Kuna sababu nyingi sana zinazowafanya watu (Watanzania) kwenda nje na kurudi nchini, moja ya sababu ya kwenda huko ni masomo unakuwa na student visa ikiisha au masomo yakiisha unalazimika kurudi nyumbani, sababu nyingine ni temporary work permit muda au kazi ikiisha unarudi nyumbani.
Sababu nyingine inayowafanya wengi kwenda nje ni kutafuta maisha, wengi huwa ni wazamiaji, wanaweza kuwa na passport halali ila wakifika huko wanazificha au kuzipoteza makusudi, wazamiaji wengine huenda kule wakiwa hawana karatasi (documents) zozote.
Kuna wanaokwenda kama wakimbizi halali na wakimbizi magumashi, kuna wanaokwenda majuu kwa kukimbia kesi mbaya zinazowakabiri kama mauaji ujambazi au madawa ya kulevya, kuna wanaokwenda huko kwa kukwepa majukumu ya kifamilia, kuna wanaokenda kwa ajili ya kuoa au kuolewa ili kupata passport au permanent residence.
Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazowafanya watu waende nje au majuu kwa lugha ya mitaani, kama nilivyosema kuna sababu nyingi kila mtu anaenda na kurudi kwa sababu zake.
Sasa tuangalie uzoefu, kwa tuliofanikiwa kufika huko na kurudi nyumbani na wengine kubaki huko, nini kilikufanya urudi kwanini usiishi hukohuko na kuendeleza maisha ughaibuni kama walivyo wengine, na waliobaki huko nini kimewafanya msirudi, na je kama ulirudi, ulikuwa deported au uliamua mwenyewe kurudi.
Mimi binafsi, nilifanikiwa kwenda UK na niliishi huko kwa takribani miaka mitano. Nilienda kwa student visa, baada ya masomo nilianza kazi za kubeba 'box' ambazo ndizo rahisi kupata. Nilibahatika kutengeneza pesa kiasi chake hadi nikajenga kibanda nyumbani TZ. Wenzangu ambao hadi leo wapo huko walinishauri 'nijilipue' waliofika huko wanajua maana yake. Lakini nilishindwa kutokana na majukumu niliyoacha nyumbani na culture ya huko ya ubaguzi, mwafrika hasa ngozi nyeusi huonekana kama kinyesi kwa baadhi ya weupe walio wengi.
Labda nishee experience yangu kidogo. Siku moja mimi na rafiki yangu tuliingia baa 'pub', tukaenda kujoin kwenye meza moja na wazungu, tulipokaa tu wale wazungu wakachukua vinywaji vyao wakaacha kula wakaenda kusimama kaunta tukaachwa peke yetu, nikajisemea moyoni kwanini kudhalilika kwenye nchi za watu namna hii.
Kwa kifupi kilichochangia mimi kurudi pamoja na mambo mengine ni tabia ya ubaguzi ya watu weupe iwe kwenye kazi au kwenye social affairs, kingine ni upweke (loneliness) hakuna jirani wa kukutembelea au kukusalimia asubuhi kama tulivyozoea huku bongo, vile vile hali ya hewa baridi 24/7 umevaa minguo saba vest, shati, koti, sweat na jaketi juu ilinishinda, nk nk.
Kizuri nilichojifunza kwao ni kwamba wazungu are hard working people, they keep time, they keep promises akikuahidi kitu juwa utapata akisema NO ni NO kweli kweli hata ulie machozi ya damu, kingine kizuri kwao hawachagui kazi, serikali zinaheshimu sana kodi, kwa UK huwezi kufanyakazi yeyote hata ya kufagia barabara kama huna (NI Number) National Insurance Number sisi tunaita TIN.
>Please, share with us your experience.
>S'il vous plaît partagez avec nous votre expérience.
>Bitte teilen Sie uns Ihre Erfahrungen mit.
>请与我们分享您的经验
>Qǐng yǔ wǒmen fēnxiǎng nín de jīngyàn.
>Vær venlig at dele din erfaring med os.
>Por favor, compartilhe conosco sua experiência
==================!
Karibu, Welcome, Bienvenu, Huānyíng/欢迎, Bemvinda, Witamy, أهلا بك, Herzlich Willkommen, स्वागत हे.