Tuliojaza Green Card Lottery mitaa ya Mlimani City surveys majibu vipi?

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,007
5,446
Poleni kwa misiba Watanzania,

Naanzisha uzi huu kama rambi rambi kwa mwanachama mwenzetu aliyefariki hivi karibuni mzee wa bomayeee, case closed, free education n.k, kifupi tutammiss kwa zile mbwembwe zake katika social networks.

Hoja yangu ni hii, nataka tufahamiane iwapo yupo yeyote aliyechezewa Green Card Lottery na yule jamaa pale Mlimani City nyuma ya lile ghorofa pale pembeni jina nimesahau.

Maana mimi jamaa alinigonga zaid ya 20 kunichezea ile lottery, chaajabu siku ananijazisha nakishangaa vitu vilivyojazwa vilikua very simple hata mi fomu yenyewe ka ilikuwa na sehemu nyingi ziliachwa wazi. nikasema mhhh mi ngosha bana kutoka nangende najua nini? Nikakausha baada ya kugongwa nikasema ngoja tuone.

Wallah juzi nacheki majibu yangu heeeh naambiwa "Fomu haikukamilika," nimeumia sana, sasa nikajiuliza ndio mana nilikuwa na wasi wasi au ndio namna wanavyojibu kwa walikosa nafasi?

Sasa wenzangu na mimi vipi mmekutana na majibu gani na je, nanyi mlijaziwajwe? Kuna aliyepokea ujumbe wa kubahatika kupata hio Green Card au tumepigwa?
 
Shida moja ya Wadanganyika sijui ni elimu, uvivu au kutokujua kwa kawaida tu....kwa mfano utakuta mtu hatak kujaza labda fomu za online....maybe latra,tra au issue yoyote inayohusisha mtandao and then unakuta pemben apo ya ofisi kuna like staionery au wajanja wamefungua kaofisi wanakujazia and then wanakucharge sio chini ya elfu 15 na zaidi.
Nway inshort kujaziwa ni uzembe wako cause ungeweza jaza mwenyewe maana hyo kitu haichukui ata dkk 5 kumaliza.Jamaa yeye aliona fursa kwa ujinga wa wengi na akaitumia....by the way sina hakika km mchizi analipa kodi maana anaingiza pesa nyng sana kwenye hyo issue.
 
Hahahahahah! Huyo EBM anawakanda hadi wa kenya na likipara lake lile, kaoa lizungu libibi hivi nadhani ndio project yake kubwa!

YouTube subscribers na viewers wake ni kutoka Bongo na Kenya na ndio aliowashika. Kuna kongamano nadhani alilifanya Ubungo plaza alijaza nyomi matata sana mamtu yenye kipara bana
 
Form tu mnajaziwa afu mnataka mje nchi ya maziwa na asali. Hakuna kinyonye kitachoingia nchi hii, kwa ujinga na uvivu huo bakini huko huko muendelee kula vumbi na kulipa tozo.
Mbaya zaidi waliojaziwa na bwana kipara wengi wao wamekutana na "Fomu yako hayajakamilika" 🤣🤣
 
Mbaya zaidi waliojaziwa na bwana kipara wengi wao wamekutana na "Fomu yako hayajakamilika" 🤣🤣

Dah kawapiga na kitu kizito kichwani huku kachukua buku20 20 zao, Bora wangekuta not selected 🤣🤣
IMG-20230504-WA0011.jpg
 
Shida moja ya Wadanganyika sijui ni elimu, uvivu au kutokujua kwa kawaida tu....kwa mfano utakuta mtu hatak kujaza labda fomu za online....maybe latra,tra au issue yoyote inayohusisha mtandao and then unakuta pemben apo ya ofisi kuna like staionery au wajanja wamefungua kaofisi wanakujazia and then wanakucharge sio chini ya elfu 15 na zaidi.
Nway inshort kujaziwa ni uzembe wako cause ungeweza jaza mwenyewe maana hyo kitu haichukui ata dkk 5 kumaliza.Jamaa yeye aliona fursa kwa ujinga wa wengi na akaitumia....by the way sina hakika km mchizi analipa kodi maana anaingiza pesa nyng sana kwenye hyo issue.
Kweli mzee najilaumi kinyama uvivu huu daah
 
Form tu mnajaziwa afu mnataka mje nchi ya maziwa na asali. Hakuna kinyonye kitachoingia nchi hii, kwa ujinga na uvivu huo bakini huko huko muendelee kula vumbi na kulipa tozo.
We jamaa unaroho ya kichawi saana
 
Kwenye kujaziwa sio tatizo tutambue kuwa ile ni bahati nasibu aidha upate au laah mlikuwa wengi umakini kidogo lazima ukosekane, next time mliojaziwa mjijazie wenyewe lakini pia mtambue ile picha yako lazima iwe na specific kb iweze kuwa uploaded. msijali next time mambo yatakuwa fresh.
Kujaziwa kupo incase huna uelewa wa hilo linalofanyika au unakuwa ujiamini vya kutosha,
mfano; hata pasipoti watu wanajaziwa kisha wanalipa 10k

Mr. Ernest hana baya alikuwa anatoa watu tongo tongo la uvivu
 
Back
Top Bottom