Paschal Mayala umeongea kwa herufi kubwa kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia tena kwako na kwa wenzako, Magufuli ni rais wetu na hilo halina mjadala, ila Magufuli sio mtu sahihi kwa nafasi ya urais. Nafasi ya mwisho iliyomstahili ni uwaziri mkuu. Ni kweli ni mchapakazi, lakini hana sifa ya kuwa rais.

Kama ulikuwepo!!Umejuaje haroo?
Marhemu Kingunge alisema kuwa MAGUFULI HAKUTAKIWA AINGIE IKULU BAALI ANGEENDELEA KUWA MNYAPARA WA MABARABARA TU..!
Hili limethibotika kwa Ukweli na Uwazi.
 
Back
Top Bottom