Tuliochaguliwa Livestock Training Institute (liti) Morogoro tukutane hapa

nkanga chief

JF-Expert Member
May 31, 2016
2,084
1,620
Kwa wale wote tuliochaguliwa chuo cha LITI, Morogoro tukutane hapa wadau tupeane taarifa mbalimbali.

Je??Kutakuwa na sponsorship mwaka huu?? Je tarehe ya kuripoti chuo lini??? Je join instruction zinapatikana wapi?
Karibuni wakongwe
 
Ni LIVESTOCK TRAINING AGENCY (LITA) na Sio Livestock Training Institute (LITI). LITI ni jina la zamani.
 
Moja kati ya upotevu mkubwa wa fedha ya umma ni uwepo wa hivi vyuo vya hovyo kabisa. Serikali inasomesha hawa watu halafu wanaishi kufanya kazi Vodacom na Breweries.

Tufikie sehemu tuwe na kozi za wakulima na sio maafisa kilimo. Tanzania inahitaji wakulima na wafugaji waliosoma. Ziwepo kozi za kuwafundisha wafugaji kufuga badala ya kozi za kufundisha maafisa mifugo ambao wakihitimu wanaanza SSK (Suti Safi Kibaruani) huku ufugaji unadodora kwa kukosa tija.....aaah, samahanini. Endeleeni kukutana
 
mmmmh hii kozi haina tija au
 
Kwa taifa, yes. Ila kama wewe ndio unaenda kusoma, ushauri wangu ukitoka huko, jitafutize mtaji kawekeze kwenye ufugaji. Hii serikali itawasomesheni kitu ambacho yenyewe haiamini katika hicho.
kwa hiyo kumbe hii kozi ni mzigo kwenye zoezi la ajira
 
Huo ni ukweli. LAKINI...ukitoka hapo na ukawa na uwezo wa kupata mtaji, hakika utakuwa milionea mkuu. Wafugaji wetu hawana elimu, wanabahatisha. Wewe utakayetoka hapo, ukiamua kufuga bila shaka utakuwa unajua nini unafanya. Lakini usiende kusoma hapo ukitaraji ajira, utakufa fukara mkuu.

Mimi nakushauri nenda kasome ukiwa na mawazo ya kujiajiri...wallah hutajuta. Utakuwa na uchumia imara miaka michache tu ya kufuga kwa tija na utaalam.
 
Moja kati ya upotevu mkubwa wa fedha ya umma ni uwepo wa hivi vyuo vya hovyo kabisa. Serikali inasomesha hawa watu halafu wanaishi kufanya kazi Vodacom na Breweries.

Tufikie sehemu tuwe na kozi za wakulima na sio maafisa kilimo. Tanzania inahitaji wakulima na wafugaji waliosoma. Ziwepo kozi za kuwafundisha wafugaji kufuga badala ya kozi za kufundisha maafisa mifugo ambao wakihitimu wanaanza SSK (Suti Safi Kibaruani) huku ufugaji unadodora kwa kukosa tija.....aaah, samahanini. Endeleeni kukutana

WACHA NIFUGE KUKU, MBUZI, KITI..... na MENGINEYO.
 
Huo ni ukweli. LAKINI...ukitoka hapo na ukawa na uwezo wa kupata mtaji, hakika utakuwa milionea mkuu. Wafugaji wetu hawana elimu, wanabahatisha. Wewe utakayetoka hapo, ukiamua kufuga bila shaka utakuwa unajua nini unafanya. Lakini usiende kusoma hapo ukitaraji ajira, utakufa fukara mkuu.

Mimi nakushauri nenda kasome ukiwa na mawazo ya kujiajiri...wallah hutajuta. Utakuwa na uchumia imara miaka michache tu ya kufuga kwa tija na utaalam.
mkuu hii certificate ya animal health and production inaweza kukupa ujuzi mkubwa kweli jinsi wanavyofundisha??
 
Of course. Sina mashaka na uwezo wa hivi vyuo.

Niliwahi kupita Tengeru, kitu niliona hapo roho iliniuma. Ng'ombe walioko pale sijawaona mahali pengine Tanzania. Nikajiuliza, sasa wanafundisha nini ikiwa hatupractise kwenye real life? Maana yafanywayo pale yakifanyika huko vijijini basi umaskini ungetoweka...jibu nikalipata HAKUNA DIRA.

Kwa hiyo ndugu yangu nenda kasome na uitumie hiyo fursa ya kupata maarifa vyema. Achana na serikali na akili za walimu utakaowakuta hapo kuhusu ajira. We soma, ukitoka hapo njoo upractise nje, hakika utakuwa na maisha yenye tija...njaa haitapita kwenye jamii yako
 
Back
Top Bottom