Tunkamanin
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 955
- 866
Hii ndio Tanzania nchi ya maziwa na asali yenye watu wanaoitwa watanzania.....watu hawa in wagumu sana kuwaelewa labda nikupe tu utambulisho wao hawa jamaa ni vigeugeu vinyonga na hawaeleweki wanataka nini, pengine nao hawajui wanataka nini, ni watu wa kulalamika sana. Wakipigwa na jua jasho likawatoka utawasikia jamani mbona mungu haleti mvua?,ukame umezidi joto Kali umeme shida mazao Hakuna basi baada ya nusu saa mvua inaanza kunyesha mtanzania yuleyule ataanza kulalamika "hizi mvua ziangaliege mahali pa kunyesha bwana badala ya kunyesha mashambani huko inakuja kunyesha huku mjini" mvua inaharibu madili yetu yaani hapa ishaleta nuksi" na matusi kadha Wa kadha hao ndio watanzania. Kushadadia mambo hata kama madogo kuyakuza na fitna ndio hasa raha yetu. President kikwete enzi zake alishadadawa sana kwa mambo madogo mno watu wakayakuza na kuyakuza rejea sakata la EPA ESCROW Teuzi za upendeleo kwa waislam sakata la mgomo Wa madaktari nk. Maamuzi yake tuliyakejeli tukayaona dhaifu cc mnyika J na dkt slaa. Tukaomba mungu atupe raisi mwenye chembe ya udikteta mkali na mwenye uthubutu. Ishu ya dawa tukajaza server hapa na pale juu kuna sticky thread ya mambo hayo tu... Alilaumiwa Jk dhaifu majina ya mapapa Wa madawa ameyaficha na kagoma kutaja. Akaibuka binti Wa watu AMINA CHIFUPA AKAJITOA SADAKA AKATOA AHADI YA KUWATAJA WOTE WANYE KUHUSIKA NA HUU MCHEZO MCHAFU. HAKUCHUKUA RAUNDI WAKAMNANIHIII ALLAH AMREHEMU HUKO ALIPO ALITHUBUTU. TUKAONGEA SANA ENZI ZILE SOTE TUKILAANI NA KUOMBA ATOKEE MKOMBOZI. MUNGU HAMFICHI MNAFIKI AKATULETEA KIBAHATIBAHATI JPM, NA JPM BILA KUPEPESA MACHO AKAMBANDIKA JIJI LETU PAUL MAKONDA...SASA MAKONDA AMEAMUA KUIENZI KAZI YA AMINA CHIFUPA KWA KUJITOA MUHANGA KABISA MAISHA YAKE. AMEJITOA SADAKA KUPAMBANA NA WATU HAWA WATANZANIA HAWAHAWA WAMEMGEUKA AAH HATAJI WAKUBWA ANATAJA VIJITEJA TU. UTADHANI WAYASEMAYO YANATOKA MOYONI VILE; MAKONDA AKAWALIPUA KWELI NCHI NZIMA IKAZIZIMA TUKAONA KILA AINA YA WATU WAKIJITOKEZA KULA SAHANI MOJA NA MZALENDO WA KWELI MAKONDA. WA TZ KAMA ILIVYOKAWAIDA YA UKIGEUGEU TUKAGEUKA TENA HATUTAKI WATAJWE MAANA WANADHALILISHWA AAH HAPANA MADAWA SI MUHIMU SISI TUNATAKA VYETI....AAH HAPANA ANAVAMIA VITUO VYA HABARI MARA ATAPINDUA NCHI AFUKUZWE. HAYA NDIO TUNAYOYAONA MTANDAONI SIJUI KATIKA MAISHA YAKE YA KAWAIDA HUYU MAKONDA WANAMTEGA MARA NGAPI KWA SIKU KUMMALIZA. KWA NGUVU ZA GIZA? KWA BUNDUKI? KWA SUMU? KWA KASHFA AU KWA ......MI SIJUI ILA WALE WALINZI UNAOTEMBEA NAO HAWAKUTOSHI ONGEZA WENGINE NA UWE UNAENDA NAO HATA ITV TBC MAANA UNAWINDWA SANA. AMINA CHIFUPA....PUMZIKA KWA AMANI MAKONDA ANAITENDEA HAKI ILE AZMA YAKO. TEAM MAKONDAJPM. HAPA KAZI TU VYETI PELEKENI KLINIKI