Tulioko kwenye ndoa kukaribisha mashosti nyumbani wamzoee Mr ni kutengeneza bomu

Hilo litategemeana na tabia ya mume.
Mimi ninawajua marafiki wa mke wangu wengi sana, wanaweza kunipigia simu wakati hata wife hana taarifa lakini sijawahi kutongoza hata mmoja wao wala sina mpango huo.

Nikiamua kuchepuka nachepuka eneo la mbali sana ambalo hata mke wangu hajulikani wala hawezi kuonana na mbaya wake kirahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi nikisikia tu hodi, namwambia hubby aingie chumbani. Utakaa hadi ukome
Hahah!, kwa kweli..




Halafu siku hiyo I'll opt my glasses for contact Ls. Ili nikonyeze vizuri..:D

Lakini haya mambo bwana. Kwa kweli inategemea na mume na aina ya marafiki mtu alie nao. Kama wote ama mmoja wa hawa macho juu, basi someone should hope for the Best. Cos utamchunga na wangapi?!

But all in all dear..
We better stick with our "Unwritten-Rule"
Don't date with your shosti's Ex/current squeeze.
 
In short angalia na aina ya rafiki yako, sio kisa mume ni mstaarabu basi unamletea marafiki ambao wanaweza kuleta ushawishi hata kwa malaika.

Mke wangu ana marafiki zake ambao huwa wanakuja kumtembelea na sioni kama nitatizo hata kama wataongea nikiwepo au nisipokuwepo ila kuna siku alikuja rafiki yake mmoja hivi ni nesi katika Hospital fulani Dar es Salaam.

Japo ni mtulivu na anaonekana ni mtu wa dini sana lakini Shape yake na aina ya muonekano wake hakuna mwanaume ambaye anaweza kumuona asimtamani.

Alivaa kiheshima sana lakini alivyoumbika sina namna ya kuelezea nikaeleweka vizuri. Nilisalimiana naye kwa kupeana mikono kisha wife akanitambulisha, tukaongea kidogo then nikawaacha nikaondoka zangu.

Niliporudi nilimkuta na alilala nyumbani, siku ya pili aliondoka kurudi na tukawa tunasalimiana bila shida lakini wife hakusita kunitahadharisha kwa kuniambia "Yule ni rafiki yangu" Amejaaliwa shape na kila kitu naomba usije ukamtongoza, akaendelea kuniambia....... Nilisoma naye na tulikua kama ndugu. Tangu shuleni alikua na maumbile hayo hayo na siku zote alikua anataka kuja kunitembelea nikawa nashindwa kumleta kwakua najua anaweza kuja kunitaifisha mume kama mume atakosa moyo wa utulivu.

Wiki yote amekua akiomba aje kunitembelea jana ndio akaja hivyo nikawa sina jinsi. Japo nilikosa kujiamini kabisa kutokana na alivyo japo hana tabia za kihuni.

Hayo ndio yalikua maelezo ya wife, sasa wewe unasema rafiki yako kuja sebuleni sio shida ila kumbuka na muonekano wake unachangia. Akiwa mzuri sana unajihatarishia ndoa yako mwenyewe, wanaume hatujaumbwa na mioyo kama malaika na vichwa vyetu vinaendeshwa na hisia kama kitaonekana kitu cha kusisimua hisia. Tamaa humpata kila mtu kwa mazingira tofauti, tuleteeni marafiki lakini kabla ya kumleta rafiki hakikisha mwanaume wako asije akapata tabu ya kumfikiria rafiki yako kwa muonekano wake tena ukigundua hata wewe unahisi rafiki yako ni mzuri kupita kiasi usimlete nyumbani.

Tunavumilia lakini kuna muda tunashindwa. Kuweni makini mapenzi hayana komandoo

Mkorintho wa 6
Marafiki wapo na nilazima uangalie ni rafiki gani kuna mwingine ni rafiki mkiwa hamjaolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom