Tulioharibu ndoa zetu baada ya wenzi wetu kuhamishiwa Dodoma, tukutane hapa

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,483
5,813
Kuharibika kwa ndoa sio Jambo la kufurahia ama kupendeza. Ndoa ni msingi na mlango mkuu wa kupitishia baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Shetani kamwe hataki Wala kukubali kuona tunabarikiwa. Hivyo kwa udi na uvumba atazisakama ndoa zetu usiku na mchana.
Kuharibika kwa ndoa ni mpango wa shetani.
Dhumuni la uzi huu ni uzoefu ili tuweze kurudisha mahusiano yetu kwenye mstari.

Binafsi, wife alihamishiwa Dodoma, mi nikabaki DSM nikiendeleza biashara zetu.
Niliweza kutunza heshima yake kwa muda wote aliokuwa huko Dodoma.

Kuna siku moja mvua ilikuwa ikinyesha, mwezi November mwaka jana. Kuna Dada akaniomba lift, nikambeba na kwenda naye Posta.

Dada yule alikuwa ni mkimya Sana, hivyo ili tusitembee kama majini nikawa nikimpigisha stori na utani wa hapa na pale.

Nilikuwa nikielekea Samora TRA kufanya marekebisho kwenye kadi yangu ya gari. Naye alikuwa anaenda Extelecom House, nikatafuta parking, akashuka, tukaagana.

Siku iliyofuata ilikuwa ni jumamosi, nilikuwa na mwaliko wa kuhudhuria harusi ya classmates wangu wa chuo.

Nilipofika ukumbini nilipokelewa vizuri na wale wa Dada wahudumu, wakanielekeza meza ya kukaa.

Moja kwa moja nikaenda kwenye ile meza niliyoelekezwa na wahudumu. Ile nimefika tu nikakutana na Yule Dada wa Jana niliyempa lift.

Nikamuuliza kama kaja na mwenzake, akasema yupo single, basi tukaendelea na story. Alikuwa anakunywa red wine🍷 na Mimi nikawa nakunya Sminorf, waliniwekea chupa nzima mezani, nikawa naipunguza taratibu.

Maongezi na yule alinoga Sana, tulikuwa Kama Ni watu tunaojuana miaka mingi nyuma.

Aliniomba aonje kidogo kinywaji changu, nikampa, akawa anachanganya na wine.
Mpaka harusi inaisha tukawa maji kwelikweli, tukapanda gari na kuanza kuelekea nyumbani.

Kwakweli siku hiyo nilizidiwa Sana na pombe kiasi kwamba nilipoteza kabisa kumbukumbu, licha ya kwamba nilifika home na kupaki gari vizuri na kufunga milango yote.

Network ilikokatikia sikumbuki, nilishtuka ni asubuhi niko kitandani na Yule mrembo.
Sikumbuki Kama tulifanya Wala sikumbuki chochote, nikalianzisha upyaaaa.

Jumapili nzima ilikuwa ni mikasi na show za kibabe. Usiku akalala tena.

Basi mazoea na yule Dada yakawa makubwa. Nyumba aliyokuwa akiishi haikuwa mbali Sana na nyumbani.

Nikazama penzini na mapenzi yakanimeza.
Nikawa nalala kwake hadi nikahamia kabisa kwake.

Kuna siku nikiwa nimelala huko, kumbe wife kaja nyumbani bila kunijulisha. Usiku mzima sikurudi, wala kesho yake sikurudi, akanifuata ofisini.

Akanieleza kuwa ana siku mbili nyumbani sijaonekana hivyo basi nimueleze nilikokuwa.

Tangu hapo mahusiano yakaanza kuyumba, nashindwa kujigawa. Kwa kweli niliharibu, wife akafanya ufukunyuku wake. Wakina Soudy Brown wakampa story kuwa mtaa wa nyuma kuna kidosho kimekamata ufahamu wangu.

Mengi yametokea lakini chanzo ni uhamisho wa Dodoma. Naamini wengi wamekutwa na dhahma tofauti tofauti kwa namna nyingine.

Tushirikiane kuyajenga
 
kuna jamaa nlikuwa kwenye seminar wiki ilopita maeneo ya double tree nae akawa anatoa stori za dizain hii, kwakweli ni changamoto aisee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom