Tulioajiriwa tunaweza kutatua tatizo la ajira kwa vijana wetu kama tutazingatia hili...

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wanabodi!

Ajira ni wimbo wa taifa huku mtaani kila unapokwenda. Graduates ni wengi mno kuanzia certificate , diploma , degree , Masters na PhD holders. Ni maelfu kwa maelfu ndugu zangu.

Kuna vijana wamekaa mtaani miaka nenda rudi bila ajira , wapo tu majumbani wanakula kwa kengere . Inaumiza mno.

Unamkuta mtu ana Msc ya Engineering , Uhasibu n.k yupo mtaani anasugua soli , amekata tamaa hataki hata kuona vyeti vyake. Wakati huohuo mtu anakuwa amesoma kwa shida na kwa magharama mengi sana , tena toka hizi familia duni.


Nini kifanyike?

Sisi ambao tumeajiliwa tupo wengi sana.. mathalani kwa serikali pekee kuna waajiliwa zaidi ya 450,000. Acha sasa sekta binafsi , acha ambao wamejiajili. Kimsingi tunafika Milioni 1.

Ukiwa umeajiliwa ukakopa hela kwa mshahara wako then ukachukua kijana 1 ambaye yupo mtaani ufanye nae kazi kwa makubaliano fulani , let say yeye anatoa utaalamu wake kama usimamizi , ufuatiliaji na wewe unatoa hela, then mwisho wa siku mnagawana hata 70 % kwa 30% monthly unakuwa tayari umemsaidia sana tu. Kwanza anapata confidence ya kuwa busy na kupata mahitaji yake madogo madogo then anawaza zaidi na zaidi.

Mfano mm nilikopa hela mahali, nikachukua vijana 2 , wanasimamia kilimo cha mbogamboga na mifugo huko shambani. Mwisho wa siku hawakosi kitu mfukoni and they are very happy yaan. Kwanza wanafanya closer supervision na wako very serious. Pia wananishauri vitu vingi sana vya kukuza project maana mostly nakuwa busy kazini.

Jamani jamani , kama umeajiliwa mchukue mwenzako umbebe kwenye projects zako. Mwisho wa siku unapunguza tatizo la ajira.

Tatizo la ajira ni issue mtambuko, siyo issue ya kuiachia serikali pekee wakuu. Hata huko Ulaya shida ya ajira ipo.

Asanteni.
 
kunywa usizidishe sana nitalipa.
Kwa point hizi naamini 28/Oct kura ni kwa Tundu Lissu.
 
Watanzania wamejaa wizi na uvivu hata ukimuajiri ataharibu. Sintosahau alichonifanyia Habiba Kibwana kwenye salon yangu.
 
Tatizo kuibiwa, kudhurumiwa.

Ni afadhari uajiri mtu asieenda shule, anaweza jitahidi kuwa mwaminifu.

Lakini kwa walioenda shule, wengi si waaminifu. Sababu wanataka kutajirika na kufanikiwa kwa haraka. Ili kuwapruvu wrong wote waliokuwa wanawabeza na kuwacheka kipindi wako broke

You know what am saying???
 
Back
Top Bottom