#COVID19 Tulioathiriwa na corona kwa namna moja au nyingine tukutane hapa

Panga Makalikuwili

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
291
432
Habari wana jamii

Namshukuru sana Mungu mpaka sasa sijaugua corona ingawa wataalamu wanasema unaweza kuwa nayo bila kutambua kutokana na uimala wa kinga yako.

Hata hivyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, corona imenigalagaza na kunichapa kimaisha vibaya sana.

Mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kupoteza ajira kutokana na athari za corona.. Nilipochukua pesa yangu NSSF nikaanzisha kibiashara fulani hivi, duuh nilijuta..kumbe watu hawakuwa na pesa mfukoni corona imewaumiza nikakosa wateja hivyo basi kibiashara kikafa.

Tangu hapo sasa ndio nikaonja joto ya jiwe .Ingawa kuna juhudi nafanya ili kujiweka sawa, lakini bado hali ngumu ndala waya. Unafuu unakuja taratibu sana.
 
Back
Top Bottom