Tulinde heshima na maendeleo yetu: Tufanye mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulinde heshima na maendeleo yetu: Tufanye mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by siyabonga, Sep 30, 2012.

 1. s

  siyabonga Senior Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, ni wachache watakaopinga kuwa heshima na maendeleo yetu kama Taifa imeshuka na kwa hivi sasa tunadharaulika sana katika medani za Kimataifa na hasa na wageni ambao wako ndani na nje ya Nchi.

  Kwa madhumuni ya kulinda heshima na maendeleo yetu, ni lazima tufanye mabadiliko:

  Sababu ni nyingi, kwa nikiwa kumbusha tu, ni pamoja na:-

  1. Kukosa na viongozi makini wa kisiasa , badala yake waliopo ni wenye upeo mdogo sana wa uongozi na kushindwa kulinda na kutetea maslahi ya Taifa.
  2. Viongozi wakuu wa kisiasa kununuliwa kwa bei ndogo na kuingizwa katika mabodi ya makampuni ya kigeni kama wenyeviti na wajumbe. Hawa ni pamoja na viongozi wakuu wa kitaifa wakiwamo wastaafu.
  3. Kushindwa kuchukua hatua za kimaamuzi na kiutawwala hata kwa masuala yalio wazi hata kwa mtu mwenye upeo mdogo kabisa.
  4. Kukiri hadharani kutojua chanzo cha tatizo la umaskini, Wenye akili wanaelewa kuwa kujua chanzo cha tatizo ni sawa kuwa tayari umelitatua kwa 50%
  5. Kuwatetemekea na kushindwa kuwachukulia hatua wageni hata pale wanapofanya ya ovyo: Mfano Mzungu mwizi wa madini, Agha Khan Hospital kugoma kuwatibu watu wa bima ya Afya, na mengine mengi.
  6. Viongozi kuwa malimbukeni wa starehe na safari za Nje.

  Wakuu, unaweza kuongeza mengi mengine. Kama Taifa, njia peke ya kujinusuru ni kufanya mabadiliko sasa. Tuchague vizuri 2015.
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Hii yote ni kwa sababu ya utawala mbovu wa serikali ya ccm. Mazuri machache yaliyopo yamefanywa na serikali ya ccm kwa kusukumwa na ukosoaji wa vyama vya upinzani, mabaya yoooooooooooooote yaliyopo yamefanywa na serikali ya ccm kwa ubia mkubwa kabisa na mafisadi na wawekezaji wezi. Mabadiliko hayaepukiki, hatuwezi kupata mabadiliko ya kimaendeleo kama Taifa kama ccm ipo madarakani. Kwa hiyo tuiondoeni madarakani ccm, kama tunataka mabadiliko chanya.
   
Loading...